DAR ES SALAAM
Waziri Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na Walemavu Jenista Mhagama ametembelea mradi wa ujenzi wa daraja la Kigamboni ambapo amehimiza kuharakishwa ujenzi wa mradi huo ili kuwapunguzia wananchi adha ya usafiri pamoja na kupunguza msongamano katika jiji la Dar es salaam.
Katika Ziara hiyo aliyoongozana na Naibu Waziri wa Wizara hiyo Anthony Mavunde Waziri Muhagama amesema msongamano katika jiji la Dar es salaam umekuwa ni tatizo kubwa linalosababisha Serikali kukosa mapato kutokana na muda mwingi kupotea katika foleni za barabarani,
Kwa Upande wake Mhandisi wa Mradi huo kutoka Shirika la Hifadhi ya Jamii NSSF Mhandisi Msemo amesema mradi huo uliotakiwa ukamilike tangu january mwaka huu ulishindwa kukamuilika kutokana na changamoto mbalimbali na kuahidi kuukamilisha mapema mwakani.
Mradi wa Ujenzi wa Daraja la Kigamboni unaotekelezwa na Mfuko wa Hifadhi ya jamii NSSF pamoja na Serikali umegharimu zaidi ya Dola za Kimarekani milioni 143.5
No comments:
Post a Comment