Rais wa Nigeria, Mohammadu Buhari, ameiambia BBC kuwa majeshi yake yanakaribia kulishinda kundi la kiislam , Boko Haram. Rais Buhari ameeleza kuwa kundi hilo halina uwezo tena wa kufanya mashambulizi dhidi ya majeshi ya serikali ama maeneo yenye mkusanyiko mkubwa wa watu na kwamba visa vya kujitoa muhanga vimepungua .
Buhari ameeleza kuwa kundi hilo awali lilikuwa na umoja ingawa kwa sasa limesambaratishwa vibaya katika majimbo ya Adamawa na Yobe na kusalia katika jimbo la Borno ambayo ndiyo ngome yao kuu .
Boko Haram wanaripotiwa kuendesha mashambulizi zaidi ya mia moja na kuua watu zaidi ya elfu moja katika kipindi cha miezi miwili iliyopita .
Ikumbukwe kwamba ,wakati wa kampeni zake kuelekea uchaguzi nchini Nigeria,Rais Buhari alitoa ahadi ya kupambana na kundi la Boko Haram mpaka kufikia mwisho wa mwaka huu.
No comments:
Post a Comment