Habari za Mahusiano Kila siku
JOURNALISM STUDENTS AT ETC COLLEGE
ETC RADIO ONLINE LIVE
http://wwweckrosnewsblogspo.radio12345.com/
VIONGOZI CHAMA CHA WALIMU CWT MKOANI NJOMBE WAPATIWA MAFUNZO YA UONGOZI
Tuesday, December 29, 2015
Walimu mkoani njombe wametakiwa kuwaandaa wanafunzi mashuleni kwaajili ya kunufaika na uwekezaji mkubwa wa madini yaliganga na mchuchuma wilayani ludewa kutokana na tathmini kuonyesha kuwa migodi hiyo miwili itahitaji wafanyakazi wengi ambao ni wazawa na wenye ujuzi
Aidha walimu wenyewe wametakiwa kujiandaa na uwekezaji huo kwa kufanya shughuli mbalimbali za ujasilia mali kama kilimo na ufugaji kufuatia kundi kubwa la wageni ambao watahitaji bidahaa mbali kama mifugo na mazao ya chakula
ushauri huo umetolewa na mkuu wa mkoa njombe dkt rehema nchimbi wakati akifungua semina elekezi kwa viongozi wa chama cha walimu mkoa wa njombe CWT Ambapo amesema kuwa zaidi ya wafanyakazi wazawae lfu 50 watanufaika na ajira huku idadi ya wageni kutoka nchini china ikiwa elfu sita ambao watahitaji bidhaa mbalimali kutoka kwa wenyeji
Mmoja wa wakufunzi katiaka semina hiyo ya siku tatu mwalimu Issa Ally Ngayama ambaye Katibu wa Chama Cha Walimu Tanzania CWT Mkoa wa Morogoro amewataka alimu hao kuacha kujigawa kwa kuanzisha vyama vya walimu nje ya CWT kwa kuwa kufanya hivyo kutapelekea wao kushindwa kupata haki zao kutoka kwa mwajiri na badala yake waendelee kuunga mkono jitihada mbalimbali zinazofanywa na chama cha walimu Tanzania CWT
Washiriki wa semina hiyo wakiwemo wenyeviti wa chama hicho wilaya za makete na ludewa mbele ya mkuu wa mkoa njombe wameendelea kupaza sauti dhidi ya kero zinazowakabili walimu huku wakionyesha kusikitishwa na kitendo cha serikali wilayani ludewa kuwatoza kodi za nyumba walimu jambo ambalo linarudisha nyuma jitihada za kukuza elimu wilayani humo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment