ECKROS SCHOOL OF JOURNALISM

eckroscollege. Powered by Blogger.

Blogroll

About

Habari za Mahusiano Kila siku

JOURNALISM STUDENTS AT ETC COLLEGE

JOURNALISM STUDENTS AT ETC COLLEGE

ETC RADIO ONLINE LIVE

http://wwweckrosnewsblogspo.radio12345.com/

Wateja wa Airtel kushinda mamilioni ya pesa kupitia promosheni ya “Airtel MKWANJIKA”

Thursday, December 17, 2015





Meneja uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando pamoja na Meneja Masoko wa Airtel Bi Anethy Muga kwa pamoja wakizindua promosheni mpya ya “Airtel MKWANJIKA” itakayowawezesha wateja wote wa Airtel nchi nzima kujishindia mamilioni ya pesa taslimu kila siku.

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imezindua promosheni kabambe ijulikanayo kama “Airtel MKWANJIKA” itakayowazawadia wateja wote wa Airtel nchi nzima hadi kiasi cha shilingi milioni 300 pesa taslimu.

Promosheni ya “Airtel MKWANJIKA” itawawezesha wateja wote wanaojinga na kifurushi chochote cha yatosha au kuongeza muda wa maongezi wa kiwango chochote kwenye simu zao kuingia kwenye droo na kupata nafasi ya kujishindia.

Kila siku wateja watakaoongeza salio wataingizwa kwenye droo ya “Airtel MKWANJIKA” ambapo washindi wanne wataibuliwa na kutakiwa kuingia katika sanduku la pesa la Airtel (Airtel Mkwanjuka Boksi) na kujikusanyia pesa hadi kiasi cha shilingi milioni moja ndani ya dakika moja

Akizindua promosheni hiyo,Meneja Masoko wa Airtel, Bi Anethy Muga alisema” tumezindua promosheni hii mwisho wa mwaka ili kuwawezesha wateja wetu kujishindia zawadi zitakazobadili maisha yao katika msimu huu wa sikukuu. Tumeshuhudia tulivyoweza kubadili maisha ya watanzania kupitia promosheni zetu zilizopita na leo tunaamini promosheni ya “Airtel MKWANJIKA” ni fulsa nyingine itakayoboresha maisha ya wateja wetu wengi..”

“Airtel tunaamini wakati wa wateja wetu kutimiza ndoto zao ni sasa, hivyo tunawahamasisha kuendelea kufurahia huduma zetu bora huku tukiwazawadi mamilioni ya pesa kupitia “Airtel MKWANJIKA”. Huu ni wakati wako sasa wakutumia mtandao wa Airtel kama bado hujajiunga” alisema Muga

Akiongea kuhusu promosheni hiyo, Meneja Uhusiano, Bwn Jackson Mmbando alisema” wateja wanaotumia mtandao wa Airtel wanaongezeka kila siku, tunaposherehekea kwa pamoja msimu huu wa sikukuu tunamuwezesha mteja yeyote atakaye jiunga na kifurushi chochote cha yatosha au kuongeza salio kwa kutumia vocha kuingizwa moja kwa moja kwenye droo ya siku inayofata ya promosheni hii ya “Airtel MKWANJIKA”.

Mmbando alisisitiza promosheni hii ni kwa wateja wote wa Airtel, hakuna gharama ya ziada, ili kushiriki unachotakiwa kufanya ni kujiunga na yatosha au kuongeza salio na vocha. Tunapenda kuwajulisha wateja wetu kuwa washindi wote watatangazwa kupitia vyombo mbalimbali vya habari na washindi pia watapigiwa simu kutoka kwenye namba 0683-442244 kwaajili ya kuchukua zawadi zao. Hakuna tozo ya aina yoyote mteja atakayotakiwa kulipa. Airtel inapenda kuwatahadharisha wateja kuwa waangalifu na taarifa ambazo si sahihi wakati wote wa promosheni.

“washindi wote watakao patikana wakati wote wa promosheni wapatiwa kiasi cha pesa alichoweza kujikusanya na kushinda kutoka kwenye kisanduku cha pesa kupitia huduma ya Airtel Money. Droo za promosheni hii ni za kuvutia kushiriki kwani uwezo wa mteja kukusanya pesa ndio unaomuhakikishia kiasi cha pesa taslimu atakachojishindia” aliongeza Mmbando.

Droo ya kwanza ya promosheni ya “Airtel MKWANJIKA” itafanyika tarehe 23 Desemba na nyingine nyingi zaidi kufanyika Januari 2016 na kuendelea.

Washindi wote watapigiwa simu na wafanyakazi wa Airtel kutoka kwenye namba 0683-442244 na kuwajulisha ushindi na siku ya kupokea zawadi zao. Zawadi itatolewa kwa mteja ambaye jina lake litafanana na usajii wa namba yake pamoja na kitambulisho chake

Masanduku ya pesa yatawekwa katika maeneo ya miji mikubwa na washindi walioko maeneo hayo watatakiwa kuja mjini ili kuzungusha sanduku na kukusanya pesa za ushindi

Washindi wote watatakiwa kuchukua zawadi zao kabla ya tarehe 30 Machi 2016

No comments:

Post a Comment

 

Most Reading

Eckros Computer Lap 1

Eckros Computer Lap 1

About ETC College

Eckros Tourism College (ETC) started admitting the first intake of students in January 2013. The college falls under tertiary higher education and training as stipulated in education and training policy of 1995.
Also the college administer Distance Learning Programmes, Evening classes, weekend classes, study tours and researchs programmes
Admission Process
New admission into the College is effected twice a year in January-July and July-December.

WALIO PITIA BLOG YETU