ECKROS SCHOOL OF JOURNALISM

eckroscollege. Powered by Blogger.

Blogroll

About

Habari za Mahusiano Kila siku

JOURNALISM STUDENTS AT ETC COLLEGE

JOURNALISM STUDENTS AT ETC COLLEGE

ETC RADIO ONLINE LIVE

http://wwweckrosnewsblogspo.radio12345.com/

Trump akiri kwamba anachunguzwa Marekani

Saturday, June 17, 2017

Donald TrumpHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionDonald Trump amekana tuhuma kwamba maafisa wake walishirikiana na maafisa wa Urusi
Rais wa Marekani Trump amethibitisha kwamba anachunguzwa yeye binafsi kutokana na hatua yake ya kumfuta kazi mkuu wa Shirika la Uchunguzi wa Jinai la Marekani FBI James Comey.
Kupitia Twitter, Bw Trump amekariri kwamba uchunguzi unaoongozwa na
mwendesha mashtaka maalum kuhusu tuhuma kwamba maafisa wa Urusi waliingilia uchaguzi wa mwaka 2016 ili kumfaa Trump hauna msingi.
Ni mara ya kwanza kwa Bw Trump kuzungumzia taarifa kwenye magazeti kwamba anachunguzwa kwa tuhuma za kuhujumu mifumo ya haki kwa kumfuta kazi Bw Comey.
Awali, taarifa kwenye vyombo vya habari Marekani vilikuwa vimeripoti kwamba wasaidizi wake pamoja na watu waliojitolea kusaidia katika kundi lake la mpito wameamrishwa kuhifadhi nyaraka zote kuhusiana na uchunguzi huo wa madai kuhusu Urusi.
Taarifa zinasema mawakili wa maafisa hao wa Trump wametakiwa kuhifadhi nyaraka zote zinazohusiana na Urusi, Ukraine na washauri wengine kadha wa kampeni.
Kuna makundi kadha yanayofanya uchunguzi, kundi moja likiongozwa na mkurugenzi wa zamani wa FBI Robert Mueller, ambayo yanachunguza iwapo maafisa wa Trump walishirikiana na maafisa wa Urusi wakati wa kampeni.
Bw Trump amekana tuhuma hizo.

No comments:

Post a Comment

 

Most Reading

Eckros Computer Lap 1

Eckros Computer Lap 1

About ETC College

Eckros Tourism College (ETC) started admitting the first intake of students in January 2013. The college falls under tertiary higher education and training as stipulated in education and training policy of 1995.
Also the college administer Distance Learning Programmes, Evening classes, weekend classes, study tours and researchs programmes
Admission Process
New admission into the College is effected twice a year in January-July and July-December.

WALIO PITIA BLOG YETU