ECKROS SCHOOL OF JOURNALISM

eckroscollege. Powered by Blogger.

Blogroll

About

Habari za Mahusiano Kila siku

JOURNALISM STUDENTS AT ETC COLLEGE

JOURNALISM STUDENTS AT ETC COLLEGE

ETC RADIO ONLINE LIVE

http://wwweckrosnewsblogspo.radio12345.com/

Rais Magufuli Kuanza Ziara Mkoani Simiyu Kesho Septemba 08

Friday, September 7, 2018

Na Stella Kalinga, Simiyu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli atafanya ziara ya siku tatu (03) Mkoani Simiyu, kuanzia kesho tarehe 08/09/2018 hadi tarehe 10/09/2018, Mkoani Simiyu.

Akizungumza na Waandishi wa habari ofisini kwake Mkuu wa Mkoa Mhe. Anthony Mtaka amesema Mhe. Rais akiwa mkoani Simiyu atapata nafasi ya kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo, kuweka mawe ya msingi, kufungua pamoja na kuzungumza na Wananchi kupitia mikutano ya hadhara.

Mtaka amesema siku ya Jumamosi tarehe 08/09/2018, Mhe. Rais atakagua na kuweka jiwe la msingi Ujenzi wa Mradi wa Maji wa Lamadi uliopo wilayani Busega na baadaye, ataelekea wilayani Bariadi.

Aidha, amesema Mhe. Rais akiwa katika Wilaya ya Bariadi, atafungua Jengo la Wagonjwa wa Nje(OPD) Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu, atakagua na kufungua barabara za lami (kilomita 6.9) zilizojengwa chini ya mradi wa kuboresha Miundombinu ya Miji (ULGSP).

“Siku hiyo pia atakagua maendeleo ya Ujenzi wa  barabara ya Bariadi-Maswa inayojengwa kwa kiwango cha lami na kuweka jiwe la msingi. Mhe.Rais atapokea salamu za Chama Cha Mapinduzi, salamu za Wilaya, Mkoa, taarifa ya mradi wa ujenzi wa barabara na baadaye kuzungumza na Wananchi wa Mkoa wa Simiyu na Watanzania wote kwa ujumla, katika Mtaa wa Salunda kwenye Viwanja vya Shule ya Msingi Salunda.”

“Tarehe 09/09/2018 Mhe. Rais atazungumza na wananchi wa wilaya ya Itilima eneo la Makao Makuu ya Wilaya (Lagangabilili) na kuelekea wilayani Meatu. Akiwa njiani kuelekea Meatu Mhe. Rais atapata fursa ya kusalimia wananchi wa Kijiji cha Mwandoya na baadaye atafungua Miundombinu ya Uboreshaji wa Huduma za Afya Hospitali ya Wilaya ya Meatu na kuzungumza na wananchi katika Viwanja vya Stendi ya Mwanhuzi” alisema Mtaka.

Ameongeza kuwa Siku ya Jumatatu tarehe 10/09/2018 Mhe. Rais Magufuli atahitimisha ziara yake Mkoani Simiyu kwa kuweka jiwe la msingi ujenzi wa daraja la Mto Sibiti linalounganisha Mkoa wa Simiyu na Singida na baadaye  kuwasalimia wananchi.

Katika hatua nyingine Mtaka ametoa wito kwa wananchi wote mkoani Simiyu hususani katika Miji ya Lamadi, Bariadi, Lagangabilili, Mwanhuzi na vitongoji vyake kujitokeza kwa wingi katika maeneo yote ambayo Mhe. Rais Magufuli atapita na kufanya mikutano ya hadhara.

No comments:

Post a Comment

 

Most Reading

Eckros Computer Lap 1

Eckros Computer Lap 1

About ETC College

Eckros Tourism College (ETC) started admitting the first intake of students in January 2013. The college falls under tertiary higher education and training as stipulated in education and training policy of 1995.
Also the college administer Distance Learning Programmes, Evening classes, weekend classes, study tours and researchs programmes
Admission Process
New admission into the College is effected twice a year in January-July and July-December.

WALIO PITIA BLOG YETU