ECKROS SCHOOL OF JOURNALISM

eckroscollege. Powered by Blogger.

Blogroll

About

Habari za Mahusiano Kila siku

JOURNALISM STUDENTS AT ETC COLLEGE

JOURNALISM STUDENTS AT ETC COLLEGE

ETC RADIO ONLINE LIVE

http://wwweckrosnewsblogspo.radio12345.com/

WAZIRI WA NISHATI DK.MEDARD KALEMANI ATEMA CHECHE MKOANI NJOMBE

Saturday, September 1, 2018


Na Chrispin kalinga.
Waziri wa Nishati DK.MEDARD KALEMANI amewataka Viongozi na wadau wa nishati kuwasaidia wananchi hususani wakazi wa mkoa wa Njombe kutunza vyanzo vya maji ili

kuwezesha ukuzaji wa mto kilombero unaolisha maji yake mto Rufiji maalumu kwa mradi wa kuzalisha umeme wa rufiji wenye uwezo wa kuzalisha umeme takribani MW.2,1OO.

Waziri KALEMANI ameyasema hayo wakati wa mkutano wa uelewa wa mradi wa kuzalisha umeme wa rufiji (rufiji hydropower project) uliofanyika katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Njombe ulio wakutanisha wadau mbali mbali wakiwemo wabunge na  viongozi wa halmashauri za mkoa wa Njombe.

Aidha dk.kalemani amesema kuwa serikali ya awamu ya tano imeamua kutekeleza mradi huo mkubwa wa mda mrefu ulionza kubuniwa tangu serikali ya awamu ya kwanza na leo umeanza kutekelezwa ukiwa na zaidi ya miaka 40 huku sababu kubwa ikiwa ni kuongezeka kwa matumizi makubwa ya umeme nchini.

Kalemani ameongeza kuwa licha ya hali ya umeme kwa sasa kuwa bora kwa kuwa na umeme wa ziada megawati 201 lakini haiwezi kutoshereza katika mahitaji ya uchumi wa viwanda ndio maana serikali imeamua kuongeza uzalishaji wa umeme mwingi na wakutosha  ambao ghalama yake ni naafuu licha ya serikali kuendelea kuzalisha umeme mchanganyiko ukiwemo wa gesi.

Kwa upande wake kaimu mkuu wa mkoa wa Njombe ALLY KASINGE licha ya kupongeza jitihada za kuanza mradi huo mkubwa wa umeme nchini, amesema kuwa ikiwa Njombe ni miongoni mwa mikoa yenye vyanzo vingi vya maji yanayolisha mto rufiji wanayosababu ya kushiriki kikamilifu katika utunzaji wa vyanzo hivyo vya maji ili kusadia juhudi za wizara katika kufikia umeme wa kutosha kuelekea uchumi wa viwanda





mubashara blog +255753121916

No comments:

Post a Comment

 

Most Reading

Eckros Computer Lap 1

Eckros Computer Lap 1

About ETC College

Eckros Tourism College (ETC) started admitting the first intake of students in January 2013. The college falls under tertiary higher education and training as stipulated in education and training policy of 1995.
Also the college administer Distance Learning Programmes, Evening classes, weekend classes, study tours and researchs programmes
Admission Process
New admission into the College is effected twice a year in January-July and July-December.

WALIO PITIA BLOG YETU