ECKROS SCHOOL OF JOURNALISM

eckroscollege. Powered by Blogger.

Blogroll

About

Habari za Mahusiano Kila siku

JOURNALISM STUDENTS AT ETC COLLEGE

JOURNALISM STUDENTS AT ETC COLLEGE

ETC RADIO ONLINE LIVE

http://wwweckrosnewsblogspo.radio12345.com/

Rais Magufuli atuma salamu za rambirambi Ajali ya Basi la New Force Iringa

Saturday, December 19, 2015


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Iringa Bi. Amina Masenza kufuatia ajali ya basi la kampuni ya New Force kugongana na lori, na kusababisha vifo vya watu 12, na wengine 15 kulazwa Hospitali.

Ajali hiyo imetokea tarehe 18 Desemba, 2015 Majira ya saa nane mchana katika Kijiji cha Mahenge, Wilaya ya Kilolo Mkoani IRINGA ambapo Basi la kampuni ya New Force lenye namba T 483 CTF lililokuwa limebeba abiria 49 limegongana na Lori la Kampuni ya Reign-ford Limited lenye namba T 616 BEF na Tela lake lenye namba T 320 DEF lililokuwa na shehena ya mbao .

Rais Magufuli amemuomba Mkuu huyo wa mkoa kufikisha salamu za pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki wote ambao wamepoteza ndugu zao katika ajali hiyo mbaya

"Nimesikitishwa sana na kutokea kwa ajali hii, ninawapa pole nyingi wote waliopoteza ndugu zao na ninawaombea Majeruhi wote wapone haraka ili waungane na familia zao na kuendelea na shughuli zao za maendeleo" amesema Rais Magufuli.

Amewaombea marehemu wote kwa Mwenyezi Mungu ili azipumzishe roho zao mahali pema peponi, Amina.

Aidha Dkt. Magufuli ametoa wito kwa watumiaji wote wa barabara hususani madereva kuwa waangalifu waendeshapo vyombo vya usafiri na amewakumbusha wananchi wanaotumia barabara kwa kusafiri ama kusafirisha mizigo kutoa ushirikiano kwa vyombo husika pale wanapobaini kuwepo vitendo ambavyo ni chanzo cha ajali.

Imetolewa na;  
Gerson Msigwa,
 Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
18 Desemba, 2015

No comments:

Post a Comment

 

Most Reading

Eckros Computer Lap 1

Eckros Computer Lap 1

About ETC College

Eckros Tourism College (ETC) started admitting the first intake of students in January 2013. The college falls under tertiary higher education and training as stipulated in education and training policy of 1995.
Also the college administer Distance Learning Programmes, Evening classes, weekend classes, study tours and researchs programmes
Admission Process
New admission into the College is effected twice a year in January-July and July-December.

WALIO PITIA BLOG YETU