ECKROS SCHOOL OF JOURNALISM

eckroscollege. Powered by Blogger.

Blogroll

About

Habari za Mahusiano Kila siku

JOURNALISM STUDENTS AT ETC COLLEGE

JOURNALISM STUDENTS AT ETC COLLEGE

ETC RADIO ONLINE LIVE

http://wwweckrosnewsblogspo.radio12345.com/

COSOTA, CMEA kuanza kulipa wanamuziki mirahaba Januari 2016

Monday, December 21, 2015


Chama cha Hakimiliki Tanzania (COSOTA) kwa kushirikiana na kampuni ya kusimamia kazi za wanamuziki nchini Copyrights Management East Africa Limited (CMEA) wataanza kulipa mirabaha ya wanamuziki na wadau wake kuanzia mwakani.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Cosota, Doreen Sinare alisema kuwa wanamuziki, watunzi na ma’producer’ watalipwa asilimia 60 kwa kila wimbo au video itakayochezwa katika redio na televisheni yoyote ndani na nje ya nchi kwa kutumia vifaa bora vilivyowekwa na kampuni ya CMEA.

Doreen alisema kuwa manamuziki, msanii alitakiwa kupata asilimia 70 ya kazi yake, lakini asimilia 10 itakatwa katika malipo hayo na kuingia katika mifuko ya jamii kwa mahitaji yake ya baadaye.

Alisema kuwa wanamuziki ni sawa na wafanyakazi wengine na asilimia 10 hiyo itamwezesha kujipatia kipato chake kama ilivyo kwa wafanyakazi wengine katika taasisi mbalimbali.

Kwa mujibu wa Sinare alisema kuwa ili kuhakikisha kila mwanamuziki anafaidika na kazi yake, watashirikiana na vyama vingine vya Hakimiliki katika nchi mbali mbali kwa kutumia hati ya malipo zinazotokana na bei za matangazo kwa televisheni na vituo vya redio.

Alisema kuwa Cosota na CMEA pia watawapa ushirikiano vyama hivyo ili nao waweze kupata haki za malipo ya wanamuziki wao kwa vituo vya televisheni na redio vitakavyotumia kazi za wanamuziki wa nje.

“Lengo la Cosota na CMEA ni kuona wasanii wanafaidika na kazi zao, mirabaha ya kwanza tutaanza kulipa Januari 2 na kwa sasa tupo katika hatua za mwisho kukamilisha jinsi tutavyolipa, ndiyo maana tumetoa semina kwa wanamuziki, lengo ni kuwahamasisha kujisajili,” alisema Sinare.

Afisa Mtendaji Mkuu wa CMEA, Paul Matthysse alisema kuwa mbali ya wanamuziki, kampuni yao itawawezeha pia watayarishaji wa muziki na wasanii wengine pamoja na vyombo vya habari kupata kufahami takwimu sahihi za nymbo zilizochezwa kwa siku, wiki, mwezi na kwa mwaka.

Matthysse alisema kuwa kampuni yao imewekeza mitambo ya kisasa inayowezesha kuchapisha na kuhakiki nyimbo pindi zinapochezwa hewani na televisheni na redio na kutoa ripoti za aina mbalimbali zinazohitajika kutumika kwa malengo maalum.

“Pia tunapokea na kuhifadhi nyimbo kwenye mitambo maalum kwa matumizi ya uhakiki, na kudhibiti kiasi cha mirabaha ambacho Cosota kupitia vyombo vya habari inatakiwa kuwalipa wasanii kulingana na idadi kamili ya urushwaji wa kazi zao,” alisema Matthysse.

Alisema kuwa wanamuziki na wasanii wengine ambao hawatakuwa na usajili, watakosa haki zao pamoja na CMEA kuendelea kurekodi kazi zao zinazochezwa katika redio na televisheni mbali mbali. “Ni muhimu kwao kujisajili, kutojisajili ni kupoteza haki zao zinazotokana na kazi yako,” alisisitiza.

No comments:

Post a Comment

 

Most Reading

Eckros Computer Lap 1

Eckros Computer Lap 1

About ETC College

Eckros Tourism College (ETC) started admitting the first intake of students in January 2013. The college falls under tertiary higher education and training as stipulated in education and training policy of 1995.
Also the college administer Distance Learning Programmes, Evening classes, weekend classes, study tours and researchs programmes
Admission Process
New admission into the College is effected twice a year in January-July and July-December.

WALIO PITIA BLOG YETU