Takriban watu 25 wameuwa na zaidi ya 100 kujeruhiwa kwenye mkasa wa moto katika hospitali moja iliyo mji wa Jazan nchini Saudi Arabia.
Moto huo ulitokea katika gorofa ya pili ya hospitali ya jazan ambapo vyumba vya kujifungua na vile vya wagonjwa mahututi vipo mapema leo Alhamisi .
Walionusurika na majeruhi wamehamishwa kupelekwa katika hospitali zingine.
Haijabainika kile kilicho sababisha moto huo na sasa uchunguzi unandelea .
Huduma za dharura sasa zimeuzima moto huo.
Picha za tukio hilo zilizochapishwa kwenye jarida la kila siku la Okaz zinaonesha mabaki ya hospitali hiyo yaliyotekekea na kuharibika kabisa.
Mji wa wa Jazan uko karibu na mpaka wa Saudia na Yemen taifa ambalo limesakamawa na vita kati wenyewe kwa wenyewe.
Jeshi la Saudia linasaidia majeshi ya serikali ya Yemen kupamabana na uasi ulioanzishwa na kundi la waasi wa Houthi.
Mapema mwezi huu kombora lililokuwa likielekea Jazan lilidunguliwa na majeshi ya Saudia hata hivyo hivyo haijabainika kufikia sasa iwapo moto huo unauhusiano wowote na mapigano yanayoendelea huko Yemen.
No comments:
Post a Comment