ECKROS SCHOOL OF JOURNALISM

eckroscollege. Powered by Blogger.

Blogroll

About

Habari za Mahusiano Kila siku

JOURNALISM STUDENTS AT ETC COLLEGE

JOURNALISM STUDENTS AT ETC COLLEGE

ETC RADIO ONLINE LIVE

http://wwweckrosnewsblogspo.radio12345.com/

HABARI YA HIVI PUNDE:..SERIKALI YA UMOJA WA KITAIFA (SUK) ZANZIBAR YAVUNJIKA RASMI, DR. SHEIN AACHWA PEKEYAKE

Saturday, December 19, 2015






Zanzibar. Wakati mazungumzo ya kutatua mgogoro wa kisiasa Zanzibar yakiendelea, utendaji wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK), unaonekana kuparaganyika baada ya mawaziri wa CUF kususia kazi, wakidai Serikali hiyo imeshamaliza muda wake.
SUK ni matokeo ya maridhiano kati ya chama tawala CCM na CUF na ilianza kufanya kazi mwaka 2010, lakini uamuzi huo wa chama hicho kikuu cha upinzani unamaanisha kuwa SUK sasa inafanya kazi kwa mawaziri kutoka upande mmoja tu.
Zanzibar, ambayo ilifanikiwa kumaliza mgogoro wa kisiasa ulioibuka katika chaguzi za mwaka 2000 na 2005, iliingia tena kwenye mgogoro Oktoba baada ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (ZEC), Jecha Salum Jecha kufuta matokeo ya urais wa visiwa hivyo na ujumbe wa Baraza la Mawakilishi kwa madai ya sheria na taratibu kutofuatwa, wajumbe wa ZEC kutofautiana na mmoja wa wagombea kujitangaza mshindi na akaahidi kuitisha uchaguzi mwingine ndani ya siku 90.
Kwa sasa imekuwa ikiripotiwa kuwa Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein na Makamu wake wa Kwanza, Maalim Seif Sharif Hamad ambao waliogombea urais wamekuwa wakiendelea na mazungumzo kuhusu suala hilo lakini hayajawekwa bayana.
Akizungumza kwa niaba ya wenzake kutoka CUF, Said Ali Mbarouk alidai Serikali imewaingizia mishahara kinyemela, kitu alichosema si halali.
Mbarouk, aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo, alisema wameshaandika barua Wizara ya Fedha ya Zanzibar iwape namba ya akaunti ili wazirejeshe fedha hizo alizoziita batili.
Alisema hawakuona haja ya kumuandikia Rais barua za kujiuzulu kwa kuwa muda wake umeshaisha kisheria. Hata hivyo, ukomo wa Rais kwa mujibu wa Katiba, humalizika mara baada ya kuapishwa mgombea aliyeshinda kwenye uchaguzi.
Wakati Mbarouk akisema hayo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mohamed Aboud Mohamed alisema pamoja na kwamba hawanyi kazi, mawaziri hao wanalipwa mishahara.
“Mimi hayo si mamlaka yangu kisheria ingawa wanalipwa. Hawajakanusha, wala hawajaandika barua,” alisema Aboud. “Sisi tupo kihalali kutokana na mambo mawili, tafsiri aliyoitoa Mwanasheria Mkuu (Said Hassan Said) na pia kikatiba. Kimantiki, Serikali ipo na uhalali huo upo na iwapo wao wanapinga, basi nasema waende mahakamani kupata ufafanuzi wa Katiba.
Lakini Aboud alisema uamuzi huo wa unadhoofisha utendaji na kuathiri ufanisi wa SUK.

No comments:

Post a Comment

 

Most Reading

Eckros Computer Lap 1

Eckros Computer Lap 1

About ETC College

Eckros Tourism College (ETC) started admitting the first intake of students in January 2013. The college falls under tertiary higher education and training as stipulated in education and training policy of 1995.
Also the college administer Distance Learning Programmes, Evening classes, weekend classes, study tours and researchs programmes
Admission Process
New admission into the College is effected twice a year in January-July and July-December.

WALIO PITIA BLOG YETU