ECKROS SCHOOL OF JOURNALISM

eckroscollege. Powered by Blogger.

Blogroll

About

Habari za Mahusiano Kila siku

JOURNALISM STUDENTS AT ETC COLLEGE

JOURNALISM STUDENTS AT ETC COLLEGE

ETC RADIO ONLINE LIVE

http://wwweckrosnewsblogspo.radio12345.com/

WATUMISHI WAANDAMIZI SABA WA TANESCO WAFUKUZWA KAZI KWA TUHUMA MBALIMBALI

Sunday, December 6, 2015

Waandishi habari wakimisikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco, Mhandisi Felschimi Mramba leo jijini Dar es Salaam.


Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
SHIRIKA la Umeme nchini (Tanesco) limewafukuzisha kazi watumishi waandamizi wa Tanesco upande wa maneja na wahasibu kutokana na ubadhirifu wa fedha katika utumishi wao.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco, Felschimi Mramba amesema kuwa shirika halitaweza kuwaacha watendaji wakawa wanafanya kazi kwa rushwa wakati wanalipwa mishahara.

Amesema wataendelea kuchukua hatua kwa watendaji wote watakabainika kufanya udanganyifu au kutoa lugha zisifaa kwa wateja na wakati mwingine kuomba fedha kwa huduma ambazo ni haki ya mwananchi kupata.

Mramba amesema Tanesco imeongeza uzalishaji wa umeme unaotumia gesi megawati 300  sawa na asilimia 115  na kufanya kuwa na umeme wa uhakika huku miradi mingi ikiendelea kufanyika.

Amesema  wanatarajia kupata megawati 240 kutoka Kinyerezi namba mbili  wakati wowote  na kufanya shirika kuwa na umeme wa uhakika.

Aidha amesema wakati wa suala miundombinu likifanyiwa kazi wananchi wawe wavumilivu wa kukatika umeme katokana na kuboresha miundombinu hiyo.

Aliongeza kuwa wanaotaka kufanya kazi na Tanesco kwa kupata nguzo lazima wazalishe nguzo zenye ubora wa kuweza kuhimili kwa muda mrefu bila kuanguka kuanguka.

No comments:

Post a Comment

 

Most Reading

Eckros Computer Lap 1

Eckros Computer Lap 1

About ETC College

Eckros Tourism College (ETC) started admitting the first intake of students in January 2013. The college falls under tertiary higher education and training as stipulated in education and training policy of 1995.
Also the college administer Distance Learning Programmes, Evening classes, weekend classes, study tours and researchs programmes
Admission Process
New admission into the College is effected twice a year in January-July and July-December.

WALIO PITIA BLOG YETU