Mshambuliaji wa kimataifa wa Ureno anayeichezea klabu ya Real Madrid ya HispaniaCristiano Ronaldo amefanikiwa kuweka rekodi kadhaa kubwa katika soka, ukiachana na kutwaa tuzo ya tatu ya mchezaji bora wa Dunia Ballon d’Or kwa mwaka 2015, Ronaldoamefanikiwa kuweka rekodi 7 mpya.
7- Ronaldo amefanikiwa kufunga jumla ya hat-trick 28 katika kipindi cha mwaka 2009-2015, toka amejiunga na Real Madrid mwaka 2009 hadi 2015, Ronaldo anakuwa mchezaji anayeongoza kwa ufungaji wa hat-trick nyingi katika historia ya Laliga.
6- Kufunga magoli 48 kwa msimu mmoja akiwa na Real Madrid. Ronaldo alifunga jumla ya magoli 48 katika msimu wa 2014/2015 na kuweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga magoli mengi katika msimu ndani ya Real Madrid.
5- Kufunga magoli 50 kwa misimu mitano mfululizo. Ronaldo amekuwa mchezaji wa kwanza Hispania kufunga magoli 50 katika misimu mitano mfululizo, alianza kufanya hivyo mwaka (2010/11–2014/15).
4- Kufunga magoli 61 kwa msimu mmoja katika mashindano yote aliyocheza ndani ya msimu wa mwaka 2014/2015.
3- Kuvunja rekodi ya ufungaji wa goli 323 ya mkongwe wa Real Madrid Raul. Ronaldoamefunga jumla ya 338 hadi sasa katika michezo 325 ndani ya Real Madrid, wakati Raulaliweka rekodi ya kufunga goli 323 kwa kucheza michezo 741.
2- Kuwa mchezaji wa kwanza kufunga goli 11 katika michuano ya klabu Bingwa Ulaya hatua za makundi kwa msimu wa 2015/2016.
1- Kuwa mchezaji pekee kutwaa tuzo ya mfungaji bora wa Ulaya mara nne kwa kufunga jumla ya goli 48 kwa msimu wa 2014/2015.
No comments:
Post a Comment