Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Uingereza, Chelsea na West Brom wametozwa faini kwa utovu wa nidhamu uwanjani katika mechi iliyozongwa na ubishi mwezi uliopita.
Shirikisho la soka nchini Uingereza FA limeitoza Chelsea faini ya pauni £65,000.
West Brom kwa upande wake imepigwa faiani ya pauni £35,000.
Mshambulizi mbishi wa Chelsea Diego Costa alihusika katika mengi ya makabiliano hayo uwanjani.
Mhispania huyo alishambuliana na kiungo cha kati wa West Brom, Claudio Yacob baada ya kuangushwa.
West Brom walijifurukuta kutoka nyuma na kutoka sare na wenyeji wao Stamford Bridge.
Katika taarifa kwa vyombo vya habari FA inasema kuwa timu zote mbili zilishindwa kudhibiti wachezaji wake.
Yacob, ambaye alikuwa keshaoneshwa kadi ya njano kwa kumuangusha Costa, aliondolewa uwanjani na kocha Tony Pulis.
Siku chache baadaye kocha wa muda wa Chelsea Guus Hiddink alielezea kutoridhika na uamuzi wa refarii Anthony Taylor, akisema kuwa alipaswa kumuonesha kadi nyekundu Yacob.
No comments:
Post a Comment