ECKROS SCHOOL OF JOURNALISM

eckroscollege. Powered by Blogger.

Blogroll

About

Habari za Mahusiano Kila siku

JOURNALISM STUDENTS AT ETC COLLEGE

JOURNALISM STUDENTS AT ETC COLLEGE

ETC RADIO ONLINE LIVE

http://wwweckrosnewsblogspo.radio12345.com/

KAMATI YA KURATIBU MISS TANZANIA YAJITOA KWENYE MASHINDANO

Friday, January 22, 2016


PI1

Mwenyekiti wa Kamati ya kuratibu Miss Tanzania Juma Pinto akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani) leo  jijini Dar-es-Salaam juu ya kujitoa kwao kama kamati ya kuratibu Miss Tanzania ambayo ilichagulia na kampuni ya Lino International Agency, kushoto ni Msemaji wa kamati hiyo Joketi Mwegelo na kulia ni Mjumbe wa kamati Gladys Shao 

PI3

Waandishi wa habari wakimfuatilia kwa makini Mwenyekiti wa Kamati ya kuratibu mashindano ya Miss Tanzania, Juma Pinto (hayupo pichani) alipokuwa akitoa sababu za kujitoa kwa kamati katika mashindano hayo.
PICHA NA Beatrice Lyimo-Maelezo
………………………………………………………………………………………………………………….
Lilian Lundo- Maelezo
Dar es Salaam.

Kamati ya kuratibu Miss Tanzania imejitoa rasmi kusimamia mashindano ya Miss Tanzania kuanzia leo tarehe 21/01/2016.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo  Juma Pinto alisema hayo leo, alipokuwa akiongea na waandishi wa habari jijini Dar-es-Salaam.
“Tumekuja
kutoa taarifa kwamba, kama tulivyo teuliwa na kampuni ya Lino International Agency, kuandaa, kuendesha na kusimamia mashindano ya Miss Tanzania, kamati yangu imeamua kujitoa kutokana na majukumu ya kamati kuingiliwa na kampuni ya Lino,” alisema Pinto.
Pinto aliongeza kwa kusema kuwa kamati yake ilipewa jukumu la kuendesha mashindano na kuwajibika kufanya kila kitu na Lino itakuwa kama washauri, lakini badala yake Lino imetaka kuhodhi majukumu yote na kamati ikawa ni ya kutafuta wadhamini.

Kamati hiyo imefanya vikao vingi vya kuhakikisha mashindano yanaboreshwa na kubadilisha mfumo ili kuifanya Miss Tanzania kuwa na mwonekano tofauti kama ambavyo Lino ilivyoamua kuweka kamati mpya ili kuboresha mashindano hayo.
Kutokana na kutopata muafaka katika vikao hivyo vya kuboresha mashindano ya Miss Tanzania, Kamati ya kuratibu mashindano hayo kwa nia njema na wala si kwa ubaya imeamua kujitoa katika Mashindano hayo.

Aidha, Pinto amewaomba radhi wadhamini ambao wameshaongea nao kama kamati na walioonesha nia ya kuwasaidia, amewataka kuendelea kufanya mawasiliano na kampuni ya Lino kwani madhumuni ni kudhamini mashindano na sio kamati.

No comments:

Post a Comment

 

Most Reading

Eckros Computer Lap 1

Eckros Computer Lap 1

About ETC College

Eckros Tourism College (ETC) started admitting the first intake of students in January 2013. The college falls under tertiary higher education and training as stipulated in education and training policy of 1995.
Also the college administer Distance Learning Programmes, Evening classes, weekend classes, study tours and researchs programmes
Admission Process
New admission into the College is effected twice a year in January-July and July-December.

WALIO PITIA BLOG YETU