Wananchi mkoani Rukwa wamelalamikia kasi ndogo, inayofanywa na mkandarasi wa kusambaza umeme wa mradi wa umeme vijijini wa REA, ambapo kati ya vijiji 142 vilivyopangwa kupitiwa na umeme huo kwa awamu ya tatu, ni vijiji saba tu vilivyofikiwa hadi sasa na kwa wateja wasiozidi kumi tu.
Mkuu wa wilaya ya Nkasi Bw. Said Mtanda, akitoa taarifa kwa naibu waziri wa nishati Mheshimiwa Subira Mgallu, alipokuwa akikagua ujenzi wa njia kuu ya umeme kwenye mji mdogo wa Kirando, katika mwambao wa ziwa Tanganyika kwa ajili ya viwanda, amesema mkandarasi huyo Nakuroi Investment amekuwa akitekeleza mradi huo kwa kasi ndogo mno, na huku akitoa visingizio vingi hali inayoashiria kushindwa kuutekelza kwa ufanisi.
Kwa upande wake naibu waziri wa nishati Mheshimiwa Subira Mgallu, akiwa katika kijiji cha Nchenje wilayani Nkasi alipotakiwa kuwasha umeme, na kugoma kwa kutoridhishwa na mwenendo mzima wa utekelezaji wa mradi huo, amemuagiza mkandarasi huyo aende Jijini Dodoma kujieleza kwanini asinyang'anywe mradi huo wa zaidi ya shilingi bilioni 42.
No comments:
Post a Comment