ECKROS SCHOOL OF JOURNALISM

eckroscollege. Powered by Blogger.

Blogroll

About

Habari za Mahusiano Kila siku

JOURNALISM STUDENTS AT ETC COLLEGE

JOURNALISM STUDENTS AT ETC COLLEGE

ETC RADIO ONLINE LIVE

http://wwweckrosnewsblogspo.radio12345.com/

Jenerali wa Magereza nchini Phaustine Kasike Awaasa Maofisa wa Jeshi la Magereza Kuzingatia Maadili ya Kazi

Thursday, August 2, 2018


Na chrispin kalinga

KAMISHNA Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike amewataka Maofisa na askari wa Jeshi hilo kujiepusha na vitendo vilivyo kinyume na maadili ya kazi yao, badala yake wazingatie kanuni, miiko na maadili ya uendeshaji wa Jeshi la Magereza.
 
Kamishna Jenerali Kasike ametoa rai hiyo jana Agosti 1, 2018 wakati akiongea na Maofisa na askari wa Jeshi la Magereza Mkoani Arusha alipofanya ziara ya kikazi Mkoani humo.
 
Alisema kuna upungufu katika uzingatiaji wa maadili kwa baadhi ya Maofisa na askari hususani mahusiano mabaya ya askari na wafungwa ikiwemo tabia za askari kuingiza simu magerezani.
 
Amesema hatua kali za kinidhamu zitachukuliwa kwa maofisa na askari watakaobainika kufanya vitendo hivyo ikiwemo kuwajibishwa na kufukuzwa kazi.
 
“Mnajua kabsaa gharama za kujihusisha na tabia hizi za mahusiano mabaya na wafungwa nawaasa mzingatie maadili mnapotekeleza majukumu yenu ya kazi”. Alisisitiza Kamishna Jenerali Kasike.
 
Kuhusu agizo la Rais Dkt.  John Pombe Magufuli kuhusu kujitosheleza kwa chakula cha wafungwa Kamishna Jenerali Kasike amesena kwa sasa Jeshi hilo linakamilisha mpango kazi wake utakaowezesha utekelezaji wa agizo hilo.
 
Amewataka askari wote nchini kujiandaa kisaikolojia kutekeleza agizo hilo bila kisingizio chochote kwani Jeshi la Magereza linazo rasilimali za kutosha kutekeleza agizo hilo.
 
“Tunayo ardhi yakutosha, nguvu kazi ya wafungwa ipo hivyo agizo la Rais na Amiri Jeshi Mkuu lazima litekelezwe bila kisingizio chochote”. Alisema Jenerali Kasike.
 
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike yupo katika ziara ya kikazi ya siku mbili Mkoani Arusha ambapo lengo la ziara hiyo ni kukagua utendaji kazi pamoja na kuzungumza na Maofisa na askari wa Jeshi hilo

No comments:

Post a Comment

 

Most Reading

Eckros Computer Lap 1

Eckros Computer Lap 1

About ETC College

Eckros Tourism College (ETC) started admitting the first intake of students in January 2013. The college falls under tertiary higher education and training as stipulated in education and training policy of 1995.
Also the college administer Distance Learning Programmes, Evening classes, weekend classes, study tours and researchs programmes
Admission Process
New admission into the College is effected twice a year in January-July and July-December.

WALIO PITIA BLOG YETU