ECKROS SCHOOL OF JOURNALISM

eckroscollege. Powered by Blogger.

Blogroll

About

Habari za Mahusiano Kila siku

JOURNALISM STUDENTS AT ETC COLLEGE

JOURNALISM STUDENTS AT ETC COLLEGE

ETC RADIO ONLINE LIVE

http://wwweckrosnewsblogspo.radio12345.com/

Kesi ya Habinder Seth na Rugemalira Yapigwa Kalenda Tena

Thursday, August 16, 2018

Kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili mshtakiwa Habinder Seth na mwenzake, leo Alhamisi 16, 2018 imeahirishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu hadi Agosti 30, 2018.

Hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo, Kelvin Mhina ameahirisha kesi hiyo leo hadi Agosti 30, 2018 baada ya wakili wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Leonard Swai kueleza upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.

Swai ameomba kesi hiyo ipangiwe tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa ili kuangalia kama upelelezi utakuwa umekamilika ama la.

Hata hivyo, Hakimu Mhina amesema kesi hiyo imeahirishwa kwa kuwa hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi anayeiendesha kesi hiyo anaumwa.

Mbali na Seth, mshtakiwa mwingine katika kesi hiyo ni mfanyabiashara, James Rugemalira, ambao kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka 12, katika Mahakama hiyo.

Mashtaka hayo ni uhujumu uchumi kwa kula njama, kujihusisha mtandao wa uhalifu, kuhushi, kutoa nyaraka za kughushi. Pia wanadaiwa kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu na kutakatisha fedha

No comments:

Post a Comment

 

Most Reading

Eckros Computer Lap 1

Eckros Computer Lap 1

About ETC College

Eckros Tourism College (ETC) started admitting the first intake of students in January 2013. The college falls under tertiary higher education and training as stipulated in education and training policy of 1995.
Also the college administer Distance Learning Programmes, Evening classes, weekend classes, study tours and researchs programmes
Admission Process
New admission into the College is effected twice a year in January-July and July-December.

WALIO PITIA BLOG YETU