ECKROS SCHOOL OF JOURNALISM

eckroscollege. Powered by Blogger.

Blogroll

About

Habari za Mahusiano Kila siku

JOURNALISM STUDENTS AT ETC COLLEGE

JOURNALISM STUDENTS AT ETC COLLEGE

ETC RADIO ONLINE LIVE

http://wwweckrosnewsblogspo.radio12345.com/

Waziri Mkuu kuwa mgeni rasmi kwenye mchezo wa tamasha la 'Simba Day'

Friday, August 3, 2018

Klabu ya soka ya Simba leo imemtangaza Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa kuwa mgeni rasmi kwenye mchezo wa tamasha la 'Simba Day' dhidi ya Asante Kotoko ya Ghana Agosti 8, 2018.

Akiongea leo na wanahabari, msemaji wa timu hiyo Haji Manara, amethibitisha kuwa tayari Waziri mkuu ameshakubali ombi lao na kuahidi atakuwepo uwanjani kuwaongoza mashabiki wa Simba katika tamasha lao lenye shughuli mbalimbali ikiwemo kutambulishwa kwa wachezaji wapya.

''Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amekubali ombi letu, na ninaomba nitangaze rasmi kuwa yeye ndio atakuwa mgeni rasmi kwenye tamasha letu la 'Simba Day' akiongoza shughuli zote ambazo zitafanyika siku hiyo'', - amesema.

Mbali na kumtangaza mgeni rasmi, Manara amewataka mashabiki wa timu hiyo kutojihusisha na masuala ya kugushi tiketi kwani wao kama klabu wamejidhatiti kuhakikisha watu wa aina hiyo hawapati mwanya ndio maana suala la usimamizi wa tiketi uwanjani wamelikabidhi kwa Suma JKT.

Aidha Manara amesema kikosi cha Simba kitatua nchini Jumatatu ya Agosti 6 kikitokea Uturuki ambako kimeweka kambi ya maandalizi ya msimu wa 2018/19. Pia siku hiyo Simba watatambulisha jezi zao mpya za nyumbani na ugenini msimu huu

No comments:

Post a Comment

 

Most Reading

Eckros Computer Lap 1

Eckros Computer Lap 1

About ETC College

Eckros Tourism College (ETC) started admitting the first intake of students in January 2013. The college falls under tertiary higher education and training as stipulated in education and training policy of 1995.
Also the college administer Distance Learning Programmes, Evening classes, weekend classes, study tours and researchs programmes
Admission Process
New admission into the College is effected twice a year in January-July and July-December.

WALIO PITIA BLOG YETU