Na Timothy Itembe, Tarime
Baadhi ya wazazi na walezi wilayani Tarime katika Mkoa wa Mara wametakiwa kuondokana na imani potofu kuwa dawa za kichocho na minyoo zina madhara kwa binadamu.
Akiongea kwenye zoezi la Uzunduzi wa Kampeni ya Kumeza Dawa za Minyoo na Kichocho kwa watoto chini ya umri wa miaka mitano na kuendelea lililofanyikia Viwanja vya Shule ya Msingi Sirari ambapo Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Sirari, Kennedy Mniko alisema kuwa wanakumbwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya jamii kundelea kujenga imani kuwa dawa hizo zinamadhara kwa binadamu jambo ambalo siyo kweli.
"Mimi nipende kusema kuwa bado jamii imejenga imani potofu kuwa dawa za minyoo na kichocho zinazotolewa na serikali ili watoto chini ya miaka mitano na kuendelea,kumeza na kutokomeza magonjwa ya kichocho na minyoo hazina madhara kwa binadamu kwa hali hiyo jamiii iondokane na dhana hiyo," alisema Mniko.
Pia mwalimu huyo aliongeza kuwa kumeza dawa kunasaidia kupunguza maambukizi ya magonjwa na kujenga jamii yenye Afya"watoto wanaoruhusiwa kumeza dawa ni wale tu ambao wameruhusiwa kisheria hususani waliotimiza umri wa miaka mitano na kuendelea na wasiwe na magonjwa nyemelezi vinginevyo akibainika kuwa Afya yake hairuhusu anatakiwa kuonana na Daktari ndipo aruhusiwe kumeza dawa," alisema Mniko.
Kwa upande wake Dk. Hamidu Adinani alisema kuwa watoto waliolengwa kumeza dawa kwa mwaka huu za kichocho na minyoo ndani ya halmashauri ya Tarime vijijini ni zaidi ya 121511.
Dk. Adinani aliongeza kuwa jamii inawajibu mkubwa kuwaelimisha watoto ili kumeza dawa kwaajili ya kinga ya magonjwa mbalimbali kwasababu dawa zimedhibitishwa na wizara ya Afya na hazina madhara yakiafya kwa binadamu.
"Lengo la Serikali ya Tanzania nikuwa na Taifa lenye watu wenye Afya bora na pia kujenga Taifa lenye watoto walio na uwezekano wa kuwa na uwelewa mzuri darasani"alisema mganga mkuu wa hospitali ya halmashauri ya Tarime Adinani.
Naye Mkuu wa Wilaya Tarime, Glorius Luoga ambaye alialikwa kuwa Mgeni Rasmi wa Uzinduzi huo alisema kuwa anasikiitishwa kuona bado kuna jamii imejenga imani potofu kuwa dawa hizi zina madhara.
Luoga aliongeza kuwa zoezi hili ni endelevu na kuwa tangu zamani za mababu zetu watu walikuwa wanameza dawa na kupewa chanjo za kinga ya magonjwa mbalimbali na kuwa serikali yetu haina lengo baya na jamiii inayowaongoza na ndio sababu Rais John Pombe Magufuli ametoa msaada wa dawa za minyoo na kichocho kwa Watoto wote chini ya miaka mitano na kuendelea kumeza.
Luoga aliwataka wazazi na walezi kujitokeza kwa wingi ili kuwapeleka watoto wao kumeza dawa hizi ili kupungua maambukizi ya magonjwa na kujenga Taifa lenye watu wenye Afya na wasiokuwa na magonjwa
No comments:
Post a Comment