ECKROS SCHOOL OF JOURNALISM

eckroscollege. Powered by Blogger.

Blogroll

About

Habari za Mahusiano Kila siku

JOURNALISM STUDENTS AT ETC COLLEGE

JOURNALISM STUDENTS AT ETC COLLEGE

ETC RADIO ONLINE LIVE

http://wwweckrosnewsblogspo.radio12345.com/

Mabasi 12 Ya Kwenda Mikoani yasitisha safari n zake

Monday, August 6, 2018

Mabasi 12 yanayofanya safari za kutoka Dar es Salaam kwenda mikoa mbalimbali leo Jumatatu Agosti 6, 2018 yamesitisha safari zake mpaka yatakapotengenezwa baada ya kubainika kuwa na kasoro katika mfumo wa usukani.

Akizungumza leo wakati akitoa maelezo kwa waandishi wa habari kuhusu ukaguzi wa mabasi katika msafara wa mafunzo ya usalama barabarani kuelekea mkoani Tanga, mrakibu wa Jeshi la Polisi, Abel Swai amesema mabasi hayo hayataruhusiwa kuondoka mpaka yatengenezwe.

Swai ambaye pia ni mkuu wa kitengo cha elimu kwa umma kikosi cha usalama barabarani, amesema changamoto kubwa ya mabasi yaliyo mengi ni tatizo la mikono ya usukani.

Amesema wanaangalia  zaidi kama basi linaweza  kukata kona vizuri, liwe na mneso na kubaini changamoto wanazokutana nazo, hasa kwa mabasi yanayosafiri umbali mrefu akibainisha kuwa kama yatabainika upungufu unaweza kuwa chanzo cha ajali.

"Ukaguzi huu unafanyika kwa mujibu wa sheria ya usalama barabarani sura ya 168 ya mwaka 2002 fungu la 39 ambayo imebainisha mambo ambayo ni ya muhimu katika gari ambayo kama yatakuwa hayafanyi kazi halitaruhusiwa kuendeshwa," amesema.

Mkaguzi wa mabasi wa kikosi cha usalama barabarani katika kituo cha mabasi yaendayo mikoani cha Ubungo (UBT), Ibrahim Samwix amesema kwa taratibu za Sumatra, mabasi hayo yanatakiwa kufungwa vipuri vipya na baada ya ukaguzi yataruhusiwa kuendelea na safari.

“Mabasi yote yana abiria na tunawapa muda wa kuyatengeneza yasizidi masaa mawili, kama wakishindwa itabidi washushe abiria watafutiwe usafiri mwingine," amesema Samwix bila kutaja majina ya mabasi hayo.

“Changamoto kubwa hata waliopo ndani ya mabasi si mafundi maana mkiingia kukagua basi huko chini wao hawaoni tatizo lolote,” amesema.

“Wanajua kutengeneza lakini hawawezi kubaini tatizo na hawataki kujifunza. Sisi tupo tayari kuwafundisha ila huwa hawajitokezi.”

No comments:

Post a Comment

 

Most Reading

Eckros Computer Lap 1

Eckros Computer Lap 1

About ETC College

Eckros Tourism College (ETC) started admitting the first intake of students in January 2013. The college falls under tertiary higher education and training as stipulated in education and training policy of 1995.
Also the college administer Distance Learning Programmes, Evening classes, weekend classes, study tours and researchs programmes
Admission Process
New admission into the College is effected twice a year in January-July and July-December.

WALIO PITIA BLOG YETU