Na chrispin kalinga
WAZIRI
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amemtaka Mkuu wa Polisi wa
Wilaya ya Bunda kuwakamata watu walioshiriki kuwatapeli wananchi katika
Sekta ya michezo wilayani humo, Mkoa wa Mara.
Watu
hao ambao walitangaza kuanzisha ligi wilayani humo na kuzitaka timu za
mpira wa miguu kata mbalimbali zichangie fedha na baadaye ligi hiyo
haikufanyika na watu hao walikimbia na fedha hizo na kufanya wananchi
hao waandamane wakitaka fedha zao zirudishwe.
Waziri
Lugola akizungumza na mamia ya wananchi wa Mji wa Bunda baada ya
kulizindua Bonanza la Amani wilayani humo, alisema kitendo
walichokifanya watu hao ni ufiadi mkubwa hivyo lazima wakamatwe ili iwe
funzo kwa wale wote wenye tabia ya kufanya ufisadi wa aina hiyo katika
sekta ya michezo nchini.
“Nimeambiwa
wanamichezo ambao walichangishwa waliandamana mpaka kwa Mkuu wa Wilaya
kuelezea jinsi walivyoibiwa na watu hao, hata hivyo Mkuu wa Wilaya
alitangaa watu hao warudishe fedha hizo, ila mimi nahitaji hawa watu
wakamatwe haraka iwezekanavyo, huu ni ufisadi mkubwa na hakika Serikali
hii ya awamu ya nne haitakubaliana na ufisadi huo.
Aliongeza
kua, mahakama ya ufisadi inahitaji wateja hivyo waliofanya wizi huo pia
ni mafisadi hivyo lazima wakamatwe haraka iwezekanavyo ili sheria
ichukue mkondo wake.
Aidha,
Bonanza ambalo alilizindua waziri huyo, linatarajiwa kufanyika nchini
nzima limezinduliwa mjini humo na baadaye litafanyika nchi nzima likiwa
na lengo kuu kutangaza amani nchini.
Waziri
Lugola alisema, michezo inaleta amani michezo inaleta ushirikinao,
michezo inaimarisha undugu, michezo inaimarisha ushikamano na michezo
uepusha wananchi wasijiingize katika uhalifu, hivyo Wizara yake
inatarajia Bonanza hilo litazidi kudumisha amani zaidi.
“Michezo
ikiimarishwa tunaimarisha amani, tukishiriki michezo kama hivi
wanaokuja kutazama na nyie mnaocheza, hivyo muda mwingi tunautumia
katika kufurahi pamoja na ndio mana vitendo vya uhalifu vitapungua
kwasababu watu tunataka tuwe wamoja kupitia michezo,” alisema Lugola.
Waziri
Lugola aliongeza kua, Bonanza la kuhubiri amani sio kwamba linafanya
wilyani Bunda bali litafnyika nchi nzima likiwa na lengo la kuwaweka
watanzania pamoja ili amani nizidi kudumu.
“Hapa
tulipo ni uwanja wa CCM na hii ilani ni ya CCM na katika ibara ya 160,
161 na 162 inazungumzia kuimarisha na kudumisha sekta ya michezo, hivyo
tupo hapa kutokana na ilani hii ya CCM na lengo kuu ni kudumisha amani,”
alisema Lugola.
Waziri
Lugola yupo wilayani Bunda mkoani Mara kwa ajili ya ziara ya kutembelea
miradi ya maendeleo ndany ya jimbo lake la Mwibara wilayani humo.
No comments:
Post a Comment