ECKROS SCHOOL OF JOURNALISM

eckroscollege. Powered by Blogger.

Blogroll

About

Habari za Mahusiano Kila siku

JOURNALISM STUDENTS AT ETC COLLEGE

JOURNALISM STUDENTS AT ETC COLLEGE

ETC RADIO ONLINE LIVE

http://wwweckrosnewsblogspo.radio12345.com/

Makamu wa rais wa zamani DRC Bemba apigwa chini kugombea urais

Saturday, August 25, 2018

Bw Bemba ni miongoni mwa wagombea sita waliokuwa wamewasilisha majina yao kutaka kugombea, lakini tume hiyo imesema hawajahitimu baada ya mashauriano ya saa kadha.
Kiongozi huyo wa zamani wa waasi aliachiliwa huru baada ya mahakama kubatilisha hukumu dhidi yake ya kumpata na hatia ya uhalifu wa kivita mwezi Juni.
Tume ya uchaguzi imesema Bw Bemba amezuiwa kuwania kwa sababu alipatikana na hatia ya kuwahonga mashahidi katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita (ICC).
Bw Bemba, aliyerejea DR Congo mwanzoni mwa Agosti baada ya kukaa miaka 11 uhamishoni au gerezani, amewasilisha rufaa kupinga hukumu hiyo dhidi yake katika ICC.
Uchaguzi wa mwaka huu utafanikisha kuchaguliwa kwa mrithi wa Rais Joseph Kabila, ambaye muhula wake wa pili na wa mwisho wa kuongoza ulimalizika miaka miwili iliyopita.
Muungano tawala nchini humo ulimteua waziri wa zamani wa mambo ya ndani Emmanuel Ramazani Shadary kuwa mgombea wake.
Kulikuwa na jumla ya watu 25 waliotaka kuwania, wakiwemo mawaziri wakuu wa zamani Antoine Gizenga na Adolphe Muzito. Wawili hao pia wamekataliwa kuwania.
Vyama vya upinzani vilishutumu hatua hiyo ya tume ya uchaguzi hata kabla ya uamuzi huo kutangazwa rasmi, wakiituhumu serikali ya sasa kwa kujaribu kudhibiti na kuelekeza mchakato wa uchaguzi.
Wale waliozuiwa kuwania akiwemo Bemba anayetazamwa na wengi kama mgombea anayetoa ushindani mkali zaidi kwa muungano tawala wa rais Kabila, wanaweza kukata rufaa uamuzi huo wa tume.

No comments:

Post a Comment

 

Most Reading

Eckros Computer Lap 1

Eckros Computer Lap 1

About ETC College

Eckros Tourism College (ETC) started admitting the first intake of students in January 2013. The college falls under tertiary higher education and training as stipulated in education and training policy of 1995.
Also the college administer Distance Learning Programmes, Evening classes, weekend classes, study tours and researchs programmes
Admission Process
New admission into the College is effected twice a year in January-July and July-December.

WALIO PITIA BLOG YETU