ECKROS SCHOOL OF JOURNALISM

eckroscollege. Powered by Blogger.

Blogroll

About

Habari za Mahusiano Kila siku

JOURNALISM STUDENTS AT ETC COLLEGE

JOURNALISM STUDENTS AT ETC COLLEGE

ETC RADIO ONLINE LIVE

http://wwweckrosnewsblogspo.radio12345.com/

Dogo Janja: Sijawahi kuwa na bifu na msanii yoyote hapa nchini

Thursday, August 2, 2018


Msanii wa muziki wa kizazi kipya Abdul Aziz Chande maarufu kama 'Dogo Janja' amesema hana bifu lolote na wasanii wenzake ambao amekuwa akihusishwa nao kama, Young Killer na Young Dee huku akidai vitu hivyo vinavumishwa na watu, lakini wao ni marafiki na wala hawana ugomvi.

Dogo Janja amebainisha hayo wakati alipokuwa anazungumza kwenye kipindi cha KIKAANGONI kinachorushwa mubashara kupitia kurasa za facebook za EATV, baada ya kuulizwa swali Abdul Yunusi ambaye alikuwa anafuatilia kipindi hicho kwa kutaka kujua kama ana ugomvi wowote na Young Killer pamoja na Young Dee.

"Sijawahi kuwa na bifu na msanii yoyote hapa nchini kwasababu mimi napita kwenye njia yangu nasio njia ya mtu kwa hiyo ni watu ndio wanaamua kufanya hivyo kwa kuweka ule 'U- young' lakini hatuna ugomvi, sisi ni marafiki", amesema Dogo Janja.

Pamoja na hayo, Dogo Janja ameendelea kwa kusema "sisi nje ya muziki tuna maisha yetu, hivyo huwa tunakutana mara moja moja na tunataniana sana, ila hawaniwezi mimi kwa matani maana nina kera na wao wanafahamu hilo".

Mbali na hilo, Dogo Janja amedai hakuna changamoto yoyote anayopitia endapo maswahiba zake wakitoa nyimbo kwa kile alichokieleza kuwa wao wana-rap na yeye anaimba kawaida.

Dogo Janja amekuwa akihusishwa kwenye ugomvi huo kutokana na wasanii hao kila mmoja akifanyiwa 'interview' na chombo cha habari huwa lazima mmoja wao amponde mwenzake kwa jambo baya na kupelekea kujenga hoja ya bifu katika vichwa vya mashabiki zao. Lakini kwa kauli ya Janjaroo aliyoitoa tunaweza kusema bifu hilo kwa sasa limefikia tamati.

No comments:

Post a Comment

 

Most Reading

Eckros Computer Lap 1

Eckros Computer Lap 1

About ETC College

Eckros Tourism College (ETC) started admitting the first intake of students in January 2013. The college falls under tertiary higher education and training as stipulated in education and training policy of 1995.
Also the college administer Distance Learning Programmes, Evening classes, weekend classes, study tours and researchs programmes
Admission Process
New admission into the College is effected twice a year in January-July and July-December.

WALIO PITIA BLOG YETU