ECKROS SCHOOL OF JOURNALISM

eckroscollege. Powered by Blogger.

Blogroll

About

Habari za Mahusiano Kila siku

JOURNALISM STUDENTS AT ETC COLLEGE

JOURNALISM STUDENTS AT ETC COLLEGE

ETC RADIO ONLINE LIVE

http://wwweckrosnewsblogspo.radio12345.com/

BREAKING NEWZZ: TAARIFA MPYA KUTOKA IKULU KUHUSU VIGOGO HAWA

Thursday, December 31, 2015




KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.
Kesho Ijumaa 01 Januari, 2016 Makatibu Wakuu na Manaibu Katibu Wakuu walioteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wataapishwa rasmi katika Ukumbi wa Ikulu, uliopo lango kuu litazamalo baharini kuanzia saa nne asubuhi.
Makatibu Wakuu na Manaibu Katibu Wakuu wote ambao wataapishwa na wale ambao walishaapishwa wanapaswa kuhudhuria katika tukio hili, ili mara baada ya kiapo kukamilika washiriki zoezi la kutia saini Hati ya Ahadi ya Uadilifu kwa Viongozi wa Umma (Integrity Pledge).
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue amesema zoezi la kutia saini hizo, litafanyika kwa uwazi mbele ya vyombo vya habari.
Aidha, Balozi Sefue amefafanua kuwa hata kama wapo baadhi ya Makatibu Wakuu na Manaibu Katibu Wakuu ambao walishasaini Hati hizo, watapaswa kusaini upya mbele ya vyombo vya habari.
Tukio hili pia litarushwa ‘live’ kupitia luninga.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi Mawasiliano, IKULU

31 Desemba, 2015.

SALAMU ZA MWAKA MPYA



Wapenzi Wasomaji wetu, Tunajisikia furaha kwa heshima mliyotupa ya kutenga muda wenu kwa ajili ya kuitembelea tovuti yetu ya Swahilivilla kila siku. Heshima hiyo ni fadhila kubwa kwetu ambayo kamwe hatuwezi kuilipa.

Kwa unyenyekevu kabisa, tunawashukuruni nyote kwa kujumuika nasi na kuwa kama familia moja inayoishi ndani ya Swahilivilla.

Kwa ndugu zetu ambao wametangulia mbele ya haki katika mwaka wa 2015 na qabla yake, tunawaombea Mola Mlezi awaingize katika Rehma zake. Na kwa wale ambao bado wako hai, tunaombea afya njema, kazi njema zenye fanaka na baraka na baada ya kazi tujumuike pamoja katika Baraza yetu ya kila siku ya Swahilivilla.

Maoni yenu ni uti wa mgongo wa ufanisi wa tovuti yetu. Kwa hivyo tunatoa shukrani na pongezi maalum kwa wale walitumia muda wao na kutoa maoni yao katika maqala mbalimbali tulizochapisha katika mwaka uliopita. Muda wenu haukupotea bure, kwani maoni yote tunayafanyia kazi kwa ajili ya kuboresha mtandao wetu.

Ni matumaini yetu kwamba mutaendelea kututumia michango yenu, na kwa wale ambao hawakufanikiwa kututumia maoni, basi imani yetu kubwa ni kuwa watafanya hivyo katika mwaka mpya kwa ajili ya ustawi wa jamii yetu ya Swahilivilla.

Tunawatakieni nyote mwaka mpya wenye kheri na baraka wa 2016, tukiwaacheni muburudike na kipande kifuatacho

Ahsanteni,

Uongozi wa Swahilivilla

Naibu waziri wa Wizara ya Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Anthony Mavunde afanya ziara makao makuu ya Tigo

Wednesday, December 30, 2015

Dar es Salaam, 30th December 2015- Tigo Tanzania leo imepokea kwa furaha ugeni wa ghafla wa Naibu waziri wa Wizara ya Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde alipotembelea makao makuu ya kampuni hiyo yaliyoko Kijitonyana jijini Dar es Salaam.



Meneja Mkuu wa Tigo, Diego Gutierrez , akizungumza na waandishi wa habari (Hawapo pichani) katika mkutano alioshiriki pia Naibu waziri wa Wizara ya Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde  baada ya kufanya ziara katika makao  makuu ya Tigo Kijtonyama  jijini Dar es laam
Mhe. Mavunde ambaye alikuwa ameongozana na waandishi wa habari na maofisa kutoka ofisi za uhamiaji alitinga ofisini hapo mnamo saa nne asubuhi ya Jumatano ya tarehe 30 Desemba na kupokelewa na Mkurugenzi Mkuu wa Tigo, Bwana Diego Gutierrez pamoja na wafanyakazi wengine wa kampuni ya Tigo.

Bwana Gutierrez alimtembeza Naibu Waziri kwenye idara mbalimbali za kampuni hiyo huku akitambulisha huduma zinazotolewa na kujibu maswali yaliyokuwa yakiulizwa na Mhe. Waziri.

Kampuni ya Tigo imekuwa mstari wa mbele kwenye sekta ya mawasiliano kwa kutoa huduma na bidhaa zenye ubunifu na manufaa makubwa kwa jamii, hivyo kuchangia kwa kiasi kukubwa sana kuendeleza sekta hii muhimu kupitia njia mbali mbali kama kutoa ajira, kuchangia pato la taifa, kuchangia maendeleo ya jamii na kuwezesha watanzania wajiendeleze kiuchumi na kijamii kupitia mawasiliano ya bei nafuu.

Bwana Gutierrez alisema kampuni ya Tigo imefurahishwa mno na ugeni huo huku akiongeza kuwa ugeni huo unadhihirisha kwamba serikali imeonesha kwamba inajali huduma zinazotolewa na mashirika ya sekta binafsi.


Bwana Gutierrez alisema “Tutaendelea kushirikianana na serikali ya awamu ya tano kuhakikisha kuwa sekta ya mawasiliano inakua zaidi na inaleta mabadiliko lukuki kwenye maisha ya watanzania na nchi nzima kwa ujumla. Tigo imejikita kwenye kupanua wigo wa mawasiliano kuhakikisha kila mtanzania popote alipo anaweza kuwasiliana kwa bei nafuu, kupitia mtandao bora na wenye huduma zenye uhakika".

Kuhusu kuitembelea Tigo, Mh. Mavunde alisema: "leo tumetembelea kampuni ya Tigo, kwa ajili ya kujitosheleza vipi kampuni hii inajali waajiri wake, na katika ziara hii tumebaini mambo kadha ambayo tungependa kampuni ya Tigo, ivifanyie kazi kwa mfano kwenye maswala ya afya na usalama, na pia tungependa kuona mikataba baina ya Tigo na watoa huduma wake, pia serikali ya awamu ya tano, ipo makini kuhakikisha sheria inafuatwa ili tuwe na jamii inayozingatia sheria"


Naibu waziri wa Wizara ya Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde  akizungumza na wafanyakazi wa tigo baada ya kufanya ziara mapema leo  katika makao  makuu ya Tigo kijtonyama  jijini Dar es laam 

Naibu waziri wa Wizara ya Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Anthony Mavunde akizungumza na waandishi wa habari na wafanyakazi wa tigo   baada ya kufanya ziara mapema leo  katika makao  makuu ya Tigo kijitonyama Dar es laam 

MKUU WA HUDUMA YA MAGEREZA AWASAIDIA WAFUNGWA KUTOROKA KATIKA GEREZA LENYE ULINZI MKALI KABLA YA KUFUKUZWA KAZI

Mkuu wa huduma ya magereza katika mji Buenos Aires Argentina amefutwa kazi baada ya wafungwa watatu mashuhuri kutoroka kutoka gereza lenye ulinzi mkali siku ya Jumapili.
Gavana wa jimbo hilo , Bi Maria Eugenia Vidal , alisema yeye alichukua hatua hiyo kwa sababu kulikuwa na ushahidi kwamba wafungwa wote walisaidiwa na maafisa wa idara ya magereza kutoroka .
Wafungwa hao Victor Schillaci na kaka wawili Cristian na Martin Lanatta, walikuwa wanatumikia hukumu ya maisha gerezani kwa makosa ya utekaji nyara na mauaji ya wafanyabiashara watatu katika tukio lililohusishwa na mzozo wa madawa ya kulevya mnamo mwaka wa 2008.
Yamkini walitoroka kutoka kwenye gereza lenye ulinzi mkali zaidi wakitumia bunduki bandia kutishia moja wa walinzi.

VIONGOZI CHAMA CHA WALIMU CWT MKOANI NJOMBE WAPATIWA MAFUNZO YA UONGOZI

Tuesday, December 29, 2015



Walimu mkoani njombe wametakiwa kuwaandaa wanafunzi mashuleni kwaajili ya kunufaika na uwekezaji mkubwa wa madini yaliganga na mchuchuma wilayani ludewa kutokana na tathmini kuonyesha kuwa migodi hiyo miwili itahitaji wafanyakazi wengi ambao ni wazawa na wenye ujuzi

Aidha walimu  wenyewe wametakiwa kujiandaa na uwekezaji huo kwa kufanya shughuli mbalimbali za ujasilia mali kama kilimo na ufugaji kufuatia kundi kubwa la wageni ambao watahitaji bidahaa mbali kama mifugo na mazao ya chakula

ushauri huo umetolewa na mkuu wa mkoa njombe dkt rehema nchimbi wakati akifungua semina elekezi kwa viongozi wa chama cha walimu mkoa wa njombe CWT Ambapo amesema kuwa zaidi ya wafanyakazi wazawae lfu 50  watanufaika na ajira  huku idadi ya wageni kutoka nchini china ikiwa elfu sita ambao watahitaji bidhaa mbalimali kutoka kwa wenyeji


Mmoja wa wakufunzi katiaka semina hiyo ya siku tatu mwalimu Issa Ally Ngayama ambaye Katibu wa Chama Cha Walimu Tanzania CWT Mkoa wa Morogoro amewataka alimu hao kuacha kujigawa kwa kuanzisha vyama vya walimu nje ya CWT kwa kuwa kufanya hivyo kutapelekea wao kushindwa kupata haki zao kutoka kwa mwajiri na badala yake waendelee kuunga mkono jitihada mbalimbali zinazofanywa na chama cha walimu Tanzania CWT



Washiriki wa  semina hiyo wakiwemo wenyeviti wa chama hicho wilaya za makete na ludewa mbele ya mkuu wa mkoa njombe wameendelea kupaza sauti dhidi ya kero zinazowakabili walimu huku wakionyesha kusikitishwa na kitendo cha serikali wilayani ludewa kuwatoza kodi za nyumba walimu jambo ambalo linarudisha nyuma jitihada za kukuza elimu wilayani humo



HABARI YA HIVI PUNDE:.VILIO NA MAJONZI..JESHI LA POLISI LAFUMULIWA NCHI NZIMA NA IGP

Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Ernest Mangu

Dar es Salaam. Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Ernest Mangu amelifumua Jeshi la Polisi nchini kwa kupanga na kupangua vigogo wake, huku baadhi wakipandishwa nyadhifa.
Pangapangua hiyo imewagusa pia maofisa waandamizi wa jeshi hilo walioko makao makuu, makamanda wa mikoa, wakuu wa upelelezi wa mikoa (RCO) na wakuu wa polisi wa wilaya (OCD).
Habari za uhakika kutoka ndani ya makao makuu ya Jeshi la Polisi zinasema pangapangua hiyo imewagusa pia wakuu wa vikosi, wakuu wa polisi wa vituo (OCS) na polisi wa vyeo cha chini.
Akizungumza na Mwananchi jana, msemaji wa polisi, Advera Bulimba alisema: “Mabadiliko hayo ni ya kawaida ya ndani, hayana uhusiano na kasi ya Rais John Magufuli ila kazi lazima ifanyike.”
Mabadiliko hayo yamekuja ikiwa ni siku chache baada ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kukutana na maofisa wa polisi kwenye Bwalo la Maofisa wa jeshi hilo Oysterbay jijini Dar es Salaam na kati ya mambo yaliyotajwa ni kukumbushana utendaji, uwajibikaji na mpango wa kulifumua jeshi hilo.
Chanzo chetu ndani ya Jeshi la Polisi kimedokeza kuwa orodha ya waliokumbwa na pangapangua hiyo ni ndefu na kwamba orodha ambayo Mwananchi iliiona ni sehemu tu ya maofisa hao.
“Nafikiri IGP ameamua kusuka upya safu ya uongozi ili kuboresha ufanisi katika utendaji wa kazi. Unajua jeshi lazima liendane na falsafa ya Rais Magufuli (John) ya Hapa Kazi Tu,” alidokeza afisa mwingine.
Mabadiliko hayo yamekuja wakati tayari makamanda wa polisi wa baadhi ya mikoa wakiwa wamebadilishwa katika vitengo walivyokuwa awali, wakiwamo Kikosi cha Usalama Barabarani, ili kuboresha utendaji wa jeshi hilo.

Mabadiliko
Katika mabadiliko hayo, Naibu Kamishina wa Polisi (DCP), Salehe Ambika amehamishwa kutoka kitengo cha Sheria na Huduma za Utafiti kwenda kuwa mkuu wa utawala.
DCP Robert Boaz amehamishwa kutoka kitengo cha intelijensia kwenda kuwa mkuu wa kitengo cha uhalifu wa kitaifa na uhalifu wa kupangwa au Transnational and Organized Crime (TOC).
Katika panguapangua hiyo, Kamishna Mwandamizi wa Polisi (SACP), Luteta Modest amehamishwa kutoka kitengo cha sheria kwenda kuwa mkuu wa kitengo cha sheria na huduma za utafiti.
Mkoa wa Kilimanjaro umetikiswa zaidi na mabadiliko hayo baada ya maofisa watano waandamizi kuhamishiwa vituo vipya na nafasi zao kuchukuliwa na sura mpya.
Kamanda wa polisi wa mkoa huo, Fulgence Ngonyani amehamishiwa Chuo cha Polisi Kilwa Road, na RCO Ramadhan Ng’anzi amehamishiwa mkoa wa Shinyanga kuendelea na wadhifa huo.
OCD wa Moshi, Mrakibu Mwandamizi Deusdedit Kasindo amepanda cheo na kwenda kuwa kamanda wa Mtwara, wakati mkuu wa kitengo cha FFU wa mkoa huo, amehamishiwa mkoa mwingine.
Katika mabadiliko hayo, kamanda wa mkoa wa Iringa, Kamishina Msaidizi Ramadhan Mungi amehamishiwa Kilimanjaro kuchukua nafasi ya Ngonyani anayekwenda chuoni.
Nafasi ya RCO wa Kilimanjaro imechukuliwa na SSP Black Magesa aliyekuwa OCD Korogwe.
Kamanda wa Mkoa wa Manyara, ACP Christopher Fuime amehamishiwa Kinondoni kuendelea na wadhifa huo, wakati kamanda wa Ruvuma, ACP Mihayo Miskhela amehamishiwa mkoani Tanga.
Pia, kamanda wa Mkoa wa Tanga, ACP Zuneri Mumbeki amehamishiwa Ruvuma kuendelea na wadhifa huo, huku kamanda wa Kinondoni, SP Camilius Wambura amehamishiwa Mkoa wa Manyara kushika wadhifa huo.
Maofisa wengine ni Gerald Ngichi, ambaye alikuwa OCD Magomeni, amehamishiwa Lindi, Nsekela M. Nsekela (OCD Nyang’wale sasa ofisa mnadhimu II Rorya, Nesto Msembele (OCD Mbalizi sasa Polisi Jamii Mbeya), William Malei (ofisa mnadhimu ll Kigoma, sasa OCD Korogwe), Melard Sindano (OCD Kigoma, sasa OCD Nyang’wale).
Wengine ni Patrilinius Mlowe (OC-CID Kwimba, sasa OCD Kawe, Edson Kasekwa (OCD Makambako, sasa OCD Kilolo), Agustino Titus (mnadhimu ll Morogoro, sasa OCS Malinyi).
Katika pangua pangua hiyo, Raphael Msela (ofisi ya RCO Kagera, sasa naibu RCO Kagera), John Samwel (OCS Malinyi, sasa ofisa mnadhimu II Morogoro), SP Debora Mrema (polisi jamii Mbeya, sasa OCD Mbalizi, SP Omari Mtungu (OCD Tanga, sasa OCD Moshi),SP Alfred Mwaikusa ambaye alikuwa OCS Singida sasa anakwenda kuwa OC-CID Serengeti.
Wengine ni SP Limited Mhongole ambaye alikuwa OC-CID Mbarali sasa anakuwa OCD Mbarali, ACP Jaffar Mohamed (RPC Pwani, sasa makao makuu) na ACP Peter Kakamba anakuwa RPC Iringa.
Pia ACP Mussa Taibu aliyekuwa RCO Shinyanga, sasa anapelekwa upelelezi makao makuu, SSP Pili Omari (OCD Kawe, sasa OCD Mwanga, David Chidingi (OCD Lindi, sasa OCD Magomeni, SSP Constantiono Mbugambi (OCD Mwanga, sasa OCD Ngara), SSP Jullius Lukindo (OCD Mbarali, sasa OCD Mvomero). 

CHANZO: MWANANCHI
Nicki Minaj is rumored to be engaged to rapper Meek Mill, while Minaj’s ex Safaree Samuels is making headlines for his as he is about to drop a diss track on Nicki. Minaj and Samuels dated for nearly fourteen years according to the up-and-coming rapper, who reveals that Nicki ended things after she learned that he wanted to launch his own rap career years after serving as her personal hype man and assistant, TMZ reports. While attending the red carpet event for the taping of Versus and Flow, HipHollywood reveals that Samuels dished about what fans can expect from his upcoming music and comments on rumors that he’s planning a scathing diss track for Minaj. 

Waganga Wasema Dr. Kingwangalla Anatafuta Sifa, Waonya Matumizi Mabaya Ya 'Hapa Kazi Tu'

Monday, December 28, 2015




Waganga wa Tiba Asili Nchini wamepinga tamko la Serikali lenye maagizo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kupiga marufuku waganga hao kujitangaza katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.
 

Waganga hao wamefikia uamuzi wa kupinga agizo hilo la serikali kwa madai kwamba agizo hilo halikushirikisha wadau wote na halikuzingatia sheria ya Tiba Asili na Tiba Mbadala

Wakizungumza kwenye mkutano ulifanyika jana kwenye Ukumbi wa Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam waganga hao kwa pamoja walisema agizo la serikali linaonesha ni kiasi gani wanadharaulika na serikali haijali mchango wao katika jamii na taifa.

Aidha, waganga hao walisema kwamba uwepo wao hapa nchini unalindwa na sheria zilizopo hivyo uamuzi wowote dhidi yao ulipaswa kutangazwa tofauti na ilivyofanya serikali kwa kuwaagiza kupitia vyombo vya habari.

Miongoni mwa wajumbe wa mkutano huo na mdau wa tiba asili Boniventure Mwalongo alisema wao kama waganga wa tiba asili na tiba mbadala hawakubaliani na agizo hilo la serikali kwa kuwa hawakushirikishwa

Naye Mkurugenzi wa Ulcers Clinic Tabibu Rahabu Rubago alieleza jinsi alivyosikitishwa na taarifa za agizo la serikali linalowapiga marufuku kujitangaza hali iliyomsababishia kulazwa hospitalini akidai kwamba wakati anasikia taarifa hiyo alikuwa tayari ametoka kulipia matangazo yake ya mwaka mzima katika kituo cha Star Tv.

Mkurugenzi wa Ulcers Clinic Tabibu Rahabu Rubago akizungumza kwenye mkutano huo alipopata nafasi kuchangia
Tabibu Rahabu Rubago aliendelea kusema kwamba “ Huku ni kurudishana nyuma kimaendeleo ..sielewi ni kwanini serikali inatupiga marufuku. Agizo hili halituumizi sisi watoa huduma pekee bali hata wananchi wake kwa ujumla”

Mbali na hayo, Tabibu Rahabu Rubago alisema kwamba “ mimi nadhani kama kuna eneo tunakwenda kinyume ni vyema serikali ingetuita na kutuambia kupitia mabaraza yetu ili turekebishe eneo hilo lakini hii ya kupiga marufuku tu kijumlajumla kwa kweli haiko sawa”

Pamoja na hayo katika kikao hicho wadau hao wa tiba asili kwa nyakati tofauti walionekana kutupa lawama zao kwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jami, Jinsia, Wazee na Watoto Dk Khamis Kigwangalla huku wakisema kuwa amedandia suala hilo kwa ajili ya kujitafutia umaarufu kisiasa na kuitumia vibaya kauli mbiu ya serikali ya awamu ya tano ya ‘Hapa Kazi Tu’

Haya yote yanafuatiwa na taarifa ya hivi karibuni iliyotolewa na Wizara ya Afya yenye agizo linalowataka waganga wote wa tiba asili wenye vibali vya kutoa huduma hiyo kuwasilisha vibali hivyo katika Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala kwa ajili ya kuvipitia upya vibali hivyo.

Katika agizo hilo  serikali imetoa siku 14 kwa watoa huduma wa Tiba Asili na Tiba Mbadala nchini kuwa wamewasilisha nyaraka zao zote zinazowaruhusu kutoa huduma hiyo na ziwasilishwe kwenye baraza hilo.

Agizo hili lilikuja siku chache baada ya  Naibu Waziri wa Afya Dk Kigwangalla, Desemba 14, mwaka huu kufanya ziara ya kushtukiza katika kituo cha Tabibu Juma Mwaka jijini Dar es Salaam.

Utafiti: Mimba nyingi hutungwa Krismasi



Utathmini wa takwimu kuhusu watoto wanaozaliwa Uingereza umebaini mimba nyingi hutungwa wakati wa Krismasi kuliko wakati mwingine wowote ule wa mwaka.
Takwimu hizo za kipindi cha miongo miwili kutoka Idara ya Taifa ya Takwimu zinaonyesha watoto wanaozaliwa huongezeka sana wiki 40 (miezi 9) baada ya msimu wa sikukuu.
Hili huenda linatokana na wanandoa kutumia muda mwingi pamoja wakisherehekea, au kulenga makusudi mwanzo wa mwaka mpya wa shule ambao huanza mapema Septemba nchini humo.
“Ongezeko la watoto wanaozaliwa mwishoni mwa Septemba ni ishara kwamba mimba nyingi hutungwa wiki chache kabla ya Krismasi na kuendelea hadi siku chache baada ya Krismasi kuliko wakati mwingine wowote wa mwaka,” idara hiyo imesema.
Kawaida watoto 1,800 huzaliwa kila siku lakini idadi hii hupanda hadi 1,974 siku yenye kuzaliwa watoto wengi zaidi ambayo ni Septemba 26.
Siku zinazoshuhudia idadi ndogo zaidi ya watoto wanaozaliwa ni siku za Krismasi, Boxing Dei na siku ya Mwaka Mpya.
Hili sana huenda linatokana na idadi ndogo ya watu wanaopangiwa kujifungua kwa kufanyiwa upasuaji siku hizo, kwani huwa ni siku za mapumziko.
Profesa wa masuala ya uzazi kutoka Chuo Kikuu cha Sheffield Allan Pacey ameambia BBC: “Wazo kwamba mimba nyingi hutungwa wakati wa Krismasi lina msingi. Nina uhakika sherehe na shamra shamra za wakati huu huchangia.”

CCM: Jiwekeni tayari kwa uchaguzi Zanzibar

Samia

Chama cha Mapinduzi kimewataka wanachama wake visiwani Zanzibar kujiandaa kwa marudio ya uchaguzi.
Tamko hilo limetolewa huku mazungumzo hakiendelea kutafuta suluhu ya mzozo kuhusu matokeo ya uchaguzi wa Oktoba 25 ambayo yalifutiliwa mbali.
Wito wa wafuasi kujiandaa kwa marudio ya uchaguzi umetolewa baada ya kikao cha kamati maalum ya halmashauri kuu ya taifa ya CCM Zanzibar katika afisi kuu za chama Kisiwandui.
“Kikao kimewataka wana CCM kujiimarisha, kujiweka tayari na hatimaye kujitokeza kwa wingi katika uchaguzi wa marudio, ili kukiletea ushindi wa kishindo Chama Cha Mapinduzi Zanzibar kuanzia Rais, Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na Madiwani wakati utakapowadia,” taarifa iliyotolewa baada ya mkutano huo inasema.
Chama hicho hata hivyo kinasema kinaridhishwa na mazungumzo yanayoendelea kuhusu mzozo huo Zanzibar.
“Kikao pia kimeridhia majadiliano yanayoendelea kuhusu hali ya Kisiasa Zanzibar yanayoshirikisha Viongozi kadhaa wakiwemo Marais Wastaafu wa Zanzibar,” taarifa hiyo, iliyotolewa na katibu wa kamati maalum ya halmashauri hiyo Bw Waride Bakari Jabu inaongeza.
Jumamosi, Rais wa Muungano wa Tanzania John Magufuli alikutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein.
Akizungumza baada ya mkutano huo, Dkt Shein alisema lengo la mazungumzo hayo ilikuwa ni kumpasha Rais Magufuli juu ya hali ya mazungumzo ya kisiasa Zanzibar.
Mazungumzo hayo yalianza tarehe 9 Novemba na, kwa mujibu wa Dkt Shein, bado yanaendelea.

MSHIRIKISHE MWENZAKO HAPA CHINI

BONDIA FRANCIS CHEKA (SMG) NAMNA ALIVYOTOA NAFASI YA KUPIGWA NA BONDIA THOMAS MASHALI SIKUKUU YA KRISMASI UWANJA WA JAMHURI MOROGORO 2015.

Francis Cheka kushoto na Thomas Mashali kulia. Juma Mtanda, Morogoro. Bingwa wa ngumi za kulipwa Tanzania, Francis Cheka (SMG) amesherehekea vibaya sikukuu ya krismasi baada ya kukung’utwa kwa pointi na bondia Thamas Mashali katika pambano...\
Francis Cheka kushoto na Thomas Mashali kulia.

Juma Mtanda, Morogoro. 
Bingwa wa ngumi za kulipwa Tanzania, Francis Cheka (SMG) amesherehekea vibaya sikukuu ya krismasi baada ya kukung’utwa kwa pointi na bondia Thamas Mashali katika pambano lisilo la ubingwa la raundi 10 uzani wa kg 77 lililofanyika kwenye uwanja wa jamhuri Desemba 25 mkoani Morogoro. 

Faraja pekee kwa Cheka katika pambano hilo ni kuondoka na kitita taslimu cha zawadi cha dola 700 na mdhamini wake Chief Ndamile Mtinginya aliyeahidi kutoa dola 1000 endapo angeshinda pambano na kujikuta ikimegwa na Thamas Mashali aliyepata dola 300 baada ya kumshinda.
Mashali aliweza kushinda pambano hilo dhidi ya Cheka kwa pointi zilizotolewa na majai baada ya pambano kumalizika. 

Jaji namba moja Hamisi Kimanga alimpa, Mashali pointi 94 dhidi ya Cheka 96 wakati jaji namba mbili, Kulwa Makalanga alimpa, Cheka pointi 93 dhidi ya, Mashali 96 na jaji namba tatu, Pasala Chaulembo alitoa pointi 93 kwa, Cheka huku Mashali akipata pointi 97. 

Kutokana na poiniti hizo Mwamuzi wa pambano hilo, Ally Bakari Champion alimtangaza bondia, Thomas Mashali kuwa bingwa. 

Dalili za ushindi kwa Mashali zilizjitokeza mapesa hasa katika raundi ya tatu kufuatia kumsukumia konge zito Francis Cheka aliyeyumba na kuendeleza kumimina ngumi mfululizo zilizomlazimu mpinzani wake ajihami kwa kuziba uso. 

Raundi ya nne bondia Francis Cheka aliweza kujibu mapigo kwa kurusha Makonde yaliyomfanya Thomas Mashali naye aige mbinu ya kuficha uso katika raundi nyingine wakishambuliana kwa zamu. 

Katika raundi ya 10 mabondia hao walicharuka kwa kuongeza umakini mkubwa kwa kurusha ngumi zenye malengo kabla ya kengele ya kuashiria kumalizika kwa mchezo huo uliojaza mamia ya mashabiki wa ngumi.


Francis Cheka kushoto na Thomas Mashali kulia. 

Pambano hilo lilitanguliwa na michezo ya utangulizi kwa mchezo kati ya bondia Deo Njiku wa Morogoro na Vichent Mbilinyi wa Dar es Salaam la raundi sita uzani wa kg 63 ambapo Deo Njiku alipoteza pambano kwa TKO raundi ya pili. 

Njiku alishindwa kuendelea na mchezo baada ya kukung’utwa ngumi nzito na Mbilinyi iliyomchana juu ya jicho na mwamuzi, Kulwa Makalanga kuamuru pambano hilo kumalizika kwa TKO.. 

Katika pambano lingine la utangulizi la raundi sita kg60 bondia Mohamed Matumla wa Dar es Salaam alishinda pambano mbele ya Kudra Tamimu wa Morogoro kwa pointi 97, 98, 95 dhidi ya mpinzani wake Tamimu aliyepata pointi 54, 55 na 54. 

Bondia Mfaume Mfaume wa Dar es Salaam alifanikiwa kumnyamazisha bondia Osama Kaogwa wa Morogoro kwa kumpiga TKO raundi ya kwanza katika uzani wa kg 60 huku pambano la ubingwa kati ya wanadada Lulu Kayage kg50 na Mwanne Haji kg 49, Kayage alifanikiwa kutwaa ubingwa wa TBPC kwa ushindi wa pointi. 

Ushindi huo kwa Kayage alipata baada ya kupata pointi 97,98 na 95 wakati mpinzani wake akipata pointi 93,93,96 wakati Omari Matenga akipata ushindi wa pointi 39, 39 mbele ya Sadik Stolo aliyepata pointi 39, 38 katika pambano la kg 64 la raundi nne. 

Bondia Alex Peter wa Dar es Salaam ndiye aliyeanza pamzia la TKO kufuatia kumtandika mpinzani wak George Marthin wa Morogoro katika raundi ya tatu kati ya raundi nne za mchezo huo.

HATARII; PETER MSINGWA AFUNGUKA ATOBOA SIRI HII JU WABUNGE WA CHADEMA NA POSHO ZA VIKAO BUNGENI



Embedded image permalink

Jose Mourinho aziingiza vitani Real Madrid, Man United



Magwiji hao wa Hispania wanaamini wanaweza wasimpate tena kocha mwenye hadhi wa kuchukua nafasi ya Rafa Benitez kama Mourinho atafanikiwa kumbadili Louis van Gaal pale Old Trafford.

Magazeti ya leo disemba 23

Thursday, December 24, 2015

https://youtu.be/wtxjoX9IAhw

HABARI ZA HIVI PUNDE 25 watekea katika hospitali Saudi Arabia



Takriban watu 25 wameuwa na zaidi ya 100 kujeruhiwa kwenye mkasa wa moto katika hospitali moja iliyo mji wa Jazan nchini Saudi Arabia.
Moto huo ulitokea katika gorofa ya pili ya hospitali ya jazan ambapo vyumba vya kujifungua na vile vya wagonjwa mahututi vipo mapema leo Alhamisi .
Walionusurika na majeruhi wamehamishwa kupelekwa katika hospitali zingine.
Haijabainika kile kilicho sababisha moto huo na sasa uchunguzi unandelea .
Huduma za dharura sasa zimeuzima moto huo.
Picha za tukio hilo zilizochapishwa kwenye jarida la kila siku la Okaz zinaonesha mabaki ya hospitali hiyo yaliyotekekea na kuharibika kabisa.
Mji wa wa Jazan uko karibu na mpaka wa Saudia na Yemen taifa ambalo limesakamawa na vita kati wenyewe kwa wenyewe.
Jeshi la Saudia linasaidia majeshi ya serikali ya Yemen kupamabana na uasi ulioanzishwa na kundi la waasi wa Houthi.
Mapema mwezi huu kombora lililokuwa likielekea Jazan lilidunguliwa na majeshi ya Saudia hata hivyo hivyo haijabainika kufikia sasa iwapo moto huo unauhusiano wowote na mapigano yanayoendelea huko Yemen.

Rais Buhari asema amewabana Boko Haram



Rais wa Nigeria, Mohammadu Buhari, ameiambia BBC kuwa majeshi yake yanakaribia kulishinda kundi la kiislam , Boko Haram. Rais Buhari ameeleza kuwa kundi hilo halina uwezo tena wa kufanya mashambulizi dhidi ya majeshi ya serikali ama maeneo yenye mkusanyiko mkubwa wa watu na kwamba visa vya kujitoa muhanga vimepungua .
Buhari ameeleza kuwa kundi hilo awali lilikuwa na umoja ingawa kwa sasa limesambaratishwa vibaya katika majimbo ya Adamawa na Yobe na kusalia katika jimbo la Borno ambayo ndiyo ngome yao kuu .
Boko Haram wanaripotiwa kuendesha mashambulizi zaidi ya mia moja na kuua watu zaidi ya elfu moja katika kipindi cha miezi miwili iliyopita .
Ikumbukwe kwamba ,wakati wa kampeni zake kuelekea uchaguzi nchini Nigeria,Rais Buhari alitoa ahadi ya kupambana na kundi la Boko Haram mpaka kufikia mwisho wa mwaka huu.

SERIKALI KUVUNJA NYUMBA YA SUMAYE, WAZIRI WA ARDHI ATHIBITISHA


DAR ES SALAAM


WAZIRI Mkuu mstaafu Fredrick Sumaye, ameingia matatani baada ya kudaiwa kuvamia eneo la wazi na kuanza kuzungushia uzio, bila kufuata sheria na utaratibu wa ujenzi.

Eneo hilo la kiwanja namba 719/1/3 lililopo Mkiocheni, mtaa wa TPDC, lilikuwa likitumika kwa ajili ya michezo, mikutano ya kisiasa, pamoja na mikusanyiko mbalimbali ya kijamii.

Kufuatia tuhuma hizo, timu ya maofisa ardhi inachunguza uhalali wa umiliki wake, hivyo wiki ijayo majengo yaliyojengwa kwenye eneo hilo yatavunjwa, endapo ikithibitika kufanya uvamizi huo.

Mbali na Sumaye, vigogo wengine wanaodaiwa wakuvamia kiwanja hicho ni aliyekuwa Katibu Mkuu Mstaafu Ofi si ya Rais, Philemon Luhanjo pamoja na Mbunge wa jimbo la Rungwe, Saul Amon, ambaye ni mfanyabiashara anayemiliki maduka ya S.H. Amon.

Awali kabla ya kuvamiwa kwa eneo hilo, ilielezwa kuwa iliyokuwa kampuni ya High Precision Technology Centre (HPTCMatsutisha), kulilinda lisivamiwe miaka ya 1970.

Hivyo mikusanyiko mbalimbali za kimichezo, pamoja na shughuli za kisiasa ilikuwa ikifanyika katika kiwanja hicho, ambako hata baada ya kampuni hiyo kufa, ililiendelea kutumika kwa shughuli za kijamii.

MAZITO YAIBUKA

Uchunguzi ulibaini kuwa, Sumaye anaendelea na ujenzi katika eneo hilo bila kuweka kibao chenye kuonyesha wakandarasi wanaohusika na ujenzi huo.

Lakini pia, licha baadhi ya nyaraka kudai kuwa kiongozi huyo mstaafu kulimiliki eneo hilo kuanzia mwaka 1998, hajawahi kulalamika kimaandishi kwenye uongozi wa mtaa kuhusu shughuli zilizokuwa zikiendelea kwenye eneo hilo.

Shughuli hizo ni pamoja na uongozi wa serikali ya mtaa kuweka kifusi, ili kusawazisha eneo hilo kuufanya uwanja utumike vizuri kwa ajili ya michezo.

Aidha wiki tatu zilizopita, Ofi sa Mtendaji wa Mtaa huo Mwanaidi Omary, aliongozana na mmoja ya maofi sa wa ardhi wa Manispaa ya Kinondoni hadi kwenye eneo hilo.

Ofi sa huyo wa ardhi alitoa notisi ya mdomo na sio ya maandishi ya kusitishwa ujenzi huo akidai mpaka mmiliki awasilishe nyaraka serikalini.

Licha ya ujenzi huo kufanyika bila kufuata taratibu za kisheria, ikiwemo kutokuwepo kwa kibao kinachoonyesha mkandarasi anayehusika na ujenzi, lakini ofi sa huyo hakuchukua hatua zozote za kisheria.

Katika kutaka kujua ukweli wa mzozo huo, gazeti la uhuru lilifanikiwa kupata barua iliyoandikwa na serikali ya mtaa kwa Halamashauri hiyo kuhoji ujenzi huo. Barua hiyo yenye kumbukumbunamba MKT/SER/MT/ TPDC/05/2015, iliyoandikwa Desemba 11, mwaka huu na kupokelewa Desemba 14, bado haijatolewa ufafanuzi na mkurugenzi kama ilivyokuwa ikielekeza.

LUKUVI KUTUMBUA JIPU

Kufuatia malalamiko hayo ya wananchi, Waziri Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, alisema serikali itavunja uzio na shughuli za ujenzi zinazoendelea kwenye eneo hilo itakapobaini ukweli, ifi kapo Jumatatu.

Katika kusisitiza hilo, Lukuvi alisema hatua hiyo itahusisha hadi vigogo wengine watakaobainika kuvamia eneo hilo.

Alisema baada ya serikali kupata taarifa, timu ya maofi sa ardhi itachunguza kwa kina eneo hilo ili kuthibitisha. Juzi gazeti hili lilishuhudia maofi sa hao wakiwa kwenye eneo hilo wakifanya uchunguzi.


CHANZO: GAZETI LA UHURU


WAZIRI ATUA KATIKA DARAJA LA KIGAMBONI NA KUTOA MAAGIZO HAYA






DAR ES SALAAM


Waziri Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na Walemavu Jenista Mhagama ametembelea mradi wa ujenzi wa daraja la Kigamboni ambapo amehimiza kuharakishwa ujenzi wa mradi huo ili kuwapunguzia wananchi adha ya usafiri pamoja na kupunguza msongamano katika jiji la Dar es salaam.
Katika Ziara hiyo aliyoongozana na Naibu Waziri wa Wizara hiyo Anthony Mavunde Waziri Muhagama amesema msongamano katika jiji la Dar es salaam umekuwa ni tatizo kubwa linalosababisha Serikali kukosa mapato kutokana na muda mwingi kupotea katika foleni za barabarani,
_MG_3722
Kwa Upande wake Mhandisi wa Mradi huo kutoka Shirika la Hifadhi ya Jamii NSSF Mhandisi Msemo amesema mradi huo uliotakiwa ukamilike tangu january mwaka huu ulishindwa kukamuilika kutokana na changamoto mbalimbali na kuahidi kuukamilisha mapema mwakani.
Mradi wa Ujenzi wa Daraja la Kigamboni unaotekelezwa na Mfuko wa Hifadhi ya jamii NSSF pamoja na Serikali umegharimu zaidi ya Dola za Kimarekani milioni 143.5


daraja

Ada Elekezi Shule Binafsi Tayari



TUME ya wataalamu waliokuwa wanakusanya maoni ya wadau wa elimu na kukokotoa ada elekezi kwa shule za msingi na sekondari zisizo za Serikali, wamemaliza kazi yao na tayari wamekabidhi ripoti hiyo kwa Serikali.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Sifuni Mchome amethibitisha kukamilika kwa kazi hiyo na sasa kinachofuata ni uchambuzi wa ripoti pamoja na kuangalia miongozo ya Serikali kabla ya ada elekezi kutangazwa na kuanza kutumika kwa majaribio mwakani Januari.

Wataalamu hao walipewa kazi na Serikali kuandaa ada elekezi baada ya kupata maoni ya wadau mbalimbali wa elimu wakiwemo wazazi, wananchi, wamiliki wa shule binafsi, walimu, asasi zisizokuwa za kiserikali, taasisi mbalimbali za umma na wadau wengine ambao wanaweza kusaidia katika ukokotoaji huo wa ada.

Katika ukokotoaji huo, wizara inaandaa mchanganuo wa gharama za kumsomesha mwanafunzi kuanzia elimu ya awali, darasa la kwanza hadi kidato cha sita kwa nia ya kutoa ada hiyo elekezi ambazo zitaendana na huduma itolewayo kwa shule zisizo za Serikali.

Alisema shule zitakazoteuliwa kuanza kutumika kwa ada hizo zitatangazwa pia na wizara hiyo baada ya kukutana na wamiliki wa shule hizo na kufanya nao mazungumzo.

Alisema majaribio hayo yatafanyika katika baadhi ya shule Tanzania nzima na sio katika baadhi ya mikoa tu.

Serikali Yatangaza ‘Kuminya’ AJIRA za Wageni......Wanaoishi Nchini Bila Kibali Kukiona cha Moto


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga ameagiza waajiri kote nchini kutowapa ajira wageni kwa kazi zinazoweza kufanywa na Watanzania.

Pia, ameagiza maofisa wa Idara ya Uhamiaji kufanya operesheni maalumu kuwatimua raia wote wasio na vibali vya kuishi nchini ifikapo Januari 31, 2016.

Kitwanga ambaye alitembelea idara hiyo jana, alisema wizara yake kwa kushirikiana na Uhamiaji imeanzisha operesheni ya kuwakamata raia wote wa kigeni wanaoishi nchini kinyume cha sheria na kuwachukulia hatua stahiki.

Waziri huyo alisema kutokana na watu wengi kuishi nchini bila vibali, amewapa mwezi mmoja Idara ya Uhamiaji kufanya uchunguzi katika maeneo yote ya kazi na makazi, ili kuwaondoa walioingia nchini kinyemela.

“Katika operesheni hii, tutahakikisha tunawakamata wote na nimetoa maelekezo kwamba nitakuwa nikipewa ripoti kila Ijumaa kuanzia wiki ijayo, mpaka ifikapo Januari 31 tuwe tumesafisha nchi kabisa,” alisema Kitwanga.

Alisema kutokana na mpaka wa nchi kuwa mkubwa, Uhamiaji watawezeshwa ili kukabiliana na tatizo la upitishwaji wa wahamiaji haramu kutoka nchi mbalimbali, kama ilivyoripotiwa hivi karibuni.

Pia, alitoa agizo kwa wananchi wa kawaida kuhakikisha wanatoa taarifa kuhusu wahamiaji haramu walioweka makazi katika maghala, kampuni na viwanda bubu ili kumaliza tatizo la wahamiaji haramu nchini.

Wafanyakazi wageni
Mbali na maagizo hayo, Kitwanga pia aliagiza wamiliki wa kampuni mbalimbali kuhakikisha hawatoi ajira kwa raia wa nje kwa kazi zinazoweza kufanywa na Watanzania.

“…Lakini kazi zote ambazo Watanzania wana utalaamu wa kuzifanya zitafanywa na wazawa na si wageni na zile ambazo inaonyesha wazi kwamba Watanzania hawana ujuzi huo, basi zifanywe na wageni,”alisema Kitwanga.

Kuhusu vibali, Waziri Kitwanga alisema hakuna raia yeyote wa kigeni atakayepata kibali cha kuishi nchini kama hajapata kibali cha kufanya kazi kama amekuja kwa ajili ya kazi. Lakini utaratibu mwingine kama mtu amekuja likizo utaendelea kama kawaida.

Kitwanga alisema kuanzia Jumatatu ijayo, viongozi wa wizara husika na uhamiaji, wakae wapange utaratibu mzuri utakaoonyesha kwamba hakuna usumbufu kwa raia wa kigeni ambaye anakuja kufanya kazi nchini kwa kuzingatia vigezo.

Pasi za kusafiria
Aidha, Waziri Kitwanga alisema mfumo wa uombaji wa pasi za kusafiria na vibali vya ukazi, hivi sasa utakamilishwa kwa njia ya Tehama.

Alisema mwombaji atatakiwa kufanyiwa mahojiano ya ana kwa ana pindi atakapokamilisha utaratibu wa kujaza na kuzilipia fomu hizo benki, na atapatiwa pasi ya kusafiria baada ya siku tatu huku kibali cha ukazi akikipata baada ya siku tano ili kupunguza urasimu.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kulia) akimsalimia Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Sylvester Ambokile wakati alipowasili Makao Makuu ya Uhamiaji, Kurasini jijini Dar es Salaam jana kwa ajili ya ziara ya kikazi. Wapili kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil, na kushoto ni Naibu Katibu Mkuu, John Mngodo.


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (aliyevaa tai) akiwasalimia wananchi  wanaosubiri kupata huduma ya Hati za Kusafiria katika Ofisi za Makao Makuu ya Uhamiaji, Kurasini, jijini Dar es Salaam.


Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Sylvester Ambokile (kushoto) akiwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga, wakati Waziri huyo alipokuwa anafanya ziara ya kikazi Makao Makuu ya Uhamiaji, Kurasini, jijini Dar es Salaam kwa lengo la kujifunza shughuli mbalimbali zinazofanywa na Uhamiaji. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.



Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati) akiwaeleza jambo Watendaji Wakuu wa Idara ya Uhamiaji wakati alipofanya ziara ya kikazi Makao Makuu ya idara hiyo, Kurasini, jijini Dar es Salaam jana. Wapili kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani
 

Most Reading

Eckros Computer Lap 1

Eckros Computer Lap 1

About ETC College

Eckros Tourism College (ETC) started admitting the first intake of students in January 2013. The college falls under tertiary higher education and training as stipulated in education and training policy of 1995.
Also the college administer Distance Learning Programmes, Evening classes, weekend classes, study tours and researchs programmes
Admission Process
New admission into the College is effected twice a year in January-July and July-December.

WALIO PITIA BLOG YETU