ECKROS SCHOOL OF JOURNALISM

eckroscollege. Powered by Blogger.

Blogroll

About

Habari za Mahusiano Kila siku

JOURNALISM STUDENTS AT ETC COLLEGE

JOURNALISM STUDENTS AT ETC COLLEGE

ETC RADIO ONLINE LIVE

http://wwweckrosnewsblogspo.radio12345.com/

Maalim Seif "Kama Vyombo vya Dola Wanayo Azma ya Kunikamata, Mimi Nipo Waje tu Wanikamate"

Thursday, July 7, 2016


Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) Maalim Seif Sharif Hamad amesema Jeshi la Polisi kama lina nia ya kumkamata na kumweka ndani lifanye hivyo kwa kuwa yeye yupo nchini. 


Akizungumza katika Baraza la Eid el Fitri lililofanyika katika ukumbi wa Wakfii wa Ngazija mjini Zanzibar, tofauti na jingine lililofanyika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la zamani na kuhutubiwa na Rais wa
Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein, Maalim Seif alisema nchi inapita katika kipindi kigumu kutokana na dhuluma inayotendwa na watawala dhidi ya raia wasiokuwa na hatia. 


“Huwezi kuamini kuwa dhuluma hii inatendwa na watawala Waislamu. Hali ni mbaya, wananchi wanapata hilaki kubwa baada ya hao wanaojiita Serikali kubaini kuwa hawakubaliki. 


"Mambo hayo yanafanywa kutokana na kushindwa kuzigeuza nyoyo za wananchi ndiyo maana wanafanya hujuma, vitendo vya kikatili na kuwatisha wananchi,” alisema Maalim Seif. 


Maalim Seif alieleza kusikitishwa na hali ya kamatakamata dhidi ya viongozi mbalimbali wa CUF katika ngazi za wilaya na majimbo na kuwekwa ndani huku wakiteswa, kuadhibiwa na kulazimishwa kukubali kushiriki katika vitendo vya uhalifu ambavyo hawakuvitenda. 


Alibainisha kuwepo mwendelezo wa kauli zinazoashiria azma ya kutaka kumkamata yeye, zinazotolewa na baadhi ya wakuu wa vyombo vya dola. 


“Hakuna haja ya kuwatesa watu, iwapo wanayo azma ya kunikamata, mimi nipo waje tu wanikamate,” alisema Maalim Seif. 


Maalim Seif alisema vitendo vyote hivyo ni mwendelezo wa dhuluma aliyoitenda Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) Jecha Salim Jecha, tarehe 28 Oktoba 2015 wakati akifuta matokeo ya Uchaguzi Mkuu kabla ya kuitisha ule wa marudio wa Machi 20. 


Hii ni mara ya kwanza mpasuko wa kisiasa unawaathiri Wazanzibari hata wakati wa Sikukuu ya Eid -El Fitr inayoadhimishwa baada ya kumalizika mfungo ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhan. 


Akihutumia Baraza lililofanyika katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la zamani, Dk Shein aliendelea kukazia kuwa Zanzibar haitakuwa na uchaguzi mwingine mpaka mwaka 2020 kwa kuwa Serikali iliyochaguliwa na wananchi imeshaundwa. 


Katika hotuba hiyo ya takriban dakika 35, alisema hakutakuwa na Serikali ya mpito na kueleza kuwa hayo “yanayosemwa mitaani ni maneno ya wababaishaji.”

No comments:

Post a Comment

 

Most Reading

Eckros Computer Lap 1

Eckros Computer Lap 1

About ETC College

Eckros Tourism College (ETC) started admitting the first intake of students in January 2013. The college falls under tertiary higher education and training as stipulated in education and training policy of 1995.
Also the college administer Distance Learning Programmes, Evening classes, weekend classes, study tours and researchs programmes
Admission Process
New admission into the College is effected twice a year in January-July and July-December.

WALIO PITIA BLOG YETU