Nchi 30 za Ulaya zimeiandikia barua Serikali ya Tanzania zikiomba ifikirie upya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kwenye shughuli za utalii iliyoanza mwezi huu au isianze kutumika hadi mwaka ujao.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango amesema
walipata wazo la kuanzisha kodi hiyo kutoka nchi jirani ya Kenya.
Wakati sheria hiyo ikianza kutumika nchini, nchi hizo za Ulaya ambazo ni wadau wakuu katika sekta ya utalii zimemwandikia barua hiyo Dk Mpango, naibu wake, Dk Ashatu Kijaji na Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe.
Chama cha Kitaifa wa Mawakala wa Usafiri na Wasimamizi wa Utalii (ECIAA) kutoka nchi 30 za Ulaya ndicho kinachoziwakilisha kampuni zaidi ya 70,000 za utalii barani humo.
Nchi hizo ndizo zinazotoa asilimia 50 ya watalii wote duniani.
No comments:
Post a Comment