Google kushirikiana na Fiat Chrysler. Kwa kipindi kirefu Google walishakuwa wazi ya kwamba ingawa wamejikita sana katika utengenezaji wa teknolojia ya magari yajiendeshayo yenyewe mwisho wa siku wao hawatajiingiza kwenye biashara ya utengenezaji wa magari.
Inasemekana Google na Fiat Chrysler Automobiles wapo njiani kukamilisha makubaliano ya utengenezaji wa magari hayo.
Kampuni ya Fiat Chrystler ni kampuni kubwa katika biashara ya magari na hivyo kwa Google kupata m-bia katika utengenezaji wa magari hayo ni dalili nzuri katika hatua ya kuleta magari hayo sokoni.
Katika uhusiano huu; Google atakuwa anachangia mfumo wa
teknolojia wakati Fiat Chrysler inachangia ujuzi, kiwanda na uingizaji wa magari hayo sokoni.Uhusiano huu unaweza fananishwa na uhusiano uliopo kati ya Google na makampuni kama vile HTC, Samsung na wengine katika utengenezaji wa simu spesheli za Google zinazofahamika kwa jina la Nexus…ambapo Google wanasimamia ubunifu wote, utengenezaji unafanywa na makampuni mengine uku suala zima la matangazo (marketing) ya simu hizo ukifanywa na Google.
Suala la maendeleo mazuri ya mazungumzo kuhusu Google kushirikiana na Fiat Chrysler zimevujishwa na mtu anayehusika katika mazungumzo hayo – habari hizo zilitolewa kwa shirika la utangazaji la Reuters. Google na Fiat Chrysler wote hawajatoa taarifa rasmi kuhusu mazungumzo hayo.
Kwa kipindi kirefu inafahamika Google (Tawi la kampuni mama ya ALPHABET) wamekuwa wakijaribu kufanikisha suala hili na makampuni mengine makubwa ya utengenezaji magari kama vile Ford Motos, General Motors n.k lakini makampuni hayo yalikuwa hayajavutiwa na ushirikiano na kampuni ya Google. Matokeo yake kampuni kama vile General Motors wamejiingiza wenyewe pia katika utengenezaji wa teknolojia hiyo kivyao vyao.
No comments:
Post a Comment