Mgeni rasmi ambaye ni Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira akikagua Gwaride la Wahitimu wa Mafunzo ya Awali ya
Uaskari Magereza, Kozi Na. 28 ya Mwaka 2016. Wahitimu wa Mafunzo ya Awali ya Uaskari Magereza, Kozi Na. 28 ya Mwaka 2016 wakila kiapo cha Utii kwa Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama inavyoonekana katika picha wakiwa wakakamavu. Mgeni rasmi akimkabidhi cheti cha sifa mmoja wa Askari Wahitimu ambaye amefanya vizuri zaidi katika nyanja ya Nidhamu katika kipindi chote cha Mafunzo hayo.
Gadi Maalum ya Gwaride la kunyakua iliyoundwa na Wahitimu wa Mafunzo ya Awali ya Uaskari Magereza wakitoa heshima mbele ya Jukwaa la Mgeni rasmi ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi(hayupo pichani). Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakifuatilia kwa karibu Maonesho mbalimbali katika Uwanja wa Gwaride kwenye hafla ya kufunga Mafunzo hayo. Wakufunzi kutoka Kikosi Maalum cha Kutuliza Ghasia Magerezani(KMKGM) wakionesha onesho la kijasiri kama inavyoonekana katika picha.
Kamishna Jenerali wa Magereza, CGP – John Casmir Minja akitoa maelezo mafupi kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi kutoa hotuba yake ya kufunga rasmi kwa Mafunzo ya Awali ya Uaskari Magereza katika Chuo cha Magereza, Kiwira Mbeya. Kamishna Jenerali wa Magereza, CGP – John Casmir Minja(wa pili kulia)akiwa ameongozana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi(wa pili kushoto) mara baada ya sherehe za kufunga Mafunzo ya Awali ya Uaskari Magereza, Chuo cha Magereza, Kiwira Mbeya(wa kwanza kulia) ni Mkuu wa Chuo cha Magereza – Kiwira, SACP. Stanford Ntirundura(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira(katikati) katika Jukwaa akipokea Salaam kutoka kwa Gwaride la Wahitimu wa Mafunzo ya Awali ya Uaskari Magereza(hawapo pichani) katika hafla ya kufunga Mafunzo hayo leo Julai 9, 2016 Chuo cha Magereza, Kiwira Mbeya. Kushoto ni Kamishna Jenerali wa Magereza, CGP- John Casmir Minja.
No comments:
Post a Comment