ECKROS SCHOOL OF JOURNALISM

eckroscollege. Powered by Blogger.

Blogroll

About

Habari za Mahusiano Kila siku

JOURNALISM STUDENTS AT ETC COLLEGE

JOURNALISM STUDENTS AT ETC COLLEGE

ETC RADIO ONLINE LIVE

http://wwweckrosnewsblogspo.radio12345.com/

Jinsi ya Kutambua kama Memori kadi (SD Card) ni feki au la!

Saturday, July 9, 2016

Umekwisha nunua memori kadi (SD Card) ya GB 4, 8 n.k kisha muda wa kuitumia unagundua ni nusu ya ujazo huo uliokua umeandikwa kwenye kadi? Au data zinakuwa zinapotea mara kwa mara…Basi ujue umenunua SD Card feki.

Wengi huwa wanajikuta wanatumia pesa zaidi wakijua wanapata memori kadi ya ukubwa unaoonekana juu ya kadi hizo lakini mwisho wa siku ni utapeli tuu.
Tunashukuru walioulizia juu ya jambo hili na leo tutakufundisha njia kadhaa za kuzitambua kama ni orijino au feki.

> KABLA YA KUNUNUA

Fahamu aina za Memori kadi (SD Card)

Kuna aina kuu tatu. Hapa cha muhimu kujua ni
kuzifahamu hizi alama zake, ukikuta memori kadi imeandikwa ina ukubwa wa GB 8 na huku ukiiangalia haina alama ya familia hiyo basi utambue unanunua kimeo.
Aina
Ujazo 
 
SDSC or SD
Hizi zina ukubwa wa hadi GB 4
 
SDHC sdhc-logo.png
Ukubwa wa GB 4 – GB 32
 
SDXC sdxc-logo.png
Ukubwa wa GB 64 – TB 2
Fahamu tofauti za muonekano wa logo na majina yake, SDSC(SD), SDHC na SDXC…pia kiasi cha ukubwa unaotegemewa kwa aina hiyo ya memori kadi. Ukiona tu haviendani ujue unanunua bomu.  Kuna viwanda vingi bubu vinavyotengeneza memori kadi na kuiga majina ya makampuni makubwa lakini huwa hizo logo wanaweka ovyo ovyo tuu.
memori kadi
Ukiangalia ujazo wa GB zake na alama zilizopo utagundua kadi kadhaa katika hizi ni feki
memori kadi
Chunguza ata boksi kwa nje kabla ya kununua, ukiangalia katika hili na ukilinganisha na maelezo ya aina za memori kadi tulizokupa basi utatambua ni feki

>USHANUNUA NA HAUNA UHAKIKA

Kama umeshainunua na unaona inasumbua sumbua na unataka kujipa uhakikisho wa ubora wake basi fuata njia hizi. Moja ya kwenye kompyuta na nyingine ya kwenye simu.

Kwenye Kompyuta

Kuhakikisha kwenye kompyuta kuna programu kadhaa, leo nitazitaja mbili zaidi zinazoaminika.
Kuna H2testw na FakeFlashTest. Kupitia programu hizi utaweza kufahamu ujazo wa ukweli ulio kwenye memori kadi au ata USB Flash. Hakikisha unazi’test’ mpya mara baada ya kununua ili kujihakikishia na hivyo kuwahi kurudisha kama inawezekana. H2testw ndio maarufu zaidi.
memori kadi usb flash h2testw
"Muhimu kujua: Ni kawaida memori kadi ya ukubwa flani, mfano GB 4, kuwa na kama GB 3.8 hivi badala ya 4 kamili. Tunachoongelea hapa ni tofauti kubwa.

Je wewe ushawahi kuuziwa kimeo? Sasa kupitia tuliyoyaeleza utakuweza kuepukana na hadha hii.

No comments:

Post a Comment

 

Most Reading

Eckros Computer Lap 1

Eckros Computer Lap 1

About ETC College

Eckros Tourism College (ETC) started admitting the first intake of students in January 2013. The college falls under tertiary higher education and training as stipulated in education and training policy of 1995.
Also the college administer Distance Learning Programmes, Evening classes, weekend classes, study tours and researchs programmes
Admission Process
New admission into the College is effected twice a year in January-July and July-December.

WALIO PITIA BLOG YETU