Baada ya Rais John Magufuli kuteua wakurugenzi 187 wapya, baadhi ya wanasiasa na wanataaluma wamesema uamuzi wa kuteua makada wa CCM kushika nafasi hizo za ukurugenzi wa wilaya utaathiri Uchaguzi Mkuu ujao.
Rais Magufuli, ambaye
alikuwa akijielezea kuwa si mwanasiasa, juzi ameteua zaidi ya makada 30 walioshindwa kwenye kinyang’anyiro cha ubunge mwaka jana, kushika nafasi hizo. Ni wakurugenzi 65 tu waliobakizwa.
Hatua hiyo ya kuteua watendaji wa wilaya kutoka miongoni mwa makada waliowahi kugombea uongozi wa kisiasa, umekuja siku chache baada ya Ofisi ya Rais-Utumishi kutangaza makada wengine kushika nafasi ya makatibu tawala wa wilaya, uteuzi ambao pia ulilalamikiwa kuwa unaingiza siasa kwenye utendaji.
“Rais anajenga mfumo wake kwa kuteua watu loyal (watiifu) kwake. Hivyo anaandaa uchaguzi wa 2020 kwa kuweka returning officers (wasimamizi) wake na bado atabadilisha maeneo mengi zaidi kuelekea huko,” amesema Zitto Kabwe, Kiongozi wa ACT Wazalendo.
No comments:
Post a Comment