ECKROS SCHOOL OF JOURNALISM

eckroscollege. Powered by Blogger.

Blogroll

About

Habari za Mahusiano Kila siku

JOURNALISM STUDENTS AT ETC COLLEGE

JOURNALISM STUDENTS AT ETC COLLEGE

ETC RADIO ONLINE LIVE

http://wwweckrosnewsblogspo.radio12345.com/

Taarifa kuhusu uamuzi wa Mahakama Kuu Kanda ya Iringa juu ya mauaji ya Daudi Mwangosi.

Tuesday, July 26, 2016


MAHAKAMA Kuu Kanda ya Iringa imemtia hatiani askari Polisi, Pacificius Cleophace Simoni, kwa kosa la mauaji ya bila kukusudia ya mwanahabari Daudi Mwangosi yaliyotokea Septemba 2 mwaka

NASHUKURU MUNGU KWA KUUTUA MZIGO SALAMA HUKU NIKIIACHA NCHI IKIWA SALAMA TULII KABISA-DKT.JAKAYA KIKWETE


Mwenyekiti Mstaafu wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt.Jakaya Kikwete akizungumza na wananchi na wafuasi wa Chama cha Mapiduzi katika hafla ya kumkaribisha nyumbani mwenyekiti huyo mstaafu wa

Guardiola na Man City wachapwa na Bayern

Wednesday, July 20, 2016

United

Manchester City, wakicheza mechi yao ya kwanza ya kujiandaa kwa msimu mpya chini ya meneja mpya Pep Guardiola, wamechapwa bao moja kwa bila na klabu ya zamani ya meneja huyo Bayern Munich.
City walifungwa bao moja na Erdal Ozturk wa Bayern, ambao kwa sasa mkufunzi wao ni Carlo Ancelotti.
Wachezaji wengi nyota hawakucheza mechi hiyo kwani bado wanapumzika baada ya kushiriki Euro 2016 na Copa America.
Guardiola alichezesha wachezaji 12 wa timu ya vijana, mechi hiyo iliyochezewa Allianz Arena.
Mlinda lango wao alikuwa Angus Gunn, mwanawe mchezaji nyota wa zamani wa Norwich Bryan.
City sasa wataelekea Uchina ambapo watacheza dhidi ya Manchester United siku ya Jumatatu.
Watasafiri na Sergio Aguero, David Silva, Nolito, Raheem Sterling na Joe Hart.

Kikosi cha Manchester City kipindi cha kwanza:

Caballero, Maffeo, Adarabioyo, Kolarov, Angelino, Fernando, Fernandinho, Zinchenko, Barker, Iheanacho, Navas

Kipindi cha pili:

Gunn, Maffeo, Adarabioyo, Kolarov, Angelino, Clichy, Fernando, Fernandinho, Delph, Bony, Navas

Jinsi Askofu Gwajima Alivyokamatwa na Polisi Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere

Monday, July 11, 2016

Hatimaye Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima ambaye amekuwa akitafutwa na Jeshi la Polisi kwa siku kadhaa alikamatwa jana katika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere (JNIA) alipowasili akitokea Japan. 



Baada ya Askofu Gwajima kukamatwa na Kikosi cha Polisi cha Uwanja wa JNIA alipelekwa moja kwa moja Kituo Kikuu cha

SANCHES ATWAA TUZO YA MCHEZAJI BORA KIJANA EURO 2016

Renato Sanches
Mchezaji na kinda wa Mabingwa wapya wa Ulaya Renato Sanches ametajwa kuwa mchezaji bora kijana wa mashindano ya Euro mwaka huu.
Kiungo huyo mwenye uwezo wa hali ya juu kabisa ameshinda tuzo hiyo na

CAF wameipiga faini Yanga ya zaidi ya milioni 9 za kitanzania

July 11 2016 shirikisho la soka Tanzania TFF limetoa taarifa iliyoipata kutoka kwa shirikisho la soka barani Afrika CAFTFF wametangaza maamuzi ya CAF yalioamuriwa juu ya klabu ya Dar es Salaam Young Africans kupigwa faini ya dola

PICHA : Mapokezi ya timu ya taifa ya Ureno baada ya kutua Lisbon na Kombe


Usiku wa July 10 2016 timu ya taifa ya Ureno ilifanikiwa kutwaa Kombe la mataifa ya Ulaya maarufu kama Euro, kwa kuifunga timu ya taifa ya Ufaransa kwa jumla ya

NEWS ALERT:UFAFANUZI KUHUSU TAMKO LA JESHI LA POLISI LA KUPIGA MARUFUKU MAANDAMANO NA MIKUTANO YA HADHARA YA VYAMA VYA SIASA.

Sunday, July 10, 2016

Jeshi La Polisi Tanzania
Ndugu zangu waandishi wa habari. 

Napenda kuchukua nafasi hii kuwapongeza kwa kazi kubwa mnayoifanya ya kuelimisha jamii hususani katika habari zinazosaidia kuzuia uhalifu na kudumisha amani na utulivu wa nchi yetu


Nimewaita leo hii kutoa ufafanuzi kufuatia tafsiri na

Google kushirikiana na Fiat Chrysler katika Uletaji wa Magari Yajiendeshayo Yenyewe

Saturday, July 9, 2016

Google kushirikiana na Fiat Chrysler. Kwa kipindi kirefu Google walishakuwa wazi ya kwamba ingawa wamejikita sana katika utengenezaji wa teknolojia ya magari yajiendeshayo yenyewe mwisho wa siku wao hawatajiingiza kwenye biashara ya utengenezaji wa magari.

Inasemekana Google na Fiat Chrysler Automobiles wapo njiani kukamilisha makubaliano ya utengenezaji wa magari hayo.

Google kushirikiana na Fiat Chrysler
Moja ya magari yanayotumiwa na Google yenye mfumo wa kujiendesha yenyewe
Kampuni ya Fiat Chrystler ni kampuni kubwa katika biashara ya magari na hivyo kwa Google kupata m-bia katika utengenezaji wa magari hayo ni dalili nzuri katika hatua ya kuleta magari hayo sokoni.
Katika uhusiano huu; Google atakuwa anachangia mfumo wa

Jinsi ya Kutambua kama Memori kadi (SD Card) ni feki au la!

Umekwisha nunua memori kadi (SD Card) ya GB 4, 8 n.k kisha muda wa kuitumia unagundua ni nusu ya ujazo huo uliokua umeandikwa kwenye kadi? Au data zinakuwa zinapotea mara kwa mara…Basi ujue umenunua SD Card feki.

Wengi huwa wanajikuta wanatumia pesa zaidi wakijua wanapata memori kadi ya ukubwa unaoonekana juu ya kadi hizo lakini mwisho wa siku ni utapeli tuu.
Tunashukuru walioulizia juu ya jambo hili na leo tutakufundisha njia kadhaa za kuzitambua kama ni orijino au feki.

> KABLA YA KUNUNUA

Fahamu aina za Memori kadi (SD Card)

Kuna aina kuu tatu. Hapa cha muhimu kujua ni

Simba wamficha Mavugo hotelini

Na Erick Mlelwa
WAKATI zikiwapo taarifa kuwa Vital’O ya Burundi imekamilisha usajili wake huku likiwamo jina la Laudit Mavugo, mashabiki wa Simba wanaweza wakaendelea kufurahi kwani straika huyo inasemekana amefichwa na Wekundu hao wa Msimbazi.
Taarifa kutoka Simba zinadai kuwa

Waarabu wa Yanga wamnasa ‘Kamusoko’

NA Erick Pekepeke
KIKOSI cha Mo Bejaia cha nchini Algeria kilichoifunga Yanga bao 1-0 katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, kimezidi kujiimarisha baada ya kusajili kiungo matata kutoka Ufaransa mwenye uwezo mkubwa ndani ya dimba kama ilivyo kwa Thaban Kamusoko na huenda akawepo mchezo wa marudiano Uwanja wa Taifa.
Waarabu hao wamemsajili, Youcef Touati, kutoka katika klabu ya

SHEREHE ZA KUFUNGA MAFUNZO YA AWALI YA UASKARI MAGEREZA ZAFANA CHUO CHA MAGEREZA, KIWIRA MKOANI MBEYA

unnamed28129-1
Mgeni rasmi ambaye ni Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira akikagua Gwaride la Wahitimu wa Mafunzo ya Awali ya

MHASIBU MKUU WA JESHI LA POLISI ASIMAMISHWA KAZI KWA KOSA LA KULIPA MALIPO HEWA


Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Meja Jenerali Projest Rwegasira amemsimamisha kazi Mhasibu Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Frank Charles Msaki kutokana na makosa ya kufanya malipo hewa yaani kulipa posho ya chakula kwa watu ambao si askari.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Wizarani hapo ambayo nakala tumeipata, Mhasibu Mkuu huyo Bw. Frank Msaki anasimamishwa kazi kwa

Serena Williams ameshinda Wimbledon na kutengeneza rekodi mbili mpya, zipo hapa

Serena Williams
Fainali ya mashindano ya tenesi ya Wimbledon kwa upande wa anawake imamalizika kwa Mmarekani, Serena Williams kuibuka mshindi baada ya kumfunga Mjerumani, Anelique Kerber.
Serena amefanikiwa kushinda taji hilo kwa kumfunga Angelique seti 7-5 na 6-3, ushindi ambao

Nchi 30 za ulaya zimeiandikia barua serikali ya tanzania kufikiria upya Kodi ya Utalii


Nchi 30 za Ulaya zimeiandikia barua Serikali ya Tanzania zikiomba ifikirie upya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kwenye shughuli za utalii iliyoanza mwezi huu au isianze kutumika hadi mwaka ujao.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango amesema

Uteuzi wa wakurugenzi 187 wazua hofu kwa Zitto

magu new2
Baada ya Rais John Magufuli kuteua wakurugenzi 187 wapya, baadhi ya wanasiasa na wanataaluma wamesema uamuzi wa kuteua makada wa  CCM kushika nafasi hizo za ukurugenzi wa wilaya utaathiri Uchaguzi Mkuu ujao.
Rais Magufuli, ambaye

RAIS DKT. MAGUFULI AHUTUBIA KATIKA BARAZA LA EID EL FITRI JIJINI DAR ES SALAAM

Thursday, July 7, 2016


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Sheikhe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhadi Mussa Salum mara baada ya kuwasili

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais

SUPER STAR LULU HATIMAYE AKATA MZIZI WA FITNA,AMWEKA HADHARANI MPENZI WAKE


Baada ya kuka muda bila kumuweka maisha yake ya mahusiano hadhari hatimaye leo muigizaji wa bongo amepost picha yake akiwa na boyfriend wake.
Elizabeth Michael maarufu Lulu, empost picha kwenye ukurasa wake wa Instagram na kuandika maneno haya“Baba Na Mama Squad katika harakati za Mapozihaikuwa rahisi Na Yebo Yebo zangu Na kilemba

…No make upSema Poa tu
Goodnight lovies”
Picha yenyewe halisi ndiyo hii

18

Maalim Seif "Kama Vyombo vya Dola Wanayo Azma ya Kunikamata, Mimi Nipo Waje tu Wanikamate"


Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) Maalim Seif Sharif Hamad amesema Jeshi la Polisi kama lina nia ya kumkamata na kumweka ndani lifanye hivyo kwa kuwa yeye yupo nchini. 


Akizungumza katika Baraza la Eid el Fitri lililofanyika katika ukumbi wa Wakfii wa Ngazija mjini Zanzibar, tofauti na jingine lililofanyika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la zamani na kuhutubiwa na Rais wa

URENO YATINGA FAINALI YA EURO 2016,YAILAZA WALES 2-0


Ulikuwa mtanange wa kukata na shoka wa nusu fainali ya michuano ya Euro 2016 inayotimua vumbi kule nchini Ufaransa kati ya Wales iliyokuwa ikiongozwa na Gareth Bale na Ureno ikiongozwa na Christian Ronaldo.

Mtanange huo ulio kanyagwa katika dimba la Parc de Olimpique jijini Lyon, ulichezeshwa vizuri na mwamuzi Jonas Eriksson wa

Siku sita za mwandishi kuuza baa (3)

Wednesday, July 6, 2016


By Jackline Masinde, Mwananchi jmasinde@mwananchi.co.tz
Jana simulizi hii iliishia wakati mteja aliponiambia nichukue Sh5,500 zilizobaki kwenye Sh10,000 baada ya kuniagiza nimletee bia moja na viroba viwili. Hii ilikuwa siku ya kwanza tangu nianze kazi ya uhudumu baa. Sasa endelea...
Nikiwa nimekaa akanifuata Matroni Rukia. Akanionyesha baba moja aliyekuwa amekaa kaunta akinywa na kuniomba nikaonane naye.
“Unamuona yule baba pale aliyevaa shati la kijivu?” anauliza huku akinionyesha na kisha ananiambia: “Nenda kaonane naye.”
Naenda kwa mwanamume huyo na baada ya kufika ananishika mashavu yangu huku akisema: “Sasa umeniona mtoto mzuri?
“Wenzako hawajakwambia taratibu za hapa?”
Nikamjibu: “Hawajaniambia, kwani kuna taratibu zipi?”
Akacheka na kunijibu akisema: “Kwani matroni alivyokwambia uje kuniona hajakwambia?”
Nikamjibu kuwa hakuniambia kitu zaidi ya kunielekeza nije kukuona, nikijua pengine unahitaji kuhudumiwa kinywaji.
Anacheka kisha ananiuliza: “Wewe ni raia wa Tanzania kweli? Nikamjibu ndiyo. Akasema: “Hapana. Wewe utakuwa Mkenya, hata lafudhi yako inaonekana wewe ni Mkenya na mwonekano wako pia. Sema ukweli kabla hatujakuitia uhamiaji. Sikiliza umeshapata bwana?”
Nami nikamuuliza kwa mshangao nikisema: “Bwana!”
“Ndiyo” akanijibu nami nikamwambia kuwa bado sijampata.
“Sasa nataka mimi niwe mume wako,” akasema.
“Hapa huwa kuna taratibu kama hawajakwambia wenzako. Ukiwa hapa lazima uwe na mwanaume wako ambaye atakutunza wewe siku zote unapokuwa hapa.”
Akaniambia kuwa anataka niwe mke wake kuanzia muda huo na nifanye shughuli zangu zote, nikimaliza atakuja kunichukua kwenda kulala naye nyumba ya wageni.
Nikaamua kumuacha na kuondoka. Nilipofika sehemu niliyokuwa nimeketi, matroni akaniuliza: “Eeh! niambie kakwambiaje?”
Nikamuelezea jinsi yule baba alivyoniambia na matroni akacheka kisha akaniambia kuwa ndivyo wanavyoishi kwenye baa hiyo.
“Wenzako wote wana waume zao wanaowatunza,” akasema matroni.
Nikabaki kinywa wazi aliposema wanaume wa aina hiyo ndiyo wanaowaleta wateja, yaani ni madalali wao. Hivyo, malipo yao ni kutembea na wahudumu wa baa hiyo na kuwapa ofa ya bia.
“Huwa wanaitwa ‘Sinaga Hela’,” akasema matroni.
Nikamuuliza itakuwaje kama sijampenda. Je, utanilazimisha?
“Hiyo ni lazima, haina cha kupenda wala kutopenda. Hao ndiyo wanaweza wakachagua uendelee kufanya kazi baa hii au uondoke kulingana na utakavyoweza kumhudumia mmojawapo kitandani na hasa anapokuwa amelewa.
“Pia, mwanaume huyo atakapokuja na wateja wake, atakuchagua wewe kwenda kuwahudumia. Siyo kwa vinywaji pekee bali hata huduma ya ngono kama watakuhitaji na yeye atatoa ruhusa na kiasi cha fedha utakacholipwa utakapotoa huduma hiyo kwa wateja anaowaleta.
“Kama utaweza kuwahudumia vyema, wateja hao wakavutika kurudi tena, hiyo ndiyo heshima yako na unaweza kupandishwa cheo,” akaniambia matroni.
Hakika haya ni ‘mashikoro mageni’ kama wajisemeavyo Wasukuma.
Lakini naambiwa na matroni huyo kwamba ukiwa na mwanaume huyo, huruhusiwi kuwa na mwingine na ikitokea mwanaume mwingine anataka kutoka na wewe, yule ambaye wamekuchagulia anatakiwa kulipia fedha kaunta Sh5,000, lakini haruhusiwi kuwa na uhusiano wa muda mrefu wa kimapenzi na wewe.
Ikitokea umempenda mwanaume tofauti na huyo uliyetafutiwa au yule anayekulipia Sh5,000 kaunta, itabidi iwe siri na bosi wako asijue, lakini ni lazima umwambie matroni wako na huyo ndiye atakufichia siri.
Hata unapotoka kwenda kustarehe na mwanaume huyo, ni lazima uache chochote kwa matroni.
Hakika ukistaajabu ya Mussa basi utayaona ya Firauni. Baada ya kupokea maelezo hayo kutoka kwa matroni, anaondoka na kuniacha nikiwa nimekaa peke yangu huku nikitafakari jambo hilo.
Mara anakuja mhudumu mwenzangu niliyemfahamu kwa jina la Neema. Ananiuliza sababu za kukaa peke yangu. Nikamjibu kuwa kuna baba mmoja kaniambia niwe mke wake.
“Mimi sipendi, halafu hata sijampenda. Kwanza mwanaume mwenyewe mzee, halafu matroni anasema ni lazima niwe naye kwa kuwa ndiyo taratibu za hapa.”
Neema akanicheka akisema, “ndiyo hivyo mama. Kwani wewe hujawahi kufanya kazi hizi? Ukija kufanya kazi ya baa, lazima ukubaliane na kila kinachokuja mbele yako”.
“Hapa kila mtu ana mwanaume wake. Siku akikuhitaji, bosi au matroni anakwambia mapema unafanya kazi zako zote ukimaliza unaondoka,” anasema.
“Wao ndiyo wanaotuhudumia. Hata mimi ninaye. Ni mtu mzima ana mke na watoto.”
Wakati nikiongea na Neema, mara anaitwa kuhudumia mteja mwingine na hivyo kuniacha nikiwa nimekaa peke yangu. Baada ya muda mfupi, anakuja rafiki yangu Sharifa na ananiambia nimpe mchapo.
“Shoga yangu nimekuona unaongea na baba pale, vipi ndo bwana nini?” Ananiuliza.
Nikamjibu, “hapana.”
“Mwanaume mwenyewe mzee mimi nitampeleka wapi?” nikasema na kusababisha acheke.
“Acha ujinga wewe. Mbona mimi ninaye mtu mzima ana pesa! Hapa anasubiri Mfungo wa Ramadhani uishe akanipangishie chumba,” anasema Sharifa huku akipepesa macho na kubinua midomo yake.
“Pia, nina bwana wangu mwingine ambaye anamjua matroni peke yake ana pesa balaaa.”
Sharifa ni msichana wa miaka 16 na anasema ameshatoa mimba mara mbili.
“Rafiki yangu, kwa hiyo wewe una wanaume wangapi hapo ulipo?” nikamuuliza.
“Loh! shoga yangu hapa mjini. Siwezi nikawahesabu, ila wengi ni wale ambao nawatumia kuwachuna pesa tu. Wanaweza kufika kumi, lakini wapo wale wa dharura, hao ni wengi sijui hata idadi,” anasema binti huyo ambaye wenzake wanamuita “digidigi”.
Msichana huyu ni mjanja machoni, ni mdogo lakini wanasema ni hatari na wenzake wanamchukia kwa sababu anawachukulia wanaume wao.
“Yule baba ana pesa, mkubali,” ananishauri.
Wakati tukiendelea na maongezi, wale wateja niliowahudumia mzinga wa konyagi wananiita. Nilipoenda, wakaniambia wanataka nikae nao.
“Mbona umetutenga? Unakaa na wenzako tu unatuacha. Hebu njoo ukae hapa, ninaketi kisha mmoja wa wateja hao aliyejiita ni ‘usalama wa taifa’, akaanza kunitongoza akitaka niondoke naye usiku huo.
Ninamkatalia, jambo lililomfanya apayuke “sijawahi kumtongoza mwanamke wa baa akanikatalia nakushangaa wewe. Fredy (meneja wa baa) kakutoa wapi? Mbona hujakaa kama wenzako?”
Aliendelea kubembeleza anataka niwe ‘mtu wake’ kwa siku hiyo tu na kwamba atanipa fedha.
“Unasikia mama. Kwanza najua hujala, naomba nikununulie chakula ule baadaye tunaondoka,” anasema baba huyo.
Wakati nikiendelea kuzungumza na ‘mwanausalama’ huyo, Sharifa ananiita na kuniuliza nachoelezwa na huyo mwanaume.
Nilipomweleza, akasema huyo mwanaume hana pesa.
“Fanya hivi, kama kakwambia anakununulia chakula, wewe kubali. Mlie hivyo viela vyake, uachane naye,” anasema Sharifa.
Nikarudi kukaa na huyo baba ambaye alimuita mhudumu wa chakula na kumwagiza atengeneze nyama choma na ndizi. Baada ya saa moja, chakula kikaletwa na tukala wote tuliokuwa kwenye meza hiyo, akiwamo Sharifa.
Baada ya kula, Neema akarudi na kuniita pembeni kukaa naye.
“Vipi sasa? Tunakaribia kufunga, utaondoka na yule baba? Nikamjibu hapana na kwamba sijamuona muda mrefu.
“Atakuwepo kama amesharuhusiwa na bosi uondoke naye, lazima utaondoka naye. Labda cha kufanya, jifanye unaumwa ndiyo itakuwa ponapona yako.”
Nikaamua kufanya kama alivyoniambia Neema. Wakati huo ilikuwa imetimia saa 5.00 usiku. Kaunta kulishafungwa na kubakia ukumbi wa baa ambako walikaa watu wachache wakitazama mpira.
Mara baba anayejiita ‘usalama wa taifa’ akanifuata na kunisisitiza niondoke naye, lakini nikakataa mbele ya Neema. Baadaye wahudumu tukaondoka kwenda ndani kulala.
Tukiwa ndani au gheto, matroni akaniuliza vipi mbona hujaenda?” akimaanisha sijaenda kulala na mwanaume niliyekabidhiwa.
Nikamwambia kuwa naumwa ugonjwa wa kikubwa, akaniuliza tena kama niliongea naye na kukubaliana naye kwamba nisiende alikotaka.
Nikamweleza kuwa sikumwambia, jibu lililomfanya matroni aende nje kumweleza, kisha akarudi na kusema: “Mtu mwenyewe keshalewa, hata hajitambui. Wewe lala tu mtamalizana kesho.”
ITAENDELEA KESHO
 0.6k

Maharusi wafariki dunia ajali ya City Boy





TRA :Mapato Bandarini Yameongezeka Zaidi

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imesema kupungua kwa mizigo bandarini kumeathiri si Tanzania pekee bali dunia nzima na kwamba kubanwa kwa mianya ya wizi kumesababisha kuongezeka kwa mapato kutoka Sh bil 458 Aprili mwaka huu kufikia Sh bil 517. 


Aidha, TRA imesema

Wateja wa Vodacom kujichagulia vifurishi wavitakavyo #YaKwako2

Katika dhamira yake ya kufanya ubunifu wa teknolojia kwa ajili ya kuwapeleka watanzania katika ulimwengu wa sayansi na teknolojia kwa kuwapatia huduma bora za kurahisisha maisha na kwa gharama nafuu, kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania imezindua ofa mpya maalum kwa wateja wake inayojulikana kama “Ya kwako tu” itakayowawezesha  kujipatia vifurushi vya gharama nafuu kwa kadri ya matakwa yao wapendayo kuanzia vya huduma ya kuperuzi intaneti (Mitandao ya kijamii, Youtube, Whatsapp na kadhalika), kupiga simu (Kuenda mitandao yote) na kutuma ujumbe mfupi wa maneno.

Mkurugenzi wa mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia (katikati) akifafanua jambo wakati wa

Taarifa kuhusu kuanzishwa kwa rajisi kuu ya namba tambulishi za mikononi

Ndugu Waandishi wa Habari;

Tumewaita hapa leo ili tuwapatieni taarifa ya utekelezaji wa mpango wa kuzuia simu bandia za kiganjani zisitumike kwenye mitandao ya simu hapa nchini.

Kama ambavyo mnakumbuka, usiku wa tarehe 16 Juni 2016 simu bandia zilizuiwa kutumika katika mitandao ya

Niyonzima akana kumuuza Samatta kwa AS Roma


Kwa ufupi

  • Katika mtandao wa twitter akaunti yenye jina la
 

Most Reading

Eckros Computer Lap 1

Eckros Computer Lap 1

About ETC College

Eckros Tourism College (ETC) started admitting the first intake of students in January 2013. The college falls under tertiary higher education and training as stipulated in education and training policy of 1995.
Also the college administer Distance Learning Programmes, Evening classes, weekend classes, study tours and researchs programmes
Admission Process
New admission into the College is effected twice a year in January-July and July-December.

WALIO PITIA BLOG YETU