ECKROS SCHOOL OF JOURNALISM

eckroscollege. Powered by Blogger.

Blogroll

About

Habari za Mahusiano Kila siku

JOURNALISM STUDENTS AT ETC COLLEGE

JOURNALISM STUDENTS AT ETC COLLEGE

ETC RADIO ONLINE LIVE

http://wwweckrosnewsblogspo.radio12345.com/

WAKAZI WA MLANDIZI WASOGEZEWA HUDUMA ZA MAWASILIANO.

Sunday, April 24, 2016


Wakaazi wa Mlandizi wasogezewa huduma za mawasiliano na Vodacom Tanzania


Wakazi wa Mlandizi mkoa wa pwani na vitongoji vyake,Wamerahisishiwa jinsi ya kupata huduma mbalimbali za huduma za mawasiliano kwa kuzinduliwa kwa duka jipya na la kisasa la Vodacom Tanzania lililozinduliwa leo ukiwa ni mkakati uliowekwa na kampuni hiyo kwa kusogeza huduma za mawasiliano karibu na wananchi nchini kote.Mwaka huu kampuni hiyo imedhamiria kufungua vituo vipatavyo 500 nchini kote. 
Kituo hiki kipya kinatarajia kutoa huduma kwa wateja wa Vodacom wanaoishi Mlandizi na vitongoji jirani ambao walikuwa wanatembea  mwendo mrefu kufuata huduma pia kitahudumia wasafiri  mbalimbali wanaotumia barabara ya morogoro. 
Ofisa Mtendaji Mkuu wa kitengo cha Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Tanzania,Hassan Saleh amesema  kuwa mkakati huu wa kufungua vituo vya kutoa huduma za Vodacom umebuniwa ili kuwapunguza wateja adha ya kutembea umbali mrefu kwa ajili ya kupata huduma. 
“Kwetu Vodacom wateja wetu ni wafalme na tunasikiliza ushauri wao,pamoja na kuwa na maduka sehemu mbalimbali lakini bado tumeona kuna haja ya kuwasogezea zaidi huduma wateja  wazipate popote pale walipo na kwa wakati wowote”.Alisema.
Aliongeza kuwa  kupitia huduma hii ya  vituo vya mauzo kampuni itazidi kupanua wigo wa ajira nchini kwa kuwa watanzania zaidi ya 1000 watanufaika na mpango huu na  ni utekelezaji wa  moja ya malengo ya kampuni ambayo ni kufanya uwekezaji wenye mwelekeo wa kuwanufaisha watanzania. 
Akifungua kituo hicho kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Pwani, Kaimu Katibu tawala wa Wilaya hiyo,Anathory Mhango aliipongeza kampuni ya Vodacom kwa kusambaza huduma zake karibu na wateja na aliwataka  wakazi wa Mlandizi kutumia huduma za mawasiliano kwa ajili ya kurahisisha maisha. 
Mmoja wa wakazi wa Mlandizi Sheikh Daruwesh Mohamed Luhanjo akiongea kwa niaba ya wakazi wenzake alisema kuwa kufunguliwa kwa duka hilo kutawapunguzia kero wakazi wa eneo hilo kutembea umbali mrefu kufuata huduma za Vodacom “Tunashakuru Vodacom kwa kutukumbuka wana Mlandizi”alisema.

No comments:

Post a Comment

 

Most Reading

Eckros Computer Lap 1

Eckros Computer Lap 1

About ETC College

Eckros Tourism College (ETC) started admitting the first intake of students in January 2013. The college falls under tertiary higher education and training as stipulated in education and training policy of 1995.
Also the college administer Distance Learning Programmes, Evening classes, weekend classes, study tours and researchs programmes
Admission Process
New admission into the College is effected twice a year in January-July and July-December.

WALIO PITIA BLOG YETU