wananchi wa kijiji cha mbalamaziwa wilaya ya mufindi mkoani iringa wamelaani vitendo wanavyotendewa na uongozi wa kijiji na kata kuapa kuto kukubali kuendelea kuongozwa nao kwa madai kuwa wanadumaza kasi ya maendeleo kijijini hapo
ZAIDI NA PROSPER MFUGALE KUTOKA MBALAMAZIWA MUFINDI
wananchi wa kijiji cha mbalamaziwa Wanaeleza baadhi ya mambo yanayo wakera dhidi ya viongozi wa serikali kuwa ni pamoja na kitendo cha uongozi huo kuuza mradi wa maji kwa kampuni ya wachina wanaotengeneza barabara ya iringa mbeya kijijini hapo mradi ambao ulikuwa unanufaisha vijiji zaidi ya sita na sasa vijiji hivyo vinakosa maji
Pia wamesema kuwa mara nyingi uongozi umekuwa ukiwatoza faini pamoja na kuwabambikizia kesi kupitia ofisi za kijiji kata na kituo cha polisi malangali pindi wanapo hoji matumizi ya fedha za miradi ya maendeleo
Mgeni sakalinga, charles mhumbi, na sharifu utenga ni miongoni mwa wananchi ambao wameeleza vitendo vya ukatili wanavyo fanyiwa na uongozi wa kijiji na kata ya mbalamaziwa
Mtendaji wa kijiji Steeven lumato na Elizabert ngwaeje afisa mtendaji wa kata wamaeeleza sababu za wananchi kuwakana
Jitihada za kumpata mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya mufindi Saada Malunde na uongozi wa wilaya Kutolea ufafanuzi malalamiko ya wananchi kuhusu watendaji hao bado zinaendelea
No comments:
Post a Comment