Dwight Yorke ameishauri Bodi ya Aston Villa kumpa Nafasi iliyo wazi ya Meneja wa Klabu hiyo.
Villa sasa wanasaka Meneja wao wa 3 Msimu huu baada ya Remi Garde kuachia ngazi Wiki iliyopita.
Garde, ambae alimbadili Tim Sherwood Mwezi Novemba hapo Villa, ameonekana kuwa chaguo bovu baada ya kushinda Mechi 2 kati ya 20 za BPL, Ligi Kuu England.
Hivi sasa Villa wapo mkiani mwa BPL na kupona kwao wasishuke Daraja itakuwa ni miujiza mikubwa.
Lakini Dwight Yorke, alieichezea Villa kati ya 1989 na 1998 na kuifungia Bao 97 katika Mechi 292 kabla kuhamia Man United, amesisitiza yeye anaweza kuwa na mafanikio makubwa akipewa fursa ya kuiongoza Klabu hiyo.
Akiongea, Yorke, ambae alikuwa na mafanikio makubwa akiwa Mchezaji wa Man United, ameeleza: “Wamejaribu uzoefu, wamejaribu Mameneja wasiojulikana na hawajapatia. Nahisi watatafuta Mtu mzoefu lakini wakati mwingine unahitaji Mtu anaeijua Klabu ya Soka na ambae ataleta uchangamfu kwenye Klabu!”
Yorke aliongeza: “Watu hawajui nimetwaa Ubingwa wa Daraja la chini Championship. Hiyo ilikuwa mara pekee nilipocheza nje ya Ligi Kuu England nikiwa na Sunderland kwenye Championship. Hivyo naijua Ligi hiyo kama Mchezaji. Nawafahamu Wachezaji wa Villa na utamaduni wote wa Klabu hiyo!”
Yorke amesisitiza: “Nitaiomba kazi hii ya Meneja wa Villa na natumai watanipa nafasi ya usaili. Nina uzoefi mkubwa na nilicheza chini ya Mameneja Bora na nimeongea na Sir Alex Ferguson ambae amenipa sapoti kwa kazi hii! Naamini naiweza na wanipe tu nafasi ya usaili!”
LIGI KUU ENGLAND
Ratiba:
Jumamosi Aprili 9
1445 West Ham v Arsenal
1700 Aston Villa v Bournemouth
1700 Crystal Palace v Norwich
1700 Southampton v Newcastle
1700 Swansea v Chelsea
1700 Watford v Everton
2030 Man City v West Brom
Jumapili Aprili 10
Jumapili Aprili 10
1530 Sunderland v Leicester
1800 Liverpool v Stoke
1800 Tottenham v Man United
Jumatano Aprili 13
2200 Crystal Palace v Everton
No comments:
Post a Comment