ECKROS SCHOOL OF JOURNALISM

eckroscollege. Powered by Blogger.

Blogroll

About

Habari za Mahusiano Kila siku

JOURNALISM STUDENTS AT ETC COLLEGE

JOURNALISM STUDENTS AT ETC COLLEGE

ETC RADIO ONLINE LIVE

http://wwweckrosnewsblogspo.radio12345.com/

WABUNGE WANAOSHIRIKI VIKAO VYA BUNGE LAKINI HAWACHANGII CHOCHOTE SASA KUTUNGIWA SHERIA

Thursday, April 28, 2016


Kiti cha Spika wa Bunge kimesema ipo haja ya kufanya marekebisho ya Sheria pamoja na Kanuni ili kila mbunge apate posho kulingana na kazi aliyofanya bungeni, badala ya utaratibu wa sasa wa kuangalia mahudhurio pekee. 
Aidha, kimewataka wabunge kubadilika na kuacha tabia ya kuchukua posho za vikao vya Bunge bila kuzitolea jasho.
Kauli hiyo imekuja kutokana na Mwongozo ulioombwa Aprili 25, mwaka huu na Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe (CCM) ambaye alikitaka kiti cha Spika kutoa Mwongozo kuhusu usahihi wa wabunge wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kulipwa posho na mishahara wakati hawashiriki na kutimiza wajibu wao wa kuchangia kwenye mjadala wa Bunge la Bajeti linaloendelea katika Mkutano wa Tatu wa Bunge la 11.
Bashe alisema mbunge huyo alitumia Kanuni ya 68(7) ya Kanuni za Kudumu za Bunge akiomba Mwongozo wa Spika kutokana na Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, kuamua kutoshiriki mjadala unaoendelea bungeni, lakini wabunge hao wanasaini na kulipwa mishahara na posho.

Hivyo akaomba Mwongozo endapo ni haki kwa wabunge hao kupokea posho wakati hawashiriki wala kutimiza wajibu wao wa kisheria. 

Katika kujenga hoja hiyo, Bashe alitumia Ibara ya 63(3) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania isemayo, “Kwa madhumuni ya utekelezaji wa madaraka yake Bunge laweza kujadili utekelezaji wa kila Wizara wakati wa Mkutano wa Bunge wa kila mwaka wa bajeti.”

Aidha, Bashe alitumia Ibara ya 73 ya Katiba ya Tanzania kufafanua kuhusu malipo ya mshahara, posho na malipo mengine kwa wabunge. 

Akitoa Mwongozo wa Spika, Naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson alisema kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania, Ibara ya 73 imeainisha masharti ya kazi ya wabunge.

Alisema mbunge anastahili kulipwa mshahara kwa kila mwezi, na kufafanua kuwa mbunge anapohudhuria vikao bungeni na kamati atalipwa posho ya vikao kwa kiwango kitakachowekwa na Serikali na Kanuni za Bunge. 

Alisema malipo ya mshahara ni suala la Kikatiba na Sheria hulipwa kwa mbunge kutokana na kazi yake ya ubunge.

Hivyo malipo ya posho kwa wabunge yanatokana na mahudhurio yao bungeni na siyo kwa kuchangia kama ambavyo wengi wao wanapenda iwe hivyo. 

“Kimsingi kuhudhuria bungeni pekee siyo njia inayopendeza kwa kuwa mbunge anapofika bungeni anatarajiwa atekeleze majukumu yake yalivyoainishwa katika Ibara ya 63.

“…Tabia hii ya kutochangia mijadala na kuzunguka zunguka bungeni haikubaliki na haitakiwi kuendelea, kila mbunge atekeleze wajibu wake na sio anahudhuria ili alipwe posho,” alisema Dk Ackson.

Wakati huo huo, Spika wa Bunge, Job Ndugai amefanya mabadiliko katika Kamati mbalimbali za Bunge, kwa kubadilisha wabunge 16 wa Kamati za Awali kwenda nyingine. 

Aidha, Spika amewapangia Kamati wabunge wapya wanne, walioapishwa mwanzoni mwa Mkutano huu wa Bunge, ambao ni Shamsi Vuai Nahodha, Rita Kabati, Oliver Semuguruka na Lucy Owenya.

RAIS MAGUFULI ATENGUA UTEUZI WA MKURUGENZI MTENDAJI WA TIC


Mwanasiasa wa miaka 90 kuoa mwanamume Marekani

Monday, April 25, 2016

Harris Wofford

Seneta mmoja wa zamani wa Marekani, ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 90, ametangaza kwamba atamuoa mwanamume wa umri wa miaka 40.
Wawili hao watafunga ndoa mwishoni mwa mwezi huu.
Harris Wofford, aliyehudumu katika utawala wa Rais J F Kennedy kama msaidizi maalum aliyehusika na masuala ya haki za raia, aliachwa akiwa mjane baada ya mkewe Clare kufariki kutokana na saratani ya damu miaka 20 iliyopita.
Walikuwa wameishi katika maisha ya ndoa kwa miaka 48.
Akiandika katika gazeti la New York Times, Bw Wofford amesema anajihisi mwenye bahati sana kuishi katika enzi ambazo Mahakama ya Juu Marekani imetambua kwamba “ndoa haitegemeu maumbile ya mtu kijinsia, uamuzi au ndoto za mtu.”
“Msingi wake ni upendo.”
Mwanamume atakayeolewa naye ametambuliwa kama Matthew Charlton.
Wofford alihudumu wakati mmoja kama seneta wa chama cha Democratic akiwakilisha jimbo la Pennsylvania.
Aidha, alihudumu kama mshauri wa Dkt Martin Luther King Jr.
"Mnamo Aprili 30, katika umri wa miaka 90 na 40, tutaunganisha mikono yetu, tukiapa kuunganizhwa pamoja (kwenye ndoa): kuwa pamoja na kuishi pamoja, kwa mema na kwa mabaya, kwa utajiri na umaskini, katika maradhi na katika afya bora, kupenda na kuenzi, tangu kifo kitutenganishe," amehitimisha Wofford katika makala yake iliyochapishwa katika gazeti la New York Times Jumapili.

Man City kuivaa Real Madrid-UEFA.


Michuano ya klabu bingwa barani Ulaya hatua ya Nusu fainali inaendelea tena leo ambapo Manchester City watamenyana na

Waziri wa Elimu Prof. Ndalichako atolea ufafanuzi sera ya Elimu Bure


Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Prof. Joyce Ndalichako, amewataka walimu na maafisa elimu kusimamia vyema majukumu yao na kuhakikisha utoaji elimu bora kwa wanafunzi ili kupata wataalamu watakaolisaidia taifa.

Waziri Ndalichako, ameyasema hayo Jijini Arusha, alipokutana na wakuu wa shule,maafisa elimu na watendaji wakuu wa idara za elimu ambapo amesisitiza nidhamu ili kusaidia matokea mazuri na ya haraka ya kuboresha elimu nchini.

Waziri Ndalichako, amesema kuwa wataalamu mbalimbali ambao wanahitajia katika idara mbalimbali katika kukuza maendeleo wote wanahitaji zaidi mchango wa sekta ya elimu katika kuwapata wataalamu hao.

Aidha katika ziara aliyoifanya katika mkoa huo wa Arusha, Waziri Ndalichako, ametoa ufafanuzi zaidi wa sera ya elimu bure ambapo amesema kuwa wazazi bado wanajukumu la kushirikiana na serikali katika kuwasadia watoto kupata elimu bora.

Prof. Ndalichako amesema serikali haijawazuia wananchi wanaotaka kuchangia sekta ya elimu kutokana na changamoto zilizopo lakini haiko tayari kuona mwanafunzi anarudishwa nyumbani kwa sababu ya michango ya aina hiyo.

Rais Magufuli kafanya uteuzi mwingine leo April 25 2016


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli leo tarehe 25 April 2016 amefanya uteuzi wa Makatibu Tawala wa Mikoa 26 ya Tanzania Bara. Taarifa iliyotolewa leo na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa

HABARI ILYOTUFIKIA HIVI PUNDE : MWANAMUZIKI PAPA WEMBA AMEAGA DUNIA.

Sunday, April 24, 2016

Wemba ameaga dunia
Nyota wa muziki wa Soukous ambaye ni raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo- Papa Wemba amefariki dunia
Papa Wemba ambaye jina lake halisi ni Jules Shungu Wembadio Pene Kikumba, alianguka na kufa jukwaani akiwatumbuiza maelfu kwa

WAKAZI WA MLANDIZI WASOGEZEWA HUDUMA ZA MAWASILIANO.


Wakaazi wa Mlandizi wasogezewa huduma za mawasiliano na Vodacom Tanzania


Wakazi wa Mlandizi

TAARIFA YA UFAFANUZI JUU YA TAARIFA YA NAFASI ZA KAZI.

Kanusho Kali Kutoka Mamlaka ya Mapato-TRA Kuhusu

UGANDA YATANGAZA RASMI KUTUMIA BANDARI YA TANGA.







Hatimaye Serikali ya Jamhuri ya Uganda imetangaza rasmi uamuzi wake wa kutumia Bandari ya Tanga nchini Tanzania kusafirishia mafuta ghafi yake.

Uamuzi huo umetangazwa na Mhe

BREAKING NEWS: MAJAMBAZI YAKAMATWA KARIAKOO MUDA HUU LIVE

Wednesday, April 20, 2016



BREAKING NEWS PRESIDENT MAGUFULI NEW DECISION TO HIS MINISTERS HE DECIDED THIS

SERIKALI YAKAMATA MZIGO MAANA WA TANZANITE UKITOROSHWA NJE.

Serikali imefanikiwa kuyakamatwa madini ya Tanzanite yenye thamani ya Sh2.5  bilioni yaliyokuwa njiani kusafirishwa nje ya nchi bila kulipiwa vibali kipindi cha Januari hadi Desemba mwaka jana.

Mwenyekiti wa zamani CHADEMA Mwanza, Adrian Tizeba ahamia CCM

Friday, April 15, 2016


Aliyekuwa Mwenyekiti wa chama cha Demokrsaia  na Maendeleo Chedema mkoa wa Mwanza Andrian Tizeba, leo amejiunga rasmi na CCM wilayani  Sengerema tawi la Lugata.


Tizeba ambaye alitangaza kujivua uanachama wa chadema Machi 29 mwaka huu baada ya kusimamishwa uongozi kwa muda wa mwaka mmoja, na kutangaza kuachana na siasa, amekabidhiwa kadi hiyo  na katibu wa tawi hilo Alfred Mwambala.

YANGA BINGWA! : NIYONZIMA AIPAISHA YANGA TAIFA.

Wednesday, April 13, 2016


Timu ya Yanga imeifunga timu ya mwadui ya mjini shinyanga bao 2 kwa 1  na kubakiza pointi moja tu kuwakamata vinara wa ligi hiyo Simba Sc walio na jumla ya pointi 57, huku yanga ikiwa na mchezo mmoja mkononi.

Breaking Newsssssssss.....MAJANGA! : HII NDIO HUKUMU ALIYOPEWA SAID KUBENEA


Hatimaye  hukumu ya kesi iliyofunguliwa na Jamhuri dhidi ya Saed Kubenea, Mbunge wa Jimbo la Ubungo  akidaiwa kumtolea lugha ya matusi Paul Makonda, Mkuu wa Wilaya ya Kindononi imefika tamati.

Haya Hapa Magazeti ya Leo Tz Jumatano,April 13,2016- Udaku,Michezo na Hard News



Dereva Teksi Atiwa Mbaroni Kwa Kubaka Mteja Wake Usiku



DEREVA teksi katika Manispaa ya Iringa, Elain Mahenge (27), anashikiliwa na polisi mkoani Iringa kwa tuhuma za kumbaka mteja wake. 


Mahenge, Mkazi wa Semtema, Kihesa katika Manispaa ya Iringa, anadaiwa alikutwa akifanya kitendo hicho dhidi ya mteja wake saa 3:45 usiku. 


Kitendo hicho cha ubakaji kimetokea ikiwa imepita takriban miezi miwili, tangu Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Iringa, kutoa elimu kwa wananchi wa Kihesa juu ya kuwafichua watu wanaodaiwa kufanya vitendo vya ubakaji. 


Elimu hiyo ilitolewa kutokana na kuripotiwa kukithiri kwa vitendo hivyo, ikiwamo dhidi ya watoto wa kike na kuwalawiti watoto wa kiume, huku zaidi ya watu 10 wakiwa wameshakamatwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kujihusisha na unyama huo. 


Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Peter Kakamba, alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea Jumapili iliyopita, katika eneo la Kihesa. Alisema mtuhumiwa alikutwa akimbaka mteja wake huyo, ambaye ni mkazi wa Mgololo, Mufindi mkoani Iringa. 


Kakamba alisema mteja huyo alimkodi dereva huyo, baada ya kushuka kwenye gari katika kituo kikuu cha mabasi cha Iringa na kumtaka ampeleke kwenye nyumba ya kulala wageni iliyoko Kihesa. 


“Inadaiwa dereva teksi huyo alimchukua stendi hapo na kwenda alikoambiwa ampeleke lakini alipofika njiani kwenye giza alisimama na kisha kumbaka binti huyo,” alisema. 


Kamanda Kakamba alisema wakati dereva huyo akiendelea kufanya kitendo hicho, binti huyo alipiga kelele ambazo zilisikika na askari polisi ambao waliokuwa doria usiku huo na wakati polisi wanafika eneo la tukio tayari mtuhumiwa alikuwa ameshamaliza kufanya kitendo hicho na ndipo walipomkamata. 


Alisema kuwa mtuhumiwa yuko polisi na ushahidi umeonekana pale pale kwa kuwa mazingira na hali waliyokutwa nayo dereva na binti huyo, yalidhihirisha mtuhumiwa alitenda jambo hilo bila ya huruma tena kwa mteja wake, hivyo mtuhumiwa anatarajiwa kufikishwa mahakani wakati wowote kuanzia sasa. 


Aidha kamanda huyo aliwataka wakazi wa mji wa Iringa na viunga vyake kupanda teksi ambazo zimesajiliwa na si kupanda teksi bubu kama aliyokuwa ameipanda msichana aliyefanyikwa unyama huo.

THIS IS HOW TO CHECK YOUR PHONE IS FAKE OR NOT

Monday, April 11, 2016


MAKANISA YA KILOKOLE KUBANWA MBAVUNI.


 "Makanisa ya Kilokole kudhibitiwa mitaani",ni kwa kuimba wakati wa usiku.Hili ni tamko la Mkuu wa Mkoa wa Arusha kufunga vipaza sauti na kusababisha kero kwa wakazi wanaoishi jirani na nyumba hizo na wengi tulitaka vipaza sauti hivi vidhibitiwe kuondoa kero ya kelele

RIDHIWANI KIKWETE APONEA CHUPUCHUPU KUTUMBULIWA.



Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete, amekanusha taarifa zilizosambaa katika mitandao ya kijamii na kwenye vyombo vya habari kuwa yeye ni mmoja wa wamiliki wa kampuni ya Lugumi, inayodaiwa kupewa zabuni ya kufunga mashine za kuchukua alama za vidole kwenye vituo vya Polisi.

Ridhiwani ametajwa katika habari hizo kuwa ni mmiliki wa kampuni ya Lugumi pamoja na wamiliki wengine ambao ni Said Lugumi na aliyekuwa mkuu wa Jeshi la Polisi, Said Mwema.

Ridhiwani ambaye ni mtoto wa Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete amesema yeye hahusiki na kampuni yoyote ya Lugumi ingawa wana urafiki wa kawaida na mmiliki wa kampuni hiyo.

“Kwanza kabisa mimi si mmoja wa wamiliki wa kampuni hiyo, hilo ni jambo la msingi kabisa watu waelewe na sijawahi kufanya biashara yoyote na Lugumi. Said Lugumi ambaye ni mmiliki wa kampuni hiyo tunafahamiana naye na ni rafiki yangu,” alisema Ridhiwani.

Ridhiwani alisisitiza kuwa hana uhusiano wa kibiashara na mtu huyo na kwamba hafahamu ni kwa nini amehusishwa na kampuni ya Lugumi.

“Hapa ni watu tu wanaamua kuingiza tu maneno yao, haya maghorofa ninayotajwa kumiliki Dar es Salaam hata sijawahi kutembelea ujenzi wake, wameamua kuniingiza, Lugumi nafahamiana naye binafsi tu lakini wananiingiza,” alisema Ridhiwani.

Alisema jambo hilo bado liko ndani ya Kamati ya Bunge na baadae ameliona kwenye magazeti ya juzi kuwa Jeshi la Polisi litatoa taarifa yao, hivyo asingependa kulizungumzia kwa undani.

Hivi karibuni Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) ilitoa siku saba kwa Jeshi la Polisi nchini kupeleka mkataba walioingia baina yao na Kampuni ya Lugumi.

Kamati hiyo ilipokutana na Jeshi hilo kupitia taarifa ya hesabu zao za mwaka 2013/14 zilizokaguliwa na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Aeshi Hilaly alisema jeshi hilo mwaka 2011 liliingia mkataba na kampuni hiyo kwa ajili ya kufunga mashine za kuchukua alama za vidole katika vituo vya Polisi vya wilaya nchi nzima ambavyo viko 108.

Alisema mkataba huo ulikuwa wa Sh bilioni 37 pamoja na kodi na kwamba hadi sasa kampuni hiyo imeshapewa asilimia 99 ya fedha zote ili hali vituo vilivyofungwa mashine hizo ni 14 tu, kati ya vituo vyote 108.

Ridhiwani alisema angependa jamii ifahamu kuwa hana uhusiano na kampuni hiyo kwa kuwa hafahamu kabisa hata malipo yaliyofanywa kati ya Serikali na kampuni ya Lugumi anasikia tu kama ambavyo watu wengine wamesikia

BAADA YA KUIONA YANGA JUZI,KOCHA WA AL AHLY ANENA HAYA...!!



KOCHA wa timu ya soka ya Al Ahly, Martin Jol, amesema uimara wa safu ya ulinzi ya Yanga ilikuwa kikwazo kibwa kwao wasiibuke na ushindi juzi. Timu hizo ziliumana katika mchezo wa kwanza Raundi ya Pili Ligi ya Mabingwa Afrika na kumalizika kwa sare ya bao 1-1 katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Al Ahly walitangulia kupata bao la mapema mfungaji akiwa Amri Gamal dakika ya 11 kabla ya Yanga kusawazisha dakika ya 18 baada ya beki wa Ahly, Ahmed Hegazy kujifunga katika harakati za kuokoa.
Akizungumza baada ya mchezo huo, Jol alisema ulikuwa mzuri vijana wake walicheza vizuri na kutengeneza nafasi nyingi za mabao, lakini kikwazo ilikuwa ni umaliziaji baada ya kazi nzuri ya mabeki wa Yanga.
“Mchezo ulikuwa mzuri na mgumu ingawa safu ya ulinzi ilifanya kazi nzuri kwa upande wa wenyeji, lakini kwa ujumla mchezo ulikuwa mzuri. Yanga ni timu inayocheza mpira mzuri wenye pasi nyingi na hii inatulazimu katika mchezo wa marudiano kutumia mipira mirefu ili tuweze kupata ushindi hata wa mabao 2-0, “ alisema Jol.
Kwa upande wake, kocha wa Yanga Hans Pluijm, alisema mchezo ulikuwa mgumu kwa sababu walikutana na timu bora Afrika ambayo inaundwa na wachezaji wenye uzoefu na vipaji vya hali ya juu.
Alisema ameona upungufu wa wapinzani wao na wanajipanga kwa ajili ya mchezo wa marudiano nchini Misri na kuahidi watajitahidi kupambana ili kupata bao la ugenini kama walivyofanya wapinzani Al Ahly.
“Nawapongeza vijana wangu walijitahidi kupambana, lakini bahati haikuwa kwetu ingawa tulicheza na timu bora Afrika yenye wachezaji wanye vipaji vya hali ya juu katika kuuchezea mpira.
 

Most Reading

Eckros Computer Lap 1

Eckros Computer Lap 1

About ETC College

Eckros Tourism College (ETC) started admitting the first intake of students in January 2013. The college falls under tertiary higher education and training as stipulated in education and training policy of 1995.
Also the college administer Distance Learning Programmes, Evening classes, weekend classes, study tours and researchs programmes
Admission Process
New admission into the College is effected twice a year in January-July and July-December.

WALIO PITIA BLOG YETU