Na Erick Mlelwa,Njombe
Siku chache baada ya kuripotiwa taarifa za mwanafunzi kushambuliwa kupigwa na walimu katika shule ya Mbeya day jijini Mbeya tukio la aina hiyo limemkuta mwanafunzi mwingine wa shule ya sekondari ya Mbogamo ya mjini Njombe ambaye ameshambuliwa kwa kupigwa mpaka kupoteza fahamu na
kulazwa katika hospitali ya mkoa huo na walimu 6 akiwemo mkuu wa shule hiyo Bi Helmina Mgaya.
Mwanafunzi huyo Elizabert Simfukwe wa kidato cha nne anaye kadiriwa kuwa na umri wa miaka 19 anadaiwa kufanyiwa kitendo hicho cha kikatili tangu Octoba 6 mwaka huu ambapo adhabu hiyo ameipata baada ya kukutwa na simu ya mkononi katika begi lake kinyume na sheria za shule.
Kwa mujibu wa diwani wa kata ya Ramadhani George Sanga ambako shule hiyo ipo amesema kuwa walimu hao walifikia hatua ya kumfanyia hivyo mwanafunzi wakimtaka aeleze matumizi ya simu hiyo.
Kumekuwa na usiri mkubwa kwa mamlaka za serikali kutoa ushirikiano kwa wandishi wa habari juu ya tukio hili likiwemo jeshi la polisi na idara ya elimu ambapo hata uongozo wa hospitali ya mkoa wa njombe kibena unaeleza kuwa umezuiliwa kutoa taarifa hizo na utawala wa ngazi za juu.
Lakini hata hivyo mkuu wa wilaya ya Njombe Bi Ruth Msafiri ambaye yuko nje ya wilaya kikazi amekiri kwa kwa njia ya siku kuwa na tarifa za shambulio hilo ameagiza walimu waliohusika kuendelea kushikiwa na jeshi la polisi mpaka sheria ichukue mkondo wake
Chanzo: ITV
No comments:
Post a Comment