Madereva na wasidizi wa wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya mbalimbali waolikuwa tayari wameshafika mkoani Simiyu kwaajili ya kusherehekea kilele cha mbio za mwenge, wameeleza kuumizwa na agizo la Rais John Magufuli la kurejesha fedha za kujikimu.
Baadhi wamesema kuwa hawana uwezo wa kuzirejesha fedha hizo kwani hawakuwaomba kufanya safari hizo kwa kuwa ilikuwa sehemu ya
kazi zao kwahiyo kiasi cha fedha hizo walizitumia kama walivyokubaliwa na ofisi kuwawezesha na kufika katika eneo hilo.
“Sisi hatukuomba kuja Bariadi kwenye sherehe za mbio za Mwenge wa uhuru, tuliambiwa kuja na tukapewa fedha ambazo tumezitumia kwa mujibu wa mahesabu ya matumizi tuliyoandikiwa kwasababu ilibidi tule na kulala kwenye nyumba za wageni,tutapata wapi hela za kuzirudisha, hapo sisi kosa letu liko wapi,”? alihoji mmoja wa madereva aliliambia gazeti la The Citizen.
“Ili nibidi nilipe chumba kwa siku 7 ambazo nilitarajia kuishi hapa kama nilivyotumwa kwa uhaba wa vyumba,sasa naanzaje kumwambia mmenyewe arudishe fedha yote ili niirejeshe ofisini ?alihoji.
Wiki iliyopita Rais John Magufuli alisitisha safari ya viongozi wa mikoa na wilaya kwenda Simiyu kwenye kilele cha mbio za Mwenge na kuwataka wale waliokwisha chukua posho kuzirejesha.
No comments:
Post a Comment