ECKROS SCHOOL OF JOURNALISM

eckroscollege. Powered by Blogger.

Blogroll

About

Habari za Mahusiano Kila siku

JOURNALISM STUDENTS AT ETC COLLEGE

JOURNALISM STUDENTS AT ETC COLLEGE

ETC RADIO ONLINE LIVE

http://wwweckrosnewsblogspo.radio12345.com/

WACHINA WAKAMATWA KWA KUITIA HASARA SERIKALI YA BILIONI MOJA

Thursday, March 10, 2016



BUKOBA,Kagera

 WASHITAKIWA wanne wakiwemo raia wawili wa China, wamepandishwa kizimbani wakikabiliwa na mashitaka 16 yakiwemo ya wizi, kughushi nyaraka na kulisababishia Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO),wilayani Karagwe mkoani Kagera, hasara ya zaidi ya sh. bilioni moja.

Wakili Mkuu wa Serikali, Hashimu Ngole, amewataja washitakiwa hao ambao ni Wang Lei aliyekuwa Meneja wa Mradi wa ujenzi wa barabara ya Kyaka Bugene , Zhang Shuaitong, aliyekuwa mfanyakazi wa Kampyni ya Chiko .

Ngole amewataja wengine kuwa ni aliyekuwa Meneja wa TANESCO wilayani Karagwe, Issack Tibita na Olver Mushumbusi aliyekuwa Meneja Msaidizi wa shirika hilo wilayani hapo.

Washitakiwa hao wamepandishwa kizimbani leo katika Mahakama ya Wilaya ya Bukoba, mbele ya Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Charles Uiso na kusomewa mashitaka yanayowakabili.

Ngole amedai washitakiwa hao walikula njama na kughushi 


nyaraka mbalimbali zilizowasababishia kujipatia kiasi hicho cha fedha kinyuma cha sheria wakati wakitambua kuwa ni watumishi wa umma.
 
Amedai kati ya mwaka 2011 na mwaka 2014 washitakiwa hao walitenda makosa hayo ya kujipatia kiasi hicho cha fedha kutokana na mamlaka walizokuwa nazo katika eneo la Kayanga wilayani Karagwe.
 
Wakili huyo amesema kuwa fedha hizo ilitengwa na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) na kuilipa Kampuni ya Chiko ya China iliyokuwa ikijenga mradi wa barabara kutoka Kyaka hadi Bugene.

Barabara hiyo ilikuwa ni ahadi ya Rais mstaafu, Jakaya Kikwete, ambapo kampuni hiyo ilipaswa kulipa kiasi hicho cha fedha kwa TANESCO ili kuwawezesha kuondoa miundombinu iliyokuwa katika maeneo ya mradi huo.
 
Ngole amedai kuwa washitakiwa hao baada ya kupokea kiasi hicho cha fedha hawakuweza hakukulilipa shirika hilo, badala yake  walighushi hundi na kuziiba fedha hizo na kusababishia hasara  TANESCO ya zaidi ya sh. bilioni moja.
 
Amesema kuwa  upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na washitakiwa walikana mashitaka hayo na walirudishwa rumande. Kesi hiyo itatajwa Desemba 7, mwaka huu.

Hakimu Mfawidhi amesema mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza kesi wala kutoa dhamana kwa washitakiwa.

No comments:

Post a Comment

 

Most Reading

Eckros Computer Lap 1

Eckros Computer Lap 1

About ETC College

Eckros Tourism College (ETC) started admitting the first intake of students in January 2013. The college falls under tertiary higher education and training as stipulated in education and training policy of 1995.
Also the college administer Distance Learning Programmes, Evening classes, weekend classes, study tours and researchs programmes
Admission Process
New admission into the College is effected twice a year in January-July and July-December.

WALIO PITIA BLOG YETU