Habari za Mahusiano Kila siku
JOURNALISM STUDENTS AT ETC COLLEGE
ETC RADIO ONLINE LIVE
http://wwweckrosnewsblogspo.radio12345.com/
NAIBU WAZIR MAMBO YA NJE DR SUSAN KOLIMBA AMWAGA MISAADA UWT ,WAZEE NA WALEMAVU NJOMBE
Friday, March 11, 2016
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Dokta Susan Kolimba Ambaye Pia ni Mbunge wa Viti Maalumu CCM Mkoa wa Njombe amehitinisha ziara yake mkoani njombe kwa kufanya kikao na baraza la umoja wa wanawake Tanzania UWT mkoani humo ambapo ameendelea kusisitiza wanawake hao kuweka nguvu katika usimamizi miradi ya maendeleo ya umoja huo pamoja na kuanzisha miradi mipya itakayo kuza uchumi kwa haraka zikiwemo mashine za kusaga na kukoboa alizowapa
Ziara hiyo ya siku nne iliyolenga kuyafikia makundi mbalimbali wakiwemo walemavu na wazee pamoja na kutatua baadhi ya changamoto zinazo wakabili imeonekana kuwanufaisha walengwa kwa kuwa sehemu kubwa ya changamoto
zimepatiwa ufumbuzi kwa muda mfupi kama kuwapa misaada ya chakula mavazi na vifaa vya ujenzi kwaajili ya kukamilisha ukarabati wa majengo wanayioishi
DR Kolimba pia ametumia ziara hiyo kutekeleza baadhi ya ahadi alizo ahidi kwa wananchi kipindi cha kampeni za uchaguzi mwaka jana ambapo akiwa wilayani ludewa ametoa vifaa kwaajili ya kukarabati soko wilayani humo kufuatia maombi ya wananchi
Baadhi ya wanufaika na misaada hiyo akiwemo Katibu wa ccm wilya ya ludewa Lusiano Mbosa na diwani wa kata ya ludewa mjini bi Monica Mchilo wamesema kuwa msaada huo wa vifaa vya kukarabati soko wilayani humo utainufaisha jamii nzima huku wakionya uongozi wa soko kutumia vifaa walivyopewa kama ilivyokusudiwa
Wakizungumzia misaada iliyotolewa na mbunge huyo mteule wa viti maalumu kwa wilaya nne za mkoa wa njombe viongozi wa umoja wa wanawake Tanzania UWT akiwemo Rosemary Lwiva mwenyekiti na mjumbu wa baraza kuu taifa Bi Farida Nurdini wamesema kwa utendaji kazi mzuri alioanza nao wanaamini kuwa mkoa wa njombe utakuwa na maendeleo makubwa
Kwa upande wao baadhi ya wazee waliopatiwa misaada pamoja na wawakilishi wa vituo vya watoto wenye ulemavu katika halmashauri zilizopatiwa ziara walikuwa na haya ya kusema
misaada Yenye thamani ya zaidi ya shi lingi milion 18 imetolewa kwa wilaya zote nne kwa umoja wa wanawake Tanzania UWT Pamoja na kwa wazeena walemavu
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment