Serikali imesema inakusudia kupunguza tatizo la ajira kwa vijana mkoani njombe kwa kufanya maandalizi ya vijana kuchukua fursa za ajira katika migodi ya makaa ya mawe na chuma wilayani ludewa ambayo inakadiriwa kutoa fursa ya ajira kwa wazawa zaidi ya elfu 30
Kauli hiyo imetolewa na waziri wa sera bunge kazi vijana ajira na walemavu mjini njombe Jenista mhagama wakati akizungumza na makundi mbalimbali ya vijana wakiwemo madereva bodaboda ambapo amezitaka halmashaurizote za wilaya kufungua saccos kwaajili ya kuwakopesha vijana kupitia mapato ya ndani na mfuko wa maendeleo ya vijana
waziri mhagama Amesema kuwa serikali inataraji kuinua uchumi wa wananchi wa kipato cha chini na itahakikisha vijana wanapata mikopo kwa masharti nafuu ili waweze kujiajiri huku akiwekea mfano kundi kubwa la madereva wa bodaboda ambao wakiwezeshwa wanaweza kumiliki pikipiki zao
Katika mkutano huo Amepokea malalamiko kutoka kwa wanachama wa kikundi cha vikoba Mkoa wa njombe kupitia mratibu wao BW Betram Ngimbuchi ambao wanaonekana kutapeliwa na muasisi wa vicoba Hapa nchini wanamuomba waziri kuwasaidia waweze kurejeshewa fedha zao ambazo ziko hatarini kupotea
Pamoja kuahidi kulifanyia kazi Sakata hilo waziri jenista amemuagiza mkuu wa mkoa pamoja na wakurugenzi kufuatilia fedha za wananchi hao zirudishwe mara moja na kueleza kuwa serikali imeanzisha utaratibu mwingine wa kusimamia mfumo wa vikoba humu nchini ambapo wanachama watapatiwa mikopo kupita bank ya posta na sio appex
No comments:
Post a Comment