Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Nchini Tanzania Bi,Jenister Mhagama
Waziri Jenister Mgahama katika mkutano na wajasiriamali mjini Njombe
Mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi ya mkoa wa Njombe ambayepia ni Mkuu wa Mkoa huo Dkt Rehema Nchimbi amesema ni marufuku kwa watumishi katika halmashauri kulipana posho katika vikao vya kujadfili matatizo ya wananchi.
kauli hiyo ameitoa leo katika kikao na wajasiriamali wadogo wadogo mjini Njombe wakiwemo mama lishe,vikoba,madereva boda boda ambapo pia pamoja na mambo mengine ametoa siku 7 kuanzia jumatano ya leo mpaka wiki ijayo kuwa tayari halmashauri zote zimeunda kamati za kushughulikia masuala ya ajira kwa vijana.
Naye Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Nchini Tanzania Bi, Jenista Mgahama ameziagiza halmashauri zote mkoani Njombe kuhakikisha zinateua wataalamu wa kusimamia uwezeshawaji wa ajira kwa vijana katika halamshauri zote.
Baada ya uteuzi huo amesema baraza la uwezeshai ajira taifa kwa wananchi kuanzia mwezi wa 3 mwaka huu litapita kutoa mafunzo kwa viongozi hao watakaoteuliwa.
Akiwa mjini Njombe Mh,Mgahama amesema sasa ni wakati wa kila mwananchi kumiliki uchumi wake mwenyewe na kuachana na mambo ya kumfanyia kazi mtu mwingine huku wenyewe maisha yao yakiendelea kuwa duni.
Anasema kundi la boda boda ni wakati wa kupewa kipaumbele na kuachana na kendesha boda boda ambazo siyo mali zao ambapo pia pamoja na mambo mengine aiagiza serikali mkoani Njombe kuona namna nzuri ya kulisaidia kundi hili ili liweze kujiinua kiuchumi.
Baada ya agizo hilo akasimama mwenyekiti wa boda boda mkoa Njombe ambaye anasema kuna zaidi ya madereva boda boda 600 lakini wanaomiliki boda boda zao hata 30 hawafikii jambo ambalo wanasimama kuomba msaada zaidi kupitia katika vyama vya ushirika ili viwasaidie kupewa mikopo yenye riba nafuu.
Baada ya agizo hilo la Mheshimiwa waziri naye mkuu wa mkoa wa Njombe Dkt Rehema Nchimbi ametoa siku 7 kwa halmashauri zote mkoani Njombe kuwa tayari zimeunda mabaraza hayo ya kushugulikia masuala ya ajira kwa vijana na wananchi kwa ujumla kuwasilisha ofisini kwake.
No comments:
Post a Comment