Wachezaji wa timu mbili hasimu nchini Ugiriki wamesusia mechi wakipinga ongezeko la vifo vya wahamiaji wanaozama wakijaribu kuingia nchioni humo kukwepa vita Syria na Iraq.
Wachezaji hao wa timu ya AEL Larissa na wenzao wa timu ya Acharnaikos waliketi chini pindi refarii alipopuliza kipenga cha kuanzwa kwa mechi hiyo ya ligi.
Tukio hilo lililodumu kwa zaidi ya dakika mbili lilimwacha muamuzi asijue la kufanya!
Hata ta hivyo alipoulizia cha mno akaelezewa kuwa muda mchache kabla ya mechi hiyo taarifa zilichipuka kuwa zaidi ya wahamiaji wengine 39 walikuwa wamekufa maji wakijaribu kuingia nchini humo wakitoroka vita.
Taarifa hiyo iliwaudhi sana na kuwachochea kuchukua hatua hiyo.
Wahamiaji hao walikuwa wametokea Uturuki wakijaribu kufika katika moja ya visiwa vya Ugiriki lakini mawimbi makali yakaifanya mtumbwi walimokuwa kuzama majini.
Timu ya AEL Larissa ilisema kuwa wachezaji wao walichukua hatua hiyo wakijaribu kuangazia macho ya ulimwengu na kila awaye yote kwa tatizo hilo la wahamiaji ambao wanazidi kufa maji kila kukicha wakitoroka vita.
Idadi kubwa ya wale wanaopoteza maisha yao baharini ni watoto wanawake na wazee.