ECKROS SCHOOL OF JOURNALISM

eckroscollege. Powered by Blogger.

Blogroll

About

Habari za Mahusiano Kila siku

JOURNALISM STUDENTS AT ETC COLLEGE

JOURNALISM STUDENTS AT ETC COLLEGE

ETC RADIO ONLINE LIVE

http://wwweckrosnewsblogspo.radio12345.com/

Valentines's Day: Asili na historia yake hadi kusisimua Ulimwengu

Tuesday, February 13, 2018


Image result for historia ya siku ya wapendanao
Siku ya Valentines Day asili yake ni kutoka Dola ya Warumi. Ni siku ya kumbukumbu (memorial day) na sehemu nyingine ni (festum) maana yake siku kuu ya daraja la kwanza kwa
kumkumbuka Padre Valentine aliyeuawa na utawala wa kirumi 

Sababu ya kutetea waumini wake kufunga ndoa badala ya kuishi na vimada tu. Lakini sikukuu hiyo imeenea sana katika nchi za magharibi na baadaye karibu sehemu kubwa ya ulimwengu kuisherehekea kama siku yamapenzi kinyume cha dhamira ya Mt. Valentine.

Watawala wa dola ya kirumi walikuwa na fikra za kueneza dola ya kirumi duniani kote na hivyo vijana hawakutakiwa kuoa, ili wawe huru muda wote kwenda vitani kupigania nchi. 

Wakioa hawangekuwa na uhuru wa kwenda vitani bali kuwa na famiia zao. Vijana wengi wakawa na mtindo wa kuwa na vimada tu kitu ambacho kanisa lilikukwa linapinga.

Padre Valentine ambaye alikuwa Roma akawa anawahimiza vijana kufunga ndoa badala ya kufanya ngono bila ndoa kwani ni dhambi na kitu kisichokubalika mbele ya Mungu.

Akawa anafungisha ndoa kwa siri kwenye makatakombe (mahandaki chini ya kanisa ambako kuna sehemu za ibada kwa watu wachache), alifanya hivyo kwa vile kufunga ndoa hadharani ilikuwa ni kukiuka amri ya wakuu wa dola ya kirumi.

Baadhi ya watu walifichua siri hiyo, hivyo Padre Valentin alishikwa na dola ya Warumi na kuuawa kama shahidi mfia dini kwa ajili ya kutetea waamini wake wafunge ndoa badala ya maisha ya ngono zembe bila ndoa.

Wakristo wakawa siku ya kumkumbuka Padre Valentin kama mfia dini sababu ya kutetea maisha ya wanakanisa kuwa wanandoa. Ikaenea katika kanisa nchi za magharibi na hata duniani ambako wanakanisa wanamkumbuka Mt. Padre Valentin.

Baadaye ikapokeleka na watu hata wasio na imani ya kikristo kama ni siku ya kufanya kumbukumbu kwa Mt. Valentin kama mtetezi wa Ndoa.

Maudhui ya siku hiyo kwa wasiowanakanisa imechukua maana nyingine ya kwamba ni siku ya wapendanao hata kwa wasio wanandoa bali mradi wanapendana, kitu ambacho ni kinyume cha malengo ya mfia dini Mt. Padre Valentin aliyetaka vijana wafunge ndoa badala ya kuwa na hawara tu (vimada).

No comments:

Post a Comment

 

Most Reading

Eckros Computer Lap 1

Eckros Computer Lap 1

About ETC College

Eckros Tourism College (ETC) started admitting the first intake of students in January 2013. The college falls under tertiary higher education and training as stipulated in education and training policy of 1995.
Also the college administer Distance Learning Programmes, Evening classes, weekend classes, study tours and researchs programmes
Admission Process
New admission into the College is effected twice a year in January-July and July-December.

WALIO PITIA BLOG YETU