Habari za Mahusiano Kila siku
JOURNALISM STUDENTS AT ETC COLLEGE
ETC RADIO ONLINE LIVE
http://wwweckrosnewsblogspo.radio12345.com/
MKUTANO WA MAWAZIRI WA SEKTA YA MALIASILI NA MAZINGIRA WA JUMUIYA YA AFRIKA YA MASHARIKI WAFANYIKA LEO JIJINI ARUSHA
Sunday, February 11, 2018
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (kushoto) akiteta jambo na Waziri wa
Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba wakati wa mkutano wa tano wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Maliasili na Mazingira wa Nchi za Jumuiya ya Afrika ya Mashariki uliohitimishwa leo katika ukumbi wa EAC jijini Arusha. Mkutano huo ulilenga kujadili na kusaini makubaliano mbalimbali ya namna bora ya kusimamia sekta hizo katika nchi wanachama.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba (kulia) akisaini baadhi ya makubaliano yaliyofikiwa katika mkutano wa tano wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Maliasili na Mazingira wa Nchi za Jumuiya ya Afrika ya Mashariki uliohitimishwa leo katika ukumbi wa EAC jijini Arusha. Mkutano huo ulilenga kujadili na kusaini makubaliano mbalimbali ya namna bora ya kusimamia sekta hizo katika nchi wanachama. Wanaoshuhudia ni Mawaziri wa Mazingira kutoka Uganda na Kenya.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia), Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba (wa pili kulia) na Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Bi. Katerina Rangnitt wakiangalia baadhi ya michoro ya katuni za kuhamasisha uhifadhi wa mazingira muda mfupi baada mkutano wa tano wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Maliasili na Mazingira wa Nchi za Jumuiya ya Afrika ya Mashariki uliohitimishwa leo katika ukumbi wa EAC jijini Arusha. Mradi huo ya katuni unafadhiliwa na Serikali ya Sweden kwa ushirikiano na Serikali ya Tanzania.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment