ECKROS SCHOOL OF JOURNALISM

eckroscollege. Powered by Blogger.

Blogroll

About

Habari za Mahusiano Kila siku

JOURNALISM STUDENTS AT ETC COLLEGE

JOURNALISM STUDENTS AT ETC COLLEGE

ETC RADIO ONLINE LIVE

http://wwweckrosnewsblogspo.radio12345.com/

UJENZI RASMI BOMBA LA MAFUTA KUANZA MEI

Friday, February 2, 2018

Na Veronica Simba – Dodoma
Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Nishati na Kampuni ya Total wamekubaliana kuharakisha hatua zote za awali katika Mradi wa Bomba la Mafuta kutoka Uganda hadi Hoima Tanga ili shughuli za ujenzi rasmi zianze mwezi Mei mwaka huu.
Makubaliano hayo yalifikiwa Alhamisi, Februari 1, wakati Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani alipokutana na uongozi wa juu wa kampuni hiyo wizarani Dodoma.
Aidha, makubaliano mengine yaliyofikiwa katika kikao hicho ni kuwa kazi za awali za maandalizi ya ujenzi ziwe zimekamilika ifikapo mwezi Machi mwaka huu.
“Ni lazima tuharakishe mchakato huu kama Mheshimiwa Rais Magufuli alivyoagiza. Hivyo, tumekubaliana kwamba shughuli zote za maandalizi ziwe zimekamilika ifikapo Machi mwaka huu ili kuwezesha shughuli rasmi za ujenzi wa Bomba kuanza mwezi Mei,” alifafanua Waziri Kalemani.
Vilevile, katika kikao hicho, Rais wa Kampuni ya Total sehemu ya Afrika, Guy Maurice ambaye alikuwa kiongozi wa Ujumbe huo, alibainisha nia ya kampuni yake kuwekeza katika shughuli nyingine mbalimbali zinazohusiana na Mradi wa Bomba jambo ambalo alisema litainufaisha zaidi Tanzania. 
Mbali na makubaliano yote yaliyofikiwa, Waziri Kalemani pia alisisitiza kuwa ni muhimu kampuni ya Total iwasilishe Mpango-Kazi wake wizarani mapema iwezekanavyo ili utumike kama mwongozo-rejea katika kutathmini utekelezaji wa Mradi huo mkubwa.
Kampuni ya Total ndiyo mwekezaji katika utekelezaji wa Mradi wa ujenzi wa Bomba la Mafuta kutoka Uganda hadi Hoima, Tanga.
Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. Hamisi Mwinyimvua, Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi wa Wizara Lusius Mwenda, Mkurugenzi wa Sera na Mipango Haji Janabi na maafisa wengine waandamizi kutoka wizarani.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, akisalimiana na Ujumbe kutoka Kampuni ya Total kabla ya kuanza kwa kikao baina yao kujadili utekelezaji wa Mradi wa Bomba la Mafuta kutoka Uganda hadi Hoima-Tanga. Kikao hicho kilifanyika Makao Makuu ya Wizara mjini Dodoma, Februari Mosi, mwaka huu.

No comments:

Post a Comment

 

Most Reading

Eckros Computer Lap 1

Eckros Computer Lap 1

About ETC College

Eckros Tourism College (ETC) started admitting the first intake of students in January 2013. The college falls under tertiary higher education and training as stipulated in education and training policy of 1995.
Also the college administer Distance Learning Programmes, Evening classes, weekend classes, study tours and researchs programmes
Admission Process
New admission into the College is effected twice a year in January-July and July-December.

WALIO PITIA BLOG YETU