ECKROS SCHOOL OF JOURNALISM

eckroscollege. Powered by Blogger.

Blogroll

About

Habari za Mahusiano Kila siku

JOURNALISM STUDENTS AT ETC COLLEGE

JOURNALISM STUDENTS AT ETC COLLEGE

ETC RADIO ONLINE LIVE

http://wwweckrosnewsblogspo.radio12345.com/

Mwanasheria mkuu wa Kenya Githu Muigai ajiuzulu

Tuesday, February 13, 2018

Aliyekuwa mwansheria mkuu Githu Muigai.

Aliyekuwa mwansheria mkuu Githu Muigai.
Mwanasheria mkuu wa Kenya, Githu Muigai, alijiuzulu siku ya Jumanne. Rais wa nchi hiyo, Uhuru Kenyatta, kupitia ujumbe wa Twitter, alisema
  ameshangazwa na hatua hiyo, lakini akamshukuru kwa huduma yake ya miaka sita na nusu kama mshauri mkuu wa sheria wa serikali.
Na akizungumza muda mfupi baadaye kutoka ikulu ya Nairobi, Kenyatta alisema kwamba amemteua jaji Paul Kihara Kariuki, kama mwanasheria mkuu mpya.
Hakuna maelezo zaidi yaliyotolewa kuhusu sababu ya kujiuzulu kwa Muigai.
Kujiuzulu kwake kumejiri huku serikali ikilaumiwa vikali kwa kukosa kutii amri za mahakama hususan kufuatia mzozo wa kisiasa unaoendelea nchini humo.
Alifahamika sana wakati wa kesi zilizowakumba rais Uhuru Kenyatta na naibu wake, William Ruto kwenye mahakama ya kimataifa ya uhalifu, ICC, mjini The Hague, Uholanzi, ambapo aliwatetea kwa dhati viongozi hao.
Muigai aliteuliwa kama mwanasheria mkuu na rais Kenyatta kufuatia uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2013, na kuchukua nafasi iliyokuwa imeshikiliwa kwa muda mrefu na Amos Wako.
Kabla ya kuwa mwanasheria mkuu, Muigai alifanya kazi kama mjumbe maalum wa umoja wa mataifa kuhusu ubaguzi wa rangi na unyanyasaji.

No comments:

Post a Comment

 

Most Reading

Eckros Computer Lap 1

Eckros Computer Lap 1

About ETC College

Eckros Tourism College (ETC) started admitting the first intake of students in January 2013. The college falls under tertiary higher education and training as stipulated in education and training policy of 1995.
Also the college administer Distance Learning Programmes, Evening classes, weekend classes, study tours and researchs programmes
Admission Process
New admission into the College is effected twice a year in January-July and July-December.

WALIO PITIA BLOG YETU