Waziri
wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina ameliomba radhi Bunge na wabunge kwa
kile kilichotokea jana Juni 19, 2018 kwa maofisa wa wizara yake kuingia
bungeni bila ridhaa.
Akitoa
taarifa ya Serikali bungeni leo Juni 20 kuhusu kilichotokea jana, Mpina
amesema sehemu ya utekelezaji wa shughuli za wizara ikiwamo operesheni
sangara ambayo jana ilitendeka bungeni, itaendelea lakini kwa bahati
mbaya utekelezaji huo haukuzingatia tararibu za Bunge.
Amesema Juni 19 akiwa katika mgawaha wa Bunge aliona samaki wa sato akahisi wapo chini ya sentimita 25.
“Nikamuagiza
katibu wangu, kwamba wakaguzi wakajiridhishe na samaki hao na wakaguzi
walimuhoji muuzaji mgahawa ambaye alikiri ni wachanga walikuwa chini ya
sentimita 25,” amesema.
Ameongeza:
“Napenda kukiri kwamba watumishi katika kutekeleza kazi hiyo waliingia
bila kibali, kupima chakula kilichopikwa na kwa taratibu hizo, wizara
inaliomba radhi Bunge lako tukufu na wewe mwenyewe.”
Mara
baada ya kauli hiyo, Spika Job Ndugai amesema anamshukuru Mpina kwa
maelezo yake lakini akaongeza kuwa, kilichofanywa na maofisa hao ni
dharau ya juu.
“Tumshukuru
waziri kwa maelezo aliyoyatoa, lakini kwa waziri mkuu tunasikitishwa
sana na kilichotokea, sisi si Bunge pekee duniani, sisi ni jumuiya ya
kimataifa, wenzetu wakisikia kuna waziri na maofisa walichofanya ni
dharau ya juu sana,”amesema.
Amesema
linapotokea kosa la jinai katika eneo la Bunge, kamanda wa polisi ana
wajibu wa kumjuluisha Spika kwani Bunge halilindi Spika.
“Wapimaji
wa wizara wanapima samaki mikono haina hata gloves, mikono wazi,
wanashika shika, si wao peke yao, wamealika na waandishi wa habari,
yaani ni kama mpango fulani wa kuliweka Bunge kusipostahili, kwa hiyo
aaaaaaaa, kwa kawaida naomba tukubaliane nami, ukiwa umekasirika sana
unapaswa kusamehe,”amesema.
No comments:
Post a Comment