Msanii
wa muziki wa kizazi kipya Abubakar Chande maarufu kama 'Dogo Janja'
ambaye pia ni mume wa msanii wa filamu nchini Irene Uwoya amedai katika
ndoa yao yeye ndio mwanaume na mwenye sauti ya kutoa maamuzi ya jambo
lolote tofauti na watu wanavyomfikilia.
Dogo
Janja amebainisha hayo wakati alipokuwa anazungumza na kituo cha EATV
baada ya kuwepo kwa tetesi za kipindi kirefu zilizokuwa zinadai
Janjaroo hana maamuzi yoyote katika ndoa yake kwa kuwa mwenye sauti ya
kuamua jambo lolote ni mke wake Irene Uwoya.
"Ukiwa
hauna maamuzi au sauti kwa mke wako wa halali ni kitu kizuri sana
tofauti ukiwa hauna sauti kwa hawala. Mimi nina mtii mke wangu naye pia
anafanya hivyo, kwenye ndoa yangu nina simama kama baba", amesema Dogo
Janja na kuongeza;
"Watu
wengi wanachukulia mambo kwa juu juu tu kwa mzaha, mimi nina sauti kwa
mke wangu ninaweza kumwambia leo usitoke na huwa atoki au asifanye kitu
fulani na akanisikiliza, 'so' sio kila jambo nitakalo mkataza basi
nitangaze ila mpaka mke wangu akifanya jambo fulani mjue nina taarifa
nayo na ninaelewa. Ndoa ni taasisi kubwa sana tofauti na watu ambao wapo
tu mtaani wanatoa maamuzi yao bila ya kuelewa".
Kwa
upande mwingine, Dogo Janja amedai watu wengi wamekuwa wanaongelea
kuhusiana na ndoa yake kwenye mitandao ya kijamii bila ya kuwa na
ufahamu wa aina yoyote juu ya taasisi hiyo ambayo ina uwanja mpana ndani
yake.
No comments:
Post a Comment