ECKROS SCHOOL OF JOURNALISM

eckroscollege. Powered by Blogger.

Blogroll

About

Habari za Mahusiano Kila siku

JOURNALISM STUDENTS AT ETC COLLEGE

JOURNALISM STUDENTS AT ETC COLLEGE

ETC RADIO ONLINE LIVE

http://wwweckrosnewsblogspo.radio12345.com/

TAASISI ZINAZOHAMASISHA NA KUTANGAZA USHOGA KUFUTIWA USAJILI TANZANIA

Wednesday, December 21, 2016


WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba ametaka apewe taarifa kuhusu taasisi na mashirika yasiyo ya kiserikali (NGO) wanaohamasisha au kutangaza ndoa za jinsia moja nchini ili azifutie usajili mara moja.
Aidha ametaka kutajwa kwa watu wanaojihusisha na vitendo hivyo ili wachukuliwe hatua za kisheria kwa kujihusisha na vitendo hivyo ambavyo vinapigwa vita dunia nzima.
Nchemba aliyasema hayo jana mjini Kibaha alipokuwa akizungumza na taasisi za Kijeshi za mkoa huo zikiwemo Uhamiaji, Polisi, Magereza na Zimamoto juu ya kujua changamoto mbalimbali zinazowakabili.Alisema kuwa taasisi hizo hazifai kwani zinafanya kazi ya laana ambayo ni kinyume cha maadili ya Kitanzania na hazistahili kuendelea kufanya kazi kwa upotoshaji huo.
“Leteni majina ya taasisi hizo ili tuzifute kwani hazistahili kuendelea kufanya jambo hilo ambalo ni laana na halipaswi kufumbiwa macho ndani ya jamii,” alisema Nchemba.
Kamanda wa polisi mkoani Pwani Bonaventura Mushongi alisema kuwa jeshi hilo linakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na upungufu wa vitendea kazi, ikiwa ni pamoja na magari
Mushongi alisema kuwa licha ya kukabiliwa na changamoto hizo wamekuwa wakikabiliana na uhalifu kwenye mkoa huo ambao umekuwa kimbilio la wahalifu kutoka mikoa jirani ya Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

 

Most Reading

Eckros Computer Lap 1

Eckros Computer Lap 1

About ETC College

Eckros Tourism College (ETC) started admitting the first intake of students in January 2013. The college falls under tertiary higher education and training as stipulated in education and training policy of 1995.
Also the college administer Distance Learning Programmes, Evening classes, weekend classes, study tours and researchs programmes
Admission Process
New admission into the College is effected twice a year in January-July and July-December.

WALIO PITIA BLOG YETU